Amini usiamini hivyo ndivyo ilivyo. Kila mtu jinsi alivyo , anavyoishi ni kutokana na Imani yake.
Naendelea kukuletea nguvu ya imani ndani yako . Mathayo: 9:29, Ndipo alipowagusa macho ,akasema,’’ kwa kadri ya imani yenu mpate’’.
Ni kuhusu nguvu ya kuamini ndani yako, watu wana imani tofauti tofauti, kila mtu ana imani yake. Ni muhimu kutambua imani ulionayo wewe ndani yako. Maisha yako yanategemea imani yako mwenyewe.
Kitu kibaya kinachoumiza watu wengi na hata kupelekea wengine kufa, ni Woga, wasiwasi, kutojiamini.
Acha kuhofia watu wengine watasema nini kuhusu wewe, watafikiria nini kuhusu wewe, uwe na uhakika na kile ambacho unakifanya na kukifikiria.
Epuka kupata magonjwa kwa ajili ya kuogopa , kuwa na wasiwasi , au kutojiamini mwenyewe kwa ajili ya watu wengine. Acha kuwaza wanachosema na kufikiria kuhusu maisha yako. Utakuta wengine ni watu wazima kabisa lakini bado wanaogopa kufanya kitu fulani kwa sababu eti watanionaje, watanifikiriaje. Huna maamuzi? Huna imani? Humwamini Mungu?
Hutaweza kwenda popote , hutaweza kufanikiwa hata siku moja katika mahusiano yako, familia yako, kifedha, kiroho, kimwili, maisha uyatakayo kama utakuwa unajali na kuhofia ya kwamba watu watafikiria na kuwaza nini kwa ajili yako.
Kila mahali ambako kumeandikwa Amini ndani ya Biblia ,Inamaanisha uamini Mpango wa Mungu.Kwamba Amani kilichopo ndani yako. Usihofie kutokana na Imani yako. Uwe na uhakika wa kile unachokifanya.
Imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, Ni bayana ya mambo yasioonekana. Ina maana uwe positive. Usiwe vuguvugu.
Ni malengo gani ulionayo, Kusaidia watu au kujisaidia mwenyewe.Vutia unachokitaka, vitu vilivyopo kwenye mawazo yako . Angalia baraka zilizokuzunguka. Milango mingi ipo wazi kwa ajili yako.
Fanya mazoezi ya kiroho, ya kimwili, na ya kiakili.
Mwili na roho vinahitajiana, kila unachokifanya ni juu yako. Fikiria kabla ya kutenda.Ni Mungu gani unaemtumikia? Uamuzi ni wako.
Ni rahisi lakini inahitaji nguvu, bila ya nguvu hakuna matokeo.Unachokifanya sasa ndicho kitakachokuwepo baadae.
Amini uwepo wa Mungu na nguvu yake ndani mwako.
Barikiwa.