megandevonblacklove-1 Mapenzi Yenye Ushindi

Tunatakiwa kujisalimisha au kubadilika?

I love you with lemon and salt, Nakupenda jinsi ulivyo, Hakuna sababu ya kukubadilisha hata kidogo.

Kushinda inatakiwa kupigania, La sivyo wangesema, Lakini kwenye mapenzi  haionekani kama kuna kitu kinafanyika kwa njia hio…Kushinda katika mapenzi ni lazima ujisalimishe.

Kutaka kumbadilisha unayempenda na kujisalimisha kwake ni zoezi la kawaida.Ingawa kila moja lina thamani  hio hio, Pamoja na upendo uliopo kwenye njia hio.Ili kutenganisha  au kutofautisha madhara yake, tunahitaji kukubali Nature ya upendo na thamani ya badiliko.

Nature ya Mapenzi: Katika kujaliana

winning-back-your-ex-with-respect-attraction-and-love-1024x372 Mapenzi Yenye Ushindi

Tumekuwa tofauti mwaka huu na ule uliopita; sio wale tuliowapenda. Ni nafasi nzuri kama  tutabadilika, Kuendelea kumpenda mtu ambaye amebadilika,  Mtu mmoja alisema .

Inategemea kama kutawezekana kubadilika tabia au kujisalimisha  kwa wale tuwapendao. Itategemea na umuhimu tulionao  katika Upendo wetu.

Hii yote inatokana na mahusiano ya kila mtu kutoka kwa wazazi wake. Alipata upendo kiasi gani, Upendo wa Mungu, na upendo wa marafiki na jamaa wote wanaomzunguka. Kutokana na maana hii, Uwezo wa kumbadilisha mtu huyu ni mdogo sana, Zaidi sana ni kujisalimisha kwake. Na huko ni kujitoa muhanga kwa huyo mtu kwa sababu umempenda.

Kwa mtazamo huu , kuendeleza  haya mapenzi ya kipekee yanahitaji usahihi na badiliko la kila mtu. Kila mtu itahitaji kujali mahitaji ya mwenzake  pamoja na upendo, Sio katika kuimarisha muungano wao bali kila mmoja aimarishe upendo.

Nature ya Mabadiliko: 

Kwa nini mwanamke anauwezo wa kujaribu kumbadilisha mwanaume kwa zaidi ya miaka 10 halafu bado atalalamika kuwa  hajaolewa na mwanaume ambaye alitakiwa kuolewa naye?

Inaonekana wazi kwamba ni ngumu kujaribu kumbadilisha mwenza, lakini ni rahisi kubadilika wewe mwenyewe. kwa sababu kufanya hivyo utaharibu uzuri wa mahusiano yako. Kitu cha kufanya badilika wewe .

Njia nzuri ya kubadilika ni kuwa tofauti na mtazamo wa kwanza uliokuwa nao,  Bila ya kupoteza kiini cha  tabia yako halisi. Ni aina ya mabadiliko ya kipekee., Ni process ya kukua kiakili kibinafsi. Kuwa na uelewa wa kipekee katika mazingira uliopo, kwa mwelekeo ulio sahihi. mabadiliko ya ndani na nje.

Kujiheshimu na kufahamu hitaji la mwenzako na hitaji lako la msingi.  Hapo mtaweza kutoshelezana  kwenye mahusiano yenu. Kuthaminiana kila mmoja. Kuonyesha upendo wa kweli. Mapenzi ya kweli ni kuona undani wa mtu sio kwa nje.  Kuona kitu alichokibeba mwenza wako kwa ajili yako.

Mabadiliko Makubwa Yanamfanya mtu Kujisalimisha?

Watu wanasema ,unapokuwa na watoto, kila kitu kinabadilika, lakini huenda mambo yamebadilika  kwa kuwa tayari tupo hapo.

Kubadilika au kutobadilika kwa mtu hakuongezi thamani  ya kuwepo kwake hapo, Kama kutakuwa hakuna upendo ni sawa na kuishi  kama waajiriwa kwenye kazi ambayo hakuna anayependa ila kwa kuwa anapata mshahara hana jinsi ya kuacha kazi.Ikiwa na maana kwamba hakuna kazi rahisi. Umehatarisha akili yako mahali ulipo.

Ili kupata ushindi katika mapenzi , hutakiwi kujisalimisha. Kama utafanya hivyo ni vizuri kuipanga akili yako  kwa ajili ya kuboresha mahusiano kwa mtindo wako wa kipekee. Hakuna badiliko  la uongo linaloweza kudumu.

Badiliko la kweli ni kila mmoja kubadilika yeye mwenyewe na kujiona kuwa yeye ni bora anapokuwepo na mwenza wake, kukua kibinafsi na kujiendeleza katika mahusiano.  Sio kusema kwamba wewe ni mtu tofauti unapokuwa na mwenza wako, Hapana. Sema wewe ni bora unapokuwa naye.

Usijaribu kumbadilisha mwenza wako awe jinsi unavyotaka wewe. Hilo sio wazo zuri hata kidogo.  Achana na hicho kipengele sio kazi yako kukibadilisha. Wewe sio Mungu. Huwezi kumtengeneza mtu kwa jinsi utakavyo wewe. Lakini uwezo wa kujibadilisha mwenyewe unao. unaweza kubadilika ndani na nje.

Toa maoni yako kuwasaidia wengine.

Subscribe kupata makala mpya.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here