4297224_orig Mungu Anapatikana Wapi? Umepoteza Mwelekeo?

Nilimpoteza Mungu nilipokuwa  nimeacha kumtafuta.

Wengi watasema Mungu anapatikana kanisani, mahali popote, milimani, na Kwa kila mtu.Lakini hilo sio jibu sahihi.

Neno la Mungu linasema kwamba  Nanyi mtanitafuta na kuniona mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Nami nitaonekana kwenu.

Tunamfahamu Mungu, Lakini ni wangapi hasa wanamfahamu kwa kina? Ni wangapi husahau kitu ambacho wanakifahamu?

Ngoja Nikuelezee Hapa.

Nafahamu kuwa Mungu anakupenda, Ananipenda.Najua anatujali. Najua ni mkamilifu. Na kwa sababu ya upendo wake sisi pia ni wakamilifu . Najua kwamba kitu watu wanachofikiria juu yako  Haijalishi, Ni yale tu ambayo Mungu anafikiria juu yako. Fahamu hata  unapokuwa mpweke  haupo peke yako, kwa sababu yupo pamoja na wewe. Wakati wote yuko pamoja na wewe.Unaposhuka moyo na kuangushwa sehemu sehemu katika maisha yako yupo na wewe.

Unaweza ukawa unaishi kama mtu ambaye hajui ukweli. hajui ukombozi wa Mungu.  Kama kweli hivi vitu vipo kwako na  unaamini  kwa nini matendo yako yanajirudia  mara kwa mara?

Nitakuambia.

Unamfahamu Mungu lakini hujui anapatikana wapi, humjui vizuri.Bila shaka, Unaona kwa watu wengine wakisema juu yake , kuwa anatenda katika mahusiano yao, kazi zao, biashara zao. Ni kweli anafanya, lakini utampata wapi?

Sehemu ya kwanza ya kumfahamu Mungu ndio kitu ambacho hata mimi nimekuwa nikifanya kila siku ,Ni katika Kuomba, nafikiri hata wewe. kwenda kanisani, msikitini na kwingine.Lakini bado hatuna uhakika  ya kuwa kweli Mungu yuko huko.

Kila wakati kuongea naye , kusema naye, Kwa nini hatuwezi kuwasiliani naye katika njia yake ya kweli anayoipenda. Ukiwa unataka kumfahamu Mungu , Jua tabia zake.Ongea lugha yake. Sio kwamba huamini, ni kwa sababu umejiweka mbali na mahali anapopatikana.

Unapoacha kumtafuta Mungu  unampoteza.

Ni kwa sababu ya kuwa busy na maisha yako, na hayo maisha hayana furaha, hayana amani, hayana upendo.Ndipo hapo unapochanganyikiwa na kuanza kupoteza muda katika vitu ambavyo havina faida katika maisha yako.

Huenda hata hutaki kuishi maisha kama hayo, unataka uwe hai, hai ndani ya Mungu. Lakini umesahamu unachokifahamu, kwa sababu hukutaka kujishughulisha kufahamu ukweli, umejiweka mbali na ukweli, kwa sababu ni rahisi kusema unaamini lakini matendo yako yanasema tofauti.

Watu wanaogopa ukweli. lakini ukweli ndio unaokuweka huru. Japo ukweli unaumiza lakini utakuweka huru .

Mungu amekuwepo  tangu mwanzo. Mara zote yupo. lakini hakusukumi, hatakusukuma wewe umwingize ndani ya moyo wako.Ni vizuri kama ukifungua moyo wako, nifungue moyo wangu na tumtafute. kwa moyo mkamilifu na tutamuona , tutamtambua, kwa njia rahisi ambayo tumekuwa tukishindwa kutambua.

Nitakuambia siri hii . Wapi Mungu anapatikana . Mungu anapatikana katika UPENDO. sio mahali kwingine.

Ukiipenda nafsi yako , Utampenda jirani yako, Utampenda Mungu. Mungu atakuja kukaa kwako kwa sababu ya upendo uliopo ndani yako.

Mungu anakaa mahali penye Upendo. mahusiano yako yakiwa na upendo wa kweli yataweza kudumu, Familia bila upendo ni mvurugano mkubwa. Jamii ikiwa haina upendo matatizo ni mengi.

Ukimpenda jirani yako hutaweza kumfanyia kitu kibaya, hutamuonea wivu, hutaweza kuzini naye, hutatamani kitu chake.

Ukiipenda nafsi yako  utamiliki maneno mazuri ya upendo, furaha, Amani. kiasi, uvumilivu. Mungu atakaa mahali pako. katika kazi yako, biashara yako.

Amebadilisha moyo wangu, Atabadilisha moyo wako, kama ukiachilia Upendo katika maisha yako. Fungua tu milango ya moyo wako na Mungu yeye atafanya sehemu yake. Inaonekana kama amepotea lakini nakuhakikishia kuwa ,kama utafungua moyo wa Upendo, na kama utamtafuta katika upendo, utamuona katika kila sekta ya maisha yako.

Na utamuona zaidi ya ulivyokuwa unakwenda kwenye nyumba za ibada na katika kuomba sana .

Subscribe kupata makala mpya.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here