tumblr_m3ur0dNEHZ1qb0lexo1_500 Mwaka 2018, Nasamehe,Naachilia Yasio Na Maana Kwangu

Katika mwaka huu mpya, Naachilia kila kitu ambacho siwezi kukidhibiti.

Nafunga macho yangu na kuomba kuondoa kila kisichokuwa cha changu kwa kuelewa  au kwa kutokuelewa. Namwamini Mungu kuniongoza na kuniwezesha kuyafanya haya.Naachana na Woga na wasiwasi na kuruhusu chochote kinachokuja kwangu . Nitajitahidi kuishi kwa uhalisia wangu , katika kweli ,na kuona kitu kipya  maishani mwangu.

Katika mwaka huu mpya , Naachana na woga.

Naenda kujaribu kwa nguvu zangu zote kuacha kuwaza kupita kiasi,  kuachana na akili ya kushangaa pale ninapokuwa siwezi kufanya kitu fulani. nitakuwa mtu wa kutabasamu, hata kama nitakutana na mashaka.  Nitakuwa naamini hata kama sina jibu . Nitatafuta kujisikia vizuri zaidi kuliko kushikilia mambo kifuani mwangu.

Katika mwaka huu mpya, Naachilia mashaka yote.

Nitaacha kuongea maneno yasio na akili kwa ajili yangu,  yale ya kujitamkia kuwa siwezi kitu fulani, sistahili, sina nguvu,  badala yake  nitalenga yalio mazuri tu, ya kujenga na kuleta mabadiliko, Nitajitahidi kusikiliza yatokayo moyoni mwangu.Nitakuwa ni mwenye busara zaidi. nitajivunia moyo wangu  na ngozi yangu.

Katika mwaka huu mpya, Naachilia mahusiano yote ya zamani.

3458-gtgtgt Mwaka 2018, Nasamehe,Naachilia Yasio Na Maana Kwangu

Mahali ambapo sipati amani. mahali ambapo pananirudisha nyuma, badala ya kunijenga.Mahali ambapo siwezi kutunza tena, Nitachukua nafasi ya kuanza upya tena.  Kuwa na uhuru wa kuamua mambo yangu bila ya kupingwa na mtu.Nitakubali upendo ambao unaleta maana maishani mwangu. Sitabeba maumivu ndani yangu wala uchungu wowote . mimi ni mpya.

Katika mwaka huu mpya, Sitavunjika moyo.

Nimechagua kuanza upya, kujipa nguvu mwenyewe na kujiponya  haijalishi niko katika hali gani na kuna umuhimu gani.Nitarekebisha kila kitu  na kuongea na watu ambao niliwakosea na kuwaumiza au walioniumiza, maana nahitaji kuwa na Afya,  sitakuwa na kinyongo na mtu yeyote aliyeniumiza moyo wangu. Nitaanza upya.

Katika mwaka huu mpya ,Naachana na Negativity.

Hurt-feelings Mwaka 2018, Nasamehe,Naachilia Yasio Na Maana Kwangu

negativity

Kwa sababu mawazo mabaya hayana maana katika maisha yangu tena. Kwa kuwa kila kitu kitakuwa sio kizuri. Lakini nitakuwa mtu wa kufurahi. Nitatafuta Amani ilipo kila mahali nitakapopita. Nitatumia muda kwa ajili ya kujiendelea na kujijenga mwenyewe kwanza na wengine . Ni nzuri zaidi kuliko kujivunja moyo.

Katika mwaka huu mpya, Naachana na Kushindwa.

Nikitambua kwamba siwezi kuwa vile, siwezi kuwa sahihi , ni sawa. Nakubali makosa na kujifunza kutokana na hayo . Nitatafuta njia mpya ya kukabiliana na kila linalokuja maishani mwangu kwa ufahamu zaidi.Nitaandika historia yangu mwenyewe.  Nitaacha yaliopita  yapite.

Katika mwaka huu , Naachilia mipango yote ilioshindwa.

Slide2 Mwaka 2018, Nasamehe,Naachilia Yasio Na Maana Kwangu

Nimeelewa kwamba  sio kila kitu nilichokipanga kukifanya kitafanikiwa kama nilivyotaka. Hii haina maana kwamba mimi ni dhaifu, Hapana. Badala ya kutazama nyuma nitatazama mbele.  Nitatengeneza  mawazo mapya, njia mpya, nitajikumbusha kuwa sio kila mipango niliyonayo itafanikiwa. mingine inaweza kushindwa.  Na hio ni sawa.  Mungu ana mpango ulio bora kwa ajili yangu.

Katika mwaka huu mpya, Nitaachilia yasionihusu.

Nitaachilia watu, vitu, hisia, mawazo  yasio kuwa ya kwangu , sitayatunza ndani yangu.  Hayatanipa matumaini. hayatanifanya kuwa mtu bora.  Naachilia upendo ambao haunijengi wala kunipa heshima ninayostahili.  Nachukua hatua moja nyuma kwa kila ambacho siwezi kukibadilisha au kukifix. Nitaelewa kuwa ipo nafasi kwa ajili yangu, mikono yangu itashikilia, nitakapojisikia kuwa tayari nipo nyumbani.

Katika mwaka huu mpya, Naachila upendo, Tumaini, na mwanzo mpya wa kila kitu kilicho chema maishani mwangu.

Subscribe. kupata  makala mpya.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here