Misingi Ya Kuwa Mtu Mpya


Prayer-Faith-God-Stones Misingi Ya Kuwa Mtu Mpya

Kuwa mtu mpya ni kuzaliwa upya.  Huwezi kuwa mtu mpya bila ya kufanya mabadiliko ndani ya moyo wako, mwili wako , Akili yako na hisia zako.

Ukifanyika upya utapata msingi wa mambo yote. Ni kiini cha mambo yote. Bila ya kufanyika mtu mpya hutaweza kushinda katika maisha yako, katika mahusiano yako , katika kufanikiwa kwako,  katika afya yako, katika familia yako  na katika utajiri wako na utele.

Mwanadamu ameumbwa katika utatu. Mwili, Roho na Moyo. Ni vizuri kuhakikisha vitu hivi vinakaa vizuri , vinakuwa na umoja . Kitu kinachohitaji ni  Nidhamu yako , Usikivu wako  ili uweze kutunza  utatu wako.  Ukitaka mtu wa zamani aondoke na abaki mtu mpya itakubidi kufanya yafuatayo.

Uwe mtu wa shukurani,  Badili mawazo yako, au fikra zako.  Badilisha tabia yako,  linda tunda la roho ambalo ni Upendo, Amani, Furaha, Utu wema, Fadhili, Imani, Uaminifu wako na uvumilivu. Lakini hapa katika uvumilivu uwe  makini kidogo. kwa nini? kwa sababu   usipende kuvumilia matatizo ya muda mrefu , hio sio Mungu.  Matatizo ya Ugonjwa wa muda mrefu usikubali. Usiombe uvumilivu wa mtindo huo . Hata Yesu alisema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke , lakini si kama nipendavyo mimi.  kuwa makini na maombi yako.

Pendelea kuwa na ushirika na Mungu , lakini pia tambua kuwa Mungu ni yote katika yote , huwezi kumfananisha Mungu na baba wa kawaida Duniani. Msifu Mungu ndani ya moyo wako, midomo yako ibebe sifa zake.Utaona neno lake linatimia maishani mwako.

Unapoomba kuwa specific. Tambua kitu unachokitaka wakati huo , usichanganye maombi yako . Omba kwa Imani, Usiangalie mazingira yaliopo wakati huo, wewe jiachie kwake bila ya kujali. Omba uongozi wa kila kitu unachokifanya. kumbuka kuwa Popote utakapokuwa Mungu yupo na wewe. Kutokana na Imani yako Utapata .

Njia za mafanikio Ambayo Utapata Katika Uongozi Wa Mungu.

Kusikiliza sauti ya ndani 

Maamuzi ambayo utafanya

Sauti ya mamlaka  ya Kiungu

Kupitia kujifunza ili kupata maarifa

Kupitia Manabii

Kutafakari  

Kutendea kazi mafundisho

Kuwa mtii.

Imani ni sasa  hivi, usisubiri kuanza kutafuta imani nyakati zingine , ni sasa hivi. Imani yako itabadilisha kikwazo chochote  katika maisha yako.  kupata nguvu ya Mungu sio machozi ,  Imani ni sasa. Imani ni wewe .  Fanya sasa kwa kuamini unachokifanya , unachotaka kukipata. Amini sasa sio baadae. Pata ngao hii ya imani, pata silaha hii ya imani. ukipata maarifa zaidi utapata ubora ulio zaidi.  Anza ndani yako , kwa kuwa kila kitu kinaanzia kutungwa ndani yako.

Nguvu Ya Maneno.

Ipo nguvu ya maneno katika kuyakiri kila siku.  Kwa kutumia kanuni ya kimungu ya kupanda na kuvuna , katika majira na nyakati zake. Kila upandacho utakivuna. ukipanda ubaya , utavuna huo na zaidi. Lakini ukipanda mbegu nzuri utavuna mara mia . Kama ukitaka kuwa mtu mpya zingatia kanuni za maisha . Anza kukiri mambo mazuri maishani mwako , hasa kile kitu ambacho unataka kitokee  kwako .

Vizuizi  Vya Kufanikio.

Ujinga

Hofu

Mashaka

Dhambi.

Tamani kuwa mtu mpya sasa hivi, usisubiri kesho . Badilisha tabia zako, badilisha maneno yako, mitazamo yako. Anza kukiri  maneno ambayo unataka yatokee katika maisha yako.  Waza mambo mazuri. kuwa positive kila wakati. achana na negative.

Kumbuka chanzo cha kila kitu ni wewe. Anza kujipenda ili uweze kuwapenda na wengine. Huwezi kumpenda Mungu Kama hujipendi wewe mwenyewe. Huwezi kumuheshimu Mungu kama hujiheshimu mwenyewe.  Tamani kujitambua. Tamani kuwa mtu mpya. jijali, tunza ulichonacho. Tunza imani yako. Na Mungu atakuwepo pamoja na wewe.

Mungu Akubariki unapoanza sasa hivi kuamini.

Kama umebarikiwa ,  share kwa wengine wajifunze. Kumbuka kutoa sio pesa tu. Hata kile unachojifunza ukitoa kwa mwingine  utafanya jambo jema. Ni kwa faida yako.

Pia usisahau  Subscribe kupata makala  mpya kila mara.

 

Previous Jinsi Ya Kuacha Tabia Zenye Sababu Ya Kutofanya Sex
Next Maumivu Na Mapenzi Huenda Pamoja?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.