Mara nyingi mwanaume anapokuacha ni dhahiri kuwa hakuwa na mapenzi ya kweli kwako, na wala hakuwa na hisia  za kweli kwako hata hakuvutiwa nawe toka mwanzo,

kama hakuwa na mvuto wowote na hakukuonekana muunganiko wowote wakati wa urafiki , ni lazima baadae mambo yatabadilika tu haijalishi itachukua muda gani.

kwa hali kama hii  wewe umempenda kweli na yeye kaamua kuondoka inaumiza sana.lakini endapo atabaki na muendelee na msuguano wa hapa na pale italeta shida pia.

JE WEWE NI  MSICHANA NA UNA MCHUMBA?soma hapa.

swali la 1

unapoongea na wanaume wengine  huona wivu?au anaogopa kuonyesha wivu mbele yako,

au ana wivu ila ni mkimya?

hana wivu hata kidogo?

swali la 2

huweka muda wa kuwa nawe  japo ana majukumu mengi?

Anajisikiaje akiwa na wewe, ukiwa nae muulize swali hilo, ukimgusa  anajisikiaje, na wewe je unajisikiaje unapoguswa nae.

Angalia kama hua anaona kama anapoteza muda anapokuwa nawe , halafu muda mwingi anaPENDA KUONGEA NA MARAFIKI. maswali mengine fuatilia  utayapata,.

Kwa kawaida mahusiano yanapoendelea  na hata wakati mwingine kushiriki tendo la ndoa  ni matokeo tu sio upendo , yalizoeleka hayo tokea mwanzo  angalia dalili za kukuachwa.

wanawake wengi tunafikiri kuwa haya ni matatizo ya kawaida  katika mahusianiano , SIO

Na zaidi tunafikiri kuwa na haya matatizo kumesababishwa na kitu fulani , sio.

mwanaume huondoka  kwa sababu nyingi , zingine ni nzuri tu zingine sio nzuri, kwa sababu inawezekana  anataka kujifahamu kwanza  yeye mwenyewe , ni nani  na anataka nini,  labda mwanzo alikurupuka tu kuamua kuoa  ,kwa sababu ya shinikizo lakitu fulani

mwamume anapoanzisha mahusiano , mara nyingi huwa kuna kitu anahitaji kutoka kwa mwanamke, lakini hujikuta kaingia ndani zaidi  ya alivyotarajia , matokeo yake ni ndoa ambayo hakupanga, mara nyingi tu wewe uliza wanaume watakuambia, hata akikaa miaka mingapi ipo siku ataona kama yuko jela.

mahusiano ya muda mrefu haikupi wewe uhakika wa kuwa na  ndoa nzuri , hiii ni safari moja ndefu sana na inatakiwa iwe na umakini wa kuamua mambo.

JE WAWEZA KUMWAMINI MWANAUME MSIKIVU?

NDIO

Lakini hata huyu anaweza kukuacha tu . anaweza kuwa msikivu kama anakuamini,

NJIA ZA KUMPATA ALIE MSIKIVU

Angalia uaminifu kati yako na yeye,

mawasiliano yako na yeye yawe ya karibu  na awe ni mwepesi kuitikia mara unapomuhitaji, kwa kadri awezavyo  .ili umwamini akuamini kabla wewe hujamwamini

je kuna mvuto, kuna connection  kati yenu?

connection inajenga uaminifu,

Nivigumu mwanamke kumwamini mwanaume,

Pia ni vigumu vilevile mwanamume kumwamini mwanamke.

Wote tuna tofauti  , na kila mmoja ana penda  vitu tofauti, kukosekana kwa uaminifu nikitu ambacho kipo ila kinatengezwa.

wanawake mara nyingi wanahitaji  vitu wavipendavyo , hutamani kuchukua vyasnzo vya wanaume,  muda wao ,usikivu wao, pesa zao, uwajibikaji, na mengine kadha wa kadha . lakini  unapomwamininae kukuamini inaleta hofu fulani na ni maumivu sana anapoamua kukuacha.

KWA NINI WANAUME HUONDOKA:

Watu wengi huamini kuwa kuondoka kwa mwanaume ni  kwa sababu ya  tabia za mwanamke ,  au mume kutekwa na kahaba  , huenda sababu hizi ni kweli nami nasema ni kweli kabisa yawezakuwa, lakini tukienda ndani kabisa bila ya kujali  kuwa sisi ni wanawake tuvute upande wetu sio.

katika kutafuta zaidi ni ninisababu  nimeona kuna sababu zingine ni kubwa na nzito sana ambazo kweli hata kufikiria utaona ni kweli ,hebu tuangalie sababu baadhi tu hapa ,

1.MAAMUZI

Hata wanaume hukurupuka kuoa kama wanawake tunavyokurupuka, baadae mambo huwashida  baadh ya watu, ingawa wengine hukomaa hadi mwisho . hao ni mashujaa.

utakuta mwanaume anaoa kwa shinikizo , labda la wazazi  au mke kutokana na kuwa pamoja kwa muda mrefu labda , au tayari binti ana mimba.

2.KIBIOLOJIA

Wanaume wameumbwa kutambulikana na misuli ya nguvu  ya kuwa ni wa kwanza kwa kila jambo mbele ya wanawake , hufanya mambo yao kwa amri , hawapendi kuona kuzarauliwa na  watu,  kama vile  wao ni vichwa . na hii huanzia toka wakiwa wadogo kabisa , hujengwa hivyo na akili na ubongo wao , wanakuwa tayari kwa lolote.

Hutamani kutambua hisia zao , hupenda kupata kitu ambacho anakipenda  , kama vile sisi tunavyotamani kupata tuvipendavyo.

KWA NINI WANAPOONDOKA TUNAPATA MAUMIVU

Mwanaume kuondoka inaumiza kwa sababu  umezoea kuwa pamoja nae na ukaribu wa muda mrefu

Inaumiza kwa sababu ya upendo ambao uliweka kwake.

Lakini kwa nini sasa unamwacha mwanaume aondoke wakati unampenda. kwa nini unapata hasira wakati hayupo?

sio nzuri , inabidi kuacha kiburi, majivuno  na hasira za ujinga,  tengeneza mahusiano mazuri kabla ya kutokea mambo mabaya. unaweza kujisifia lakini utateseka sana na maumivu.

Sababu nyingine wanawake hawakubali kuwa chini ya mwanaume,  hawataki kushuka na kuomba msamaha ndio maana wanaume huondoka ,

Hakuna mwanaume angeweza kumwacha mke anaempenda  ana hisia zote  kwake na halaumiwi na chochote .

lakini ataondoka tu endapo ataona kila afanyacho  wewe unaona sio sahihi.

unaweza kutuambia zaidi uzoefu wako , katika hili la mwanaume kuondoka, uzoefu wako utasaidia mwanamke mwingine .

love.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here