Msichana Mwenye Ujasiri Anafahamu Kwamba Maisha Yanasonga


f8267dcd6b8ea4d8507bca7735951837-1024x683 Msichana Mwenye Ujasiri Anafahamu Kwamba Maisha Yanasonga

Unaweza usione , lakini una siku nzuri . Kabla  hatujashindwana , ngoja nikuambie kwa nini. Umeamka leo kutoka kitandani mwako , kwenye chumba chako, nyumba yako.Umeamka. umesafisha mdomo wako, umeoga.  Unayo maji mengi hapo nyumbani huna shida ya kutafuta maji.

Umewaona rafiki zako , familia yako, umeongea nao , umepata chai pamoja , wanakufurahia,  na hata kukukumbatia. Una chakula cha kula na yule umpendaye. Umeenda kazini. Una kazi.  Umefanya yote vizuri na kurudi nyumbani. Unapumzika  Unalala. Unayo ahadi yako kesho tena.

Una simu yako ya smartphone au computer, na sasa unasoma makala hii. Ngoja nikuambie  jinsi ulivyo na maisha mazuri.  Na sio tu mazuri tu kwa sababu una kila kitu , Lakini ni kwa sababu Ya wewe ni nani.

Sifahamu upekee wako, Lakini nafahamu wewe ni mzuri. Unapigana vita ambayo sio kila mtu anaweza kupigana kama wewe. Unawajibika kwenye mahukumu yako, Umebeba mzigo mzito, Lakini bado Unaweza kujiweka vizuri. Una Maswali mengi kichwani mwako, Unajilaumu sana, Lakini bado unakabiliana na kila kitu. Unatafuta pesa, lakini bado unaweza kutabasamu. Wakati mwingine unajisikia hasira. Lakini bado unaweza kufurahia vitu vidogo ulivyonavyo.  Hujui unakoelekea. Lakini unakazana kutafuta njia  yako.  Umekuwa ukikatishwa tamaa miaka mingi lakini umekomaa. Bado movie au ukisoma kitabu  unajikuta kulia .Uwezo wa kufanya vitu hivyo  na hasa kwa kile unachopambana nacho, inakupa nguvu ya tofauti.  ni kama una kitu kinachoondoka, uko kimya, nguvu yako ni laini. Unajua kwa Nini?  Wewe ni msichana wa kushangaza.

Unapotaka kukata tamaa ,tazama ulikotoka . Sio watu wengi wanaweza kufanya kama  unachokifanya kila siku.  Unafanya katika ubora wako, na ubora wako ndio  ukamilifu  wako. Baki hapo. ipo siku utakuja kuamka na kutambua kuwa  uko sahihi. Utaanza kuhisi hii furaha ndani ya moyo wako. . Mizigo haitakuwepo tena. utatazama maisha yako na kuanza kutengeneza  future mpya  tena.utayacheka makosa yaliopita. utakuwa mtu ambaye ulitaka kuwa. tofauti—mwenye  ujasiri, hekima, mzuri. baki hapo. msichana mwenye ujasiri.  nyakati ngumu hazidumu . na utakuwa mshindi.

Previous Wanawake Wanatakiwa Kusaidia Wanawake Wengine
Next Jifunze Kumpenda Mtu Unayemuona Kwenye Kioo

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.