4495439099001_5326034067001_5312825658001-th-1024x576 Maswali 10 Ya Kukusaidia Kufahamu Kusudi Lako

Wote tunao uzoefu wa kufanya mambo ambayo hayatufikishi kwenye malengo yetu,  tunakwama kila mara mahali fulani.

Binafsi ,  nafahamu jinsi ilivyo rahisi  kuchanganyikiwa na kwenda katika mwelekeo mwingine.  Kwa hio nilipopata msukumo wa nguvu  nilikumbuka kusudi langu la juu. Wakati nafanya maamuzi ya kuamsha mradi wangu muhimu ,  ilinisaidia kukusanya nguvu zangu zote  ili kuweka wazi  nia yangu. Ufahamu kamili na msukumo.

Hapa chini , Nia yako na kusudi lako  linaweza kukurudisha kwenye mstari , na kukupeleka kwenye mwelekeo mzuri  ambao uliutaka . Kujua Kusudi lako  utaweza kuweka msingi imara kwenye ufahamu wako na kujenga maisha yako vizuri.

Kwa nini kusudi lako halionekani kuwa Halisi.

Watu wengi wanafikiri kuwa wanafahamu kusudi lao , lakini hawana uhakika asilimia mia moja kama ni kweli. hii ni kwa sababu ipo kwenye akili zao , bila ya hisia na wala hamu   inayounganisha haipo.

Nimegundua kuwa , kama ukipata kusudi lako utajisikia kuishi ndani yako , sio kwenye akili tu, tumeunganishwa na hayo . hio ndio hutushikilia maisha yetu. Na hii ndio kanuni ya kivutio.

Nilikuwa nikitafuta kusudi kupitia kuongea na kufikiria  mwenyewe kwa vitendo. lakini roho yangu na mwili wangu  havikuwepo kwenye hayo mawazo. Akili yangu ina hamu ya kitu kingine . lakini ndani yangu hakipo. wakati mwingine moyo unakataa.  Kusikiliza mwili , hisia, Na kuamini sauti ya ndani inaweza kukusaidia  kufika mahali sahihi kwa wakati sahihi.

Maswali 10 ya kutambua kusudi lako.

1.Ni nini kusudi langu katika maisha haya sasa hivi?

2.Thamani yangu ya kipekee ni ipi?

3.Nafanya nini kinachonisaidia na kuwasaidia wengine?

4.Natamani nini katika maisha yangu?

5.Wapi na lini nitaelezea kusudi  langu kupitia afya yangu?

6.Nitaelezea wapi na lini kusudi la mahusiano yangu?

7.Nitaelezea wapi na lini kusudi la kazi yangu?

8. Ni wapi nimeunganishwa na kusudi langu?

9. Ni mahali gani ambapo siliishi kusudi langu?

10.Nitachukua hatua gani  ili niunganike na kusudi langu?

Baada ya kusoma , funika macho yako  na usikilize majibu, halafu fungua macho yako na useme kwa sauti hayo majibu. Au andika mawazo  uliyopata au picha iliyokuja kwenye akili yako. Uwe wazi na mwenye udadisi. maneno, picha ya matokeo yanaweza kukushangaza.

Unaweza kurudi mara nyingi. kila unaporudia  kumbuka kuvuta pumzi ndani na kutoa nje ukiwa umefunika macho. endelea kufanya hivyo na usubiri kitu gani kinatokea.

Umegundua nini?  huenda umejisikia kutaka kuweka ahadi ya kuwa mtu mwenye upendo. au umepokea ujumbe wa wazi  wa kutaka kubadilisha maisha yako.

Tunza ufahamu wako kila siku . kila unapopata jibu kutoka kwenye maswali hayo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here