Maisha Yanayofanya Kazi Na Muda


hiphopcongregation Maisha Yanayofanya Kazi Na Muda

Kutubu maana yake ni kubadilika jinsi unavyofikiria , jinsi unavyowaza, jinsi unavyohisi, jinsi unavyoona Na jinsi unavyotenda. Badilisha Akili yako.

Tokea wakati huo Yesu  alianza kuhubiri  na kusema, Tubuni kwa maana ufalme wa Mungu umekaribia.

Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.zipate kuja  nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake bwana.

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya  nia zenu  mpate kujua hakika  mapenzi  ya Mungu yalio mema  ya kumpendeza Mungu na ukamilifu.

Kama watu wengi wanafanya jambo la kufanana  , tambua kabisa kuwa ni cha kijinga. Lakini kama ukiona jambo linafanywa na watu wachache ni la akili.

Kijana wa kiume kama akifika miaka 30 na hakupata usimamizi wa wazazi hasa baba yake,  hataweza kuwa na mafanikio mazuri. Kwa sababu wazazi huwa hawaishi Duniani. Hata kama wazazi waliokuzaa wamekufa , lakini bado utaweza kupata wazazi  wengine.

Watu watatu ambao ni muhimu sana katika maisha yako  ni kama hawa;

1.Baba mzazi.

baba huyu kazi yake ni kutoa baraka kwa watoto wake.

2. Mkufunzi , Mlezi  au Coarch

Hawa ni watu ambao watakuongoza katika kupata Pesa. mafanikio.

3.Baba wa Kiroho.

Mzazi huyu atakuongoza  katika maisha yako ya kiroho na kufanikiwa kwako Kimungu.

Watoto wa kike kuanzia miaka   12-22 wasipopata usimamizi mzuri , wanaweza kuingia katika tabia mbaya  za ulevi, umalaya,  madawa ya kulevya, ugomvi, kuolewa mapema na kuzaa mapema. kwa sababu wanakuwa hawana taarifa kamili ya maisha wanayoendea , wanajikuta hawafiki miaka 35 wanakufa.

Watoto wa kiume nao wasipopata malezi bora  kati ya miaka 12-25,  wakaingia kwenye mambo mabaya. hawawezi kufikisha miaka 40 wanakufa. Wachunguzi wameliona hili na kusisitiza watu kubadilika kama wanataka kuishi kwa muda wa kutosha.

Lakini kama wakipita vizuri umri huu wa kijinga , wataishi maisha mazuri na yalioshiba siku.

Kwa hio kuwa makini kama kuna kitu unakipenda kukifanya  ndio hicho kitakachokuondoa Duniani.

Kama unapenda  kula vizuri bila ya kuhangaika na mateso ya magonjwa ya kisukari,  saratani,  maumivu ya mgongo,  magonjwa ya moyo acha dhambi. Unapenda sigara acha, Unapenda pombe acha.

Umri wa Upumbavu kwa watu wazima ni ule wa kati . Miaka 35–45. wanaume kwa wanawake. hapa kuna shida kubwa kama vile umri wa upumbavu wa  vijana wa kike na kiume.

Wanaume ndio wakati wa kuwa na nyumba ndogo, kutembea na  wasichana wa kazi. kuwa na madeni mengi, kulewa, kuuza vitu amabavyo ni muhimu kwa ajili ya watoto wao.  kuwa wezi, kuwa na hasira, kuchukua rushwa, kuwa na pesa nyingi isio kuwa ya Mungu. mwisho wake  ni kufa mapema .

Wanawake wao kama hawajaolewa, au kama hawajapata watoto, wanakuwa ni watu wa huzuni,  mashaka , hofu, kutojiamini. Kipindi hiki ni sawa na mtu ambaye alikuwa anasubiri gari kituoni. lolote likipita atapata kwa ajili ya kuwahi.

Badilika mapema , badili nia yako, badili kuwaza kwako, kutenda kwako. Tubu ili upate kuishi kwa siku ambazo umepewa na Mungu wako. uzifurahie.

 

Previous Inapokuwa Ngumu Kupenda Tena
Next Advanced Mindset (Akili iliyopevuka)

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.