images-1 Maisha Hayakutokea Tu Kwetu.Mipenyo Inahitaji  Nguvu Mpya

Unaweza kubadilika bila ya kukua, lakini huwezi kukua  bila kubadilika.

Kamwe hutaweza kupita katika mto huo huo mara mbili na ukapita kwa usahihi, utahitaji umakini mkubwa.

Tunaishi katika Ulimwengu ambao mabadiliko yake  yana makosa. Mara utaambiwa utumie hiki, mara wengine kukuza miili , wengine kupunguza miili. Hayo yote yanapita. tuendelee na kilichopo, mto ambao unakupa  uwezo usioguswa na mtu mwingine. Uwe tayari  kuflow. Huu ni ushauri  mkubwa kwa wakati huu unapokaribia kumaliza mwaka 2017.

Mwezi ni mpya tena,  kila siku ni mpya. huoni? sasa fikiria hii sentensi  kwa muda mfupi hasa wakati huu tunapojiandaa kuingia mwaka mpya. Kila siku  na kila dirisha  lililopo lina Fursa mpya kwa ajili yako, uzoefu mpya, utasafiri,  utafanya mambo makubwa mapya. Ni juu yetu , kila mtu na kila siku, Ingawa, Ni kuamua kama  tutataka kutoka kwenye giza na kufuata mwanga wa jua au tutaendelea kujificha ndani kwa hofu mbalimbali za maisha.

Ni uamuzi wetu, ni majukumu yetu wenyewe. Na ukumbuke kuwa Ulimwengu tunaoishi utabadilika hata kama sisi hatutachagua kubadilika, Upende usipende. Kuna msemo unaosema kwamba, Kama unataka vitu vibaki kama vilivyo, Wakati huo kuna kitu kinabadilika, lazima kitabadilika.

sunrise-sky-blue-sunlight-67832 Maisha Hayakutokea Tu Kwetu.Mipenyo Inahitaji  Nguvu Mpya

Njia nzuri ya kutambua ndoto yako ni kuamka kutoka usingizini. Amsha akili. Kwa maneno mengine,  Siku zetu nzuri, miaka yetu mizuri, na maisha yetu bora yanaweza  kuamuliwa na kufanya kitu fulani. Lakini ukifanye kweli.

Kila mtu hatakiwi kuanza kujiuliza nini maana halisi ya maisha yake, Lakini, badala yake, atambue kwamba  maisha ni maamuzi. Weka utofauti. Kila mtu amekuwa akijiuliza kuhusu maisha yake na jibu lake ni rahisi,

Maisha ni kuishi wakati uliopo, Yaliopita yamepita, Yaliopo ndio mpango mzima, Yajayo huyajui. Hii yote ipo katika kuwajibika kwa mwanadamu.

RLRLArticle1Photo2 Maisha Hayakutokea Tu Kwetu.Mipenyo Inahitaji  Nguvu Mpya
Close-up of a mature couple smiling

Kwa hio kwa sababu ya kukaribia kwa mwaka mpya , Kitu gani unataka kufanya kwenye maisha yako?  Uko tayari kutoka nje  kwenye jua na kuifanya kila siku iwe  bora na yenye faida kwako, Na wewe mwenyewe uwe faida kwa siku hio?  Haijalishi  umejaribu kwa ugumu wa aina gani, Bado utakuwa na uhakika kwamba hutatembea kwenye mto huo huo mara mbili.

Kwa hio chukua hatua mpya ya Kumkumbuka Mungu, Kumsifu Mungu na Kumshukuru Mungu Kila baada ya dakika 60. Toa dakika moja kama mbegu katika ufalme wa Mungu . Anza kujifunza matumizi ya MUDA. Jipange upya kwa ajili ya kumpa Mungu muda wako japo kila saa dakika moja utakuwa umepanda .

Kasome , kwa wale wenye Biblia. Chukua mwongozo wa kuanza zoezi hili la kufungua mwaka mpya na mambo yako mapya.

Kumkumbuka Mungu. soma Kumb.Torati 8:18

Kama unataka kupata mipenyo kwenye kazi yako, ndoa yako, familia yako, biashara yako. Anza kufanya hili zoezi ambao limefungua wengi.

Zaburi 100:4

Zaburi 103:3

zaburi 23:1

Isaya 11:2

Wagalatia 5:22,23

Ufunuo 1.8

Ufunuo 5: 12

Sasa basi utafanyaje katika mistari hio ili uweze kupata mipenyo kwenye maisha yako. Nikukumbushe kuwa Mfalme Daudi alikuwa akimsifu Mungu  mara saba kwa siku  Zaburi 119: 164, alimshukuru Mungu  .Mara tatu kwa siku alimuomba Mungu Zaburi 55:17. Mara  Kumi kwa siku alikuwepo uweponi mwa Mungu. Tujifikirie na sisi.

Ukiingia kwenye maombi ya kila inapofika saa kamili. unapopanda muda kwa Mungu dakika moja. Omba kwa kutumia hio mistari hapo juu. Zaburi 103:3 ni toba,hio iwe ni dozi yako ya kila inapofika saa kamili. Ukifika bwana ndiye mchungaji wangu, usiseme hutapungukiwa na kitu, sema hutapungukiwa na  Isaya 11: 2 , roho ya hekima na ufahamu, roho ya ushauri na uweza, roho ya maarifa na kumcha bwana, na furaha katika kumcha bwana. halafu sema sitapungukiwa na tunda la roho,upendo,furaha, amani,uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, kiasi ,upole.

Kwa hio chukua hatua , ni siku mpya, ni mwaka mpya, unapotumia muda wako vizuri hutaweza kutenda dhambi.  Tumia muda wako kwa kufikiri, kuamini, na kufanyia kazi mafunzo unayopata, tumia mfumo huu. kwingine kote umekwama tayari.  Utajikuta unaona kuwa kuna siku nzuri zinakuja kwa ajili yako.  Hutashikiliwa na wala hutafungwa na mawazo yako mwenyewe, utaweza kuona mbele zaidi, ukweli zaidi na uhalisia wa maisha yenye maana kwako.

Nakuhakikishia hutakosa mpenyo wako kama kweli utaamua kumtolea Mungu Muda wa dakika moja.

Nifuatilie youtube hili somo nitaliongea kwa mapana zaidi.

Umependa makala yangu? shirikisha wengi wapate mipenyo yao.

Subscribe ni bure kabisa

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here