ChrisJStill-672x372 MAMBO GANI 3 AMBAYO WATU HALISI HUYAFANYA

Lini nitakuwa mimi kabisa?

Kujifahamu wewe ni nani ndio ushauri tunaopewa mara nyngi. Unapoenda kusailiwa kwa ajili ya kupata kazi au kwenye siku ya kumpata mpenzi unaemtaka, marafiki hutuambia kuwa jiamini mwenyewe. Ni ushauri mzuri.  Lakini  unamaanisha nini?

Kuanzia muda tunaoamka asubuhi na wakati tunapoenda kulala wengi wetu huwa na muda wa kujitambua kuwa wao ni akina nani; lakini kwa sehemu nyingi tunajiweka kwenye maonyesho. Hatufanyi kama watu Halisi. ni watu wa kuiga maisha mengine.

Mara nyingi watu hupatwa na hisia za wasiwasi kwamba  katika maisha yao kuna kitu fulani hakipo vizuri; hizi hisia za kujihisi zimejengwa kwenye tahadhali zetu kwenye mvuto wa kuishi bila uhalisia na kutusisitiza kufanya mabadiliko.

Na haya ni mambo 3 ambayo watu halisi huyafanya.

1. Husema kitu wanachomaanisha

Watu halisi husema kitu wanachomaanisha , na humaanisha kile wanachosema , wanaweza kuwa wanatunza mawazo yao wenyewe lakini kama ukiwauliza moja kwa moja maswali ya nafasi wanazotaka au kitu wanachohitaji, watakupa jibu la moja kwa moja. huwa  hawajiulizi ulizi ndani yao. wana uhakika na wanachokiongea.

2.Hawategemei mtu.

Watu halisi hawamtegemei mtu, ndugu, jamaa au rafiki, hujisimamia wenyewe. Kitu muhimu kwao ni kuwa wakweli kwa ajili yao wenyewe kuliko kuanza kuomba msaada kwa mtu. ingawa zipo nyakati za kuomba msaada , wanafahamu kipi ni cha kusaidiwa na kipi sio cha kusaidiwa.

3.Wanafahamu kitu gani wanajisikia.

Watu halisi hufahamu nini kinaendelea ndani mwao. wanafahamu wakati ambao wamechoka,  wakati hawana furaha,wakati wanawoga, na wakati wanasikia huzuni, na zaidi wanafahamu hisia zao vizuri .

Hio hali Ipo kwako?

hapa kuna swali lingine. Vipi kuhusu muda ambao unajihisi kwamba huwezi kuwa wewe kabisa? Ni kwa njia gani unajihisi kuwa huwezi kuwa wewe halisi?

Sasa chukua dakika chache tu kufikiria kuhusu muda ambao unahisi kujisikia kuwa ndio wewe. Kitu gani kinakuwa tofauti? Ni wewe kweli ?

Endapo utagundua tofauti, elewa kuwa wewe unaishi maisha ya mtu mwingine , na sio maisha yako.

Fuatilia kujua  utafanyaje ili uishi maisha yako mwenyewe.  uwe halisi.

=Dondoo za kukuongezea uwezo wa kujiamini

=Tabia 15 watu wenye akili za nguvu hushiriki pamoja.

=Zoea kuanza siku kwa dakika chache za utulivu wa akili

 

Umeipenda hii makala? shirikisha wengi wajifunze.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here