NI WAKATI WA KUACHA KUWAPONGEZA WANAOPOTEZA UZITO, KWA NINI?


iStock_000021775901Small NI WAKATI WA KUACHA KUWAPONGEZA WANAOPOTEZA UZITO, KWA NINI?

Umepungua uzito? hili ni swali la kawaida limekuwa likiuulizwa mara nyingi. Nimemwona mtu ambae sijamuona siku nyingi , Anaonekana vizuri, ndio mawazo ya watu wengi. Ni tabia mbaya , na najaribu kuikata kabisa.

Kwa Nini ndio kifuatacho.

1.Hii ”pongezi ” kawaida ni kama aina ya matusi.

Unapouliza kama mtu amepoteza uzito wakati unajua  kabisa kuwa wana uzito unaotakiwa kupunguzwa. Ni kama unawajaji, kufikiri kuwa wanatakiwa kujiweka vizuri.Unapokuwa unauliza hayo maneno madogo . hio sio pongezi ni maneno ya kukejeli mtu.

2.Mtazamo mzuri wa mtu hauna maana kwamba lazima awe amepunguza uzito.

Unapogundua kuwa mtu anaonekana vizuri, utakuwa umeona kitu kipya chema juu yake.

Unapojisikia vizuri wewe mwenyewe, kuna kitu kizuri kinaumbika kwako. Fahamu kuwa kila tazama ya mtu huwa na maana tofauti. Na ukumbuke sio kila mtu anaamini kuwa sifa ya ujasiri ni kuonekana vyema, katika mwili, uvaaji .

Mtu anapokuwa na furaha na Amani ya kweli , Huonekana . Na watu hutamani kuiga jinsi alivyo. Inaitwa ” positive self-Image.

3.Unalisha Jamii Fikra za Mwonekano.

Nafikiri watu wengi wamekuwa wakikereka na maswali haya ya kupungua uzito. ukweli yanakatisha tamaa, kwa kuwa waulizaji , huuliza kwa kutomaanisha mazuri. Mtu mwingine anaweza kuwa anajijali kwa njia yake nzuri tu.

Lakini mtu anapokuja kukuuliza swali la kwa nini haupungui uzito. Utafanyaje? Unaweza kutoa pesa zako zote kwa ajili ya kupata mwonekano mzuri? Au utajitahidi kujijali kwa ajili ya kupata afya ilio bora.

4.Inaweza Kuwa Mtu Unaempongeza amepata Mwenza Muhimu Maishani Mwake.

Haijalishi hisia za kimwili ndani ya mwili wako au kuhusu maisha yako,Hisia hizi huleta madhara ya jinsi tunavyoonekana kwa wengine na kwetu sisi wenyewe. Kama una tabia mbaya zinazoathiri mwili wako, au unakuwa unaongea vibaya kuhusu wewe. hutapenda unachokiona kwenye kioo.

Lakini ukijikubali jinsi ulivyo, una uzito au huna uzito. na unaamini unafanya kila uwezalo kwa ajili yako. utakuwa na mwonekano mzuri.
Unafahamu kuona badiliko la tabia ya mtu wakati wanapokuwa kwenye mapenzi, ni kama hivyo. kubali, badala ya kumpenda mtu kwa mwonekano, mpende kwa tabia. Kitu ambacho ni kizuri.

5.Kutazama ndani ni Muhimu Zaidi.

Hapa kuna Pendekezo langu; Unapomuona mtu na kufikiria ”Wow, wanaonekana vizuri!” Badala ya kuwaambia wanaonekana vizuri ( wanapendeza), waambie kwamba wanaonekana kama wanafikiria wako vizuri. hivyohivyo, muda mwingine mtu anapokuambia kama umepungua uzito, jipongeze kuonyesha kujijali. hio ndio kwa nini wanapongeza kweli.
Kilichopo ndani ndicho kinachoonekana nje.

Tubadilishe malengo yetu ya kupenda na kukubalika. Jisikie mwenyewe kuwa upo vizuri , na wote wanaokuzunguka waone hivyo. Self-love is true one size -fit-all. Inaonekana kwa uzuri kwa kila mtu.

 

Umeipenda hii makala? shirikisha wengi wajifunze.

Previous MAISHA YETU YA KILA SIKU NDANI YA MIOYO YETU
Next WATU WENYE AFYA WANAZO SIRI ZIFUATAZO

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.