Msingi Wa Siri Uliojificha Ndani Yako


wolf5 Msingi Wa Siri Uliojificha Ndani Yako

Kuishi maisha ya uhuru na kuachana na yaliopita, Ni vizuri kuangalia mpangilio uliopo ndani ya mhariri wako wa ndani. Fikiria kuhusu  umakini wa kuchagua kila unachotaka kukifanya. Kuoa, kuolewa, kazi, mazingira, afya,hisia , tabia…

Yapo Mapigano yanayoendelea ndani yako.

Mapigano hayo ni ya hatari ni kati ya mbwa mwitu wawili.

MMOJA NI MBAYA.

images-3 Msingi Wa Siri Uliojificha Ndani Yako

Mbwa mwitu huyu amejawa na hasira, masikitiko, Uchoyo, Chuki, Kiburi, Kujihurumia  pasipo sababu yoyote, huna tatizo lakini unalalamika huna kazi, wakati siku hizi ni ruhusa kufanya kitu unachokitaka , huzuiliwi. Raisi wetu  ameachilia fursa kwa kila mtu .Uongo, kujikuza , kujilaumu, kujidharau, kukata tamaa, kutokuwa na tumaini,  huzuni, upweke, kujihukumu, kuchanganyikiwa,  na kila kilicho kibaya kipo ndani yake .

MWINGINE NI MZURI

Mystic_Wolf_1280x800 Msingi Wa Siri Uliojificha Ndani Yako

Ana furaha, Amani, Upendo, Fadhili, Wema, Matumaini, Ubinadamu, Msamaha, Huruma, Uelewa, Uaminifu, Imani, Utu wema, Uvumilivu,ujasiri,  hamu, shauku, uzuri, uhuru, nguvu, afya, na utele.

Mapigano haya yanaendelea  ndani ya kila mtu. Fikiria ni mbwa mwitu yupi ambaye atashinda ndani yako?

Msingi wa siri ambao hukujua ni katika kuchagua , ni mbwa mwitu yupi utamlisha ili akupatie msingi mzuri wa maisha yako? Umakini wako ndio kitu cha pekee katika kufanya maamuzi. 

Utaendelea kumwachia mhariri wako wa ndani  Aharibu  Kila kitu unachokitaka kwa kubaki kulenga mambo ambayo hutaki na kutunza mambo ambayo huyataki?

Au Uko tayari kujipanga upya, kuanza kuujenga ubongo wako upya kulisha vitu vipya ili kuondokana na ya zamani ili uwe mtu mpya?  Amini usiamini kuzaliwa upya inawezekana , kwa sababu unapobadilisha mwelekeo wako, unapobadilisha mawazo yako, kufikiria kwako, kutenda kwako,  Lazima utakuwa mtu mpya. Mtu akiwa kiumbe kipya , ya kale yamepita , tazama amekuwa mpya.

Kwa kuingiza yale tu unayoyataka na kuachana na mambo yote ambayo  huyataki katika maisha yako, Ni katika kudhihirisha maneno yako. Kujitamkia mambo ambayo unataka yawepo katika maisha yako. Hii ni kuanza kuishi wakati Uliopo. Unaweza kujiona unaishi lakini ndugu yangu , bado hujaanza kuishi. Ngoja nikuambiie, Kila siku ongea maneno mazuri tu japo kwa dakika 5. hayo maneno yatabadilisha kila kitu. mtazamo wako, tabia.

images-1 Msingi Wa Siri Uliojificha Ndani Yako

Ukitaka kufahamu kuishi wakati uliopo anza leo kujipenda wewe, mpende Mungu.Wapende wengine, Watendee watu kwa jinsi ambavyo unataka utendewe, Chukua hatua leo, Rahisisha kila kitu, Mimi huwa naita Utele ulio rahisi ni kukubaliana na hali halisi. kushukuru ulicho nacho, wakati huo huo ukiwa na tumaini kubwa mbele yako. Unapofanya sasa, hutakuwa unafanya yaliopita,  Utakuwa unaweka msingi mzuri wa baadae. huko ndio kuishi wakati uliopo.

Utakapoanza kujisemea maneno mazuri ndio muda ambao utakuwa nunamlisha  mbwa mwitu mwenye utele. Anza kuishi maisha ya utele leo, Simple Abundance. Unastahili.

bobmarley1 Msingi Wa Siri Uliojificha Ndani Yako

Maisha ni safari, Kama ukiipenda safari Utakuwa ndani ya Upendo Milele.

Love you.

Washirikishe wengi , kisha  toa maoni yako.

Usisahau  Subscribe ili kupata makala mpya.

Previous Fahamu Kuishi Kwa Amani Wakati Wengine Hawawezi
Next Jinsi Ya Kuacha Tabia Zenye Sababu Ya Kutofanya Sex

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.