perseverance-in-prayer-1 Mungu Anataka Ujue Jinsi Ya Kujipenda

Umuhimu wa kujipenda ni wazo la Mungu mwenyewe. Ni kitu kimoja kigumu. Mungu anatutaka tuwe hivyo kuliko mawazo yetu  yanavyotunyonya na kushindwa kuwepo katika usalama.

Mungu anaumia anapokuona huna furaha, hujipendi. Lakini kwa upande mwingine  Mungu hataki mawazo yetu yabadilike kuwa na uchoyo wa kupenda wengine. kwa hio ni jinsi gani unavyojipenda mwenyewe?

Yote ni katika kubalance. Kulinda moyo wako ni kujipenda. hio inatakiwa iwe ni kawaida kwako kujilinda. Hutakiwi kuiga maisha yasio  lingana na uwezo wako. Jithamini. jikubali.  Jipende mwenyewe full kama binadamu mwingine yeyote. pendezesha, furahia na upende mwili wako na moyo wako. Mungu amekutengeneza.  Na amekuumba kwa mfano wake.  Amekuunda na kukufanya kuwa mkamilifu kwa jinsi ulivyo. Anakupenda ulivyo.

Kusema kweli kama utaanza kutumia muda mwingi katika mawazo ya kuondoa mikunjo, madoa, vipele, kutengeneza uso wako kwa namna nyingine,  na kutafuta mavazi mazuri  kwa ajili yako,  Je unao muda wa kumwabudu yeye? au umerudi kwenye sanamu,  unapenda uzuri wa sanamu?

Ni kawaida kuangukia kwenye mtego wa viwango vya juu siku hizi. Kama mimi nilivyokaa hapa naandika hii makala . Najiona nina hatia kwa hilo. Sina uhakika kama kweli nimefanya kitu cha kutosha kwa ajili ya Mungu. Lakini  hapa nilipo sina makeup usoni mwangu,  tumbo langu halina kitu,  natakiwa nichunguze kuhusu hilo, lakini nimechagua nisile kwanza, Sio kwamba nataka niwe na  Abs ,nisiwe na tumbo hapana.  Lakini pia ni muhimu kukumbuka kuwa Mungu anataka sisi tulishe  na kuIjali miili yetu .

Nitafanya hivyo ili nijisikie vizuri , nijipende. Sio kwa sababu nimeufanya mwili wangu kuwa sanamu yangu. Kujipenda ni hali ya kuwa huru kutoka kwenye  mawazo mabaya kuhusu sisi wenyewe, kujilaumu,  na kukosa usalama ni kitu kinachoturudisha nyuma. Jinsi unavyozidi  kujijali, kujipenda, ndivyo utakavyowapenda wengine, na kumpenda Mungu.  Lakini kadri unavyojichukia , ndio utakuwa mbali na Mungu na hutaweza kuwapenda wala kuwahudumia wengine. Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe.

Wakati tunapoambiwa kuwapenda wengine  haijalishi wakoje, inaweza kuwa ni njia nzuri ya kutumia kwa ajili ya kujipenda wenyewe, na kuwafanyia wengine kama sisi tunavyopenda kufanyiwa.

Somo kuu kwa kila mwanadamu ni Upendo. Mpende kila mtu, pamoja na wewe.  Mungu hataki tuwe na kiburi, kujisikia na hataki tujilaumu wenyewe. kwa sababu yapo madhara.

Self-awareness na self-love ni vitu vinavyoenda pamoja. Jifahamu kabisa wewe ni nani,  Na Mfahamu Mungu , Unapokuja kwake  kwa ajili ya kutaka msamaha  na msaada wa  kujitambua na kuwa mtu bora.  Jione kama Mungu anavyokuona wewe. pamoja na madhaifu yako, kwa sababu sisi ni wanadamu tunafanya makosa. Huhitaji kujilinganisha na mtu mwingine, huhitaji kuthibitishwa  na maneno  ya watu kwamba wewe ni mzuri, unapendeza. Mungu anakujua tayari, na anakupenda jinsi ulivyo.

Men__039811_29 Mungu Anataka Ujue Jinsi Ya Kujipenda

Kwa kumalizia , nakuachia maneno haya

Ee Bwana umenichunguza na kunijua,wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu. Umelifahamu wazo langu tokea mbali. ( Zaburi 139:1….) Nakushukuru kwa kuwa nimetambua  kwamba maisha ya Imani huanzia  ndani yangu, katika kujipenda .

Tafadhali kama unafaidika na makala zangu share kwa wingi.

Toa maoni yako kuwasaidia wengine, kama unaelewa zaidi ya hapo ongeza hapa chini  kwenye maoni.

Kisha Subscribe.

Mungu akubariki unapofanya hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here