Madhabahu Binafsi


Tu-palabra-me-da-vida-1024x706 Madhabahu Binafsi

Kila mtu anatakiwa kuwa na madhabahu yake mwenyewe mbali na madhabahu ya kuchangia na wengi.  Kuna madhabahu ya aina mbili . 

1.Madhabahu ya kiroho

2.Madhabahu ya kimwili

Huwezi kufanikiwa  kwenye madhabahu ya watu wote. Kumbuka ukitafuta pesa utapata . Ukimtafuta Mungu utafanikiwa.

Madhabahu ya kiroho.

Ni vema ukalinda sana moyo wako kuliko kitu chochote unachokilinda kwa maana ndiko huko zitokako chemchemi za uzima. Utakuta mtu analinda mali yake, analinda mume, mke, lakini anasahau madhabahu ya moyo wake.

Nafsi iliyoshiba hukinai sega la asali. Bali nafsi yenye njaa huona kila kitu kichungu kuwa ni kitamu.

1555604_Articolo Madhabahu Binafsi

Madhabahu ya Kimwili.

Unaweza kutengeneza madhabahu yako nyumbani . Ukayaheshimu kama unavyoheshimu ya mahali kwingine. Moyo ni jukwaa la taarifa. Madhabahu ni jukwaa la taarifa.

Taarifa za kiroho ndizo zinazotengeneza taarifa za kimwili, kama ni nzuri au mbaya. Ni vizuri kuwa makini na kitu gani unaongea , kitu gani unasikiliza, kitu gani unatazama. Ni kitu gani unaingiza ndani ya akili yako kila siku, ndani ya moyo wako kila siku.

IMG_6105-1024x576 Madhabahu Binafsi

Kuna mazingira mengine husababisha mtu ajione kuwa yuko salama lakini kumbe sio salama. Mithali 16:25.  Mtu anaweza kuona yuko njia sahihi  katika kufanya mambo yake lakini mwisho wake ukawa sio mzuri.

Ukiona magonjwa yanakufuatilia, na unaishi kwa vidonge angalia sana chanzo cha mapato yako.  Kama unafanya biashara ambayo inaumiza watu , hutumii muda wako vizuri kazini , kuwa makini , maana utavuna ulichopanda.

Nidhamu ya maisha ya kila mwanadamu ni kuchunga vitu anavyovifanya kila siku.  Chunga sana unachoongea, unachosikiliza, na unachokiangalia. chunga marafiki ulio nao. Ukitembea na Tajiri utakuwa tajiri. Ukitembea na mwenye Hekima utakuwa mwenye Hekima.

Ukichunga kinywa chako, utachunga maisha yako. Linda moyo wako linda akili yako kila siku. Unaruhusiwa kufikiri mambo mengi sana lakini huruhusiwi kusema yale unayofikiria. Kinywa chako ndio hatima ya maisha yako.  Mtu akiweza kuteka ufahamu wako  atakupepeta kama ngano. Tumia sana imani yako. Huwezi kuwa na imani halafu ukaishi tofauti na imani yako.

Kumbuka maisha sio biashara yako. Maisha ni biashara ya Mungu. Mukumbuke Mungu, Mshukuru Mungu, Msifu Mungu Kila Baada ya dakika 60.  Panda mbegu ya Muda kwa Mungu. Mzaliwa wa kwanza ni wa Mungu. Mpe Mungu dakika moja Kila inapofika saa kamili. Ikifika Dakika 59, Anza kumshukuru Mungu , Ombea watu, Omba mambo yako.

Mungu ni Alpha na Omega. Anapatikana mwanzo wa lisaa na mwisho, mwanzo wa wiki na mwisho, mwanzo wa mwezi na mwisho, mwanzo wa mwaka na mwisho wa mwaka.

Weka Agano na Mungu la kumshukuru kila  baada ya dakika 60. utaona jinsi Mungu anavyokuletea Nguvu mpya, Kibali, Ulinzi na Akili njema.

Mungu akubariki kwa kujifunza.

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Kufanya Ngono Bila Ufahamu Inaweza Kuumiza Mahusiano
Next Unawakumbuka Lakini Huwataki

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.