YFCS-1024x576-1024x576 Nini Kusudi La Mungu Katika Ndoa Na Familia

Kusudi la Mungu katika ndoa na umuhimu wa mafanikio katika ndoa.

Ndoa ni Mafanikio ya watu wawili. Kuoa Na Kuolewa.

Familia ni kundi lenye wazazi, watoto na ndugu wa karibu wanaohusiana.  Ndoa ni watu wawili tu. Mahali pasipo na ndoa hakuna familia.  Familia ni zaidi ya watu wawili.

Kuna ndoa za watu ambao wameenda kanisani na kuna ndoa za watu ambao wanaishi tu.

Ndoa ni Msingi wa Mungu. Ni taasisi iliyoanzishwa na Mungu. Sio ya kijamii ni ya Mungu. Ndoa na familia ni ya kwanza Duniani. Ilianzishwa zamani na Mungu

Ndoa inapofanikiwa, tambua kuwa unafanikiwa katika mambo yako yote.

Ndoa ilitengenezwa ili kuwepo usaidizi sio kuwepo maumivu. Kwa hio kama uko kwenye ndoa na unapata maumivu, hio sio ndoa yako. Umelazimisha.

Ndoa ina siri kubwa katika kujibiwa maombi hasa kwa wanaume.

Kusudi La Ndoa .

1.Ni Kukutana na Msaada.

Nenda kwenye ndoa na ufahamu wa kutoa sio kupokea tu. Wanandoa wanatakiwa kusaidiana katika maeneo haya makubwa.

Kimwili, kiroho, Kiakili, Kijamii, Kiuchumi, Kisaikolojia, Kihisia na vingine.

2.Kutumika na kusaidiana pamoja

3. Ushirika wa pamoja. kuwa marafiki na wapenzi

4.Umoja. Katika vitu vyote. roho na mwili.

5.Kuzaa na kutunza. Kwa Mungu hakuna tasa.

6.Kuepuka Uzinzi.

Mwanadamu ana asili ya utatu.

1 Mwanadamu kama roho. Hapa katika kiroho kuna falme mbili. upande wa giza na upande wa nuru. Sio rahisi mtu kuishi katika falme zote mbili.  Lakini unaweza kuhamia ufalme mwingine kwa wakati mmoja.

2. Akili. Hapa ni mahali pa makubaliano kati ya watu wawili  katika mambo mbalimbali ya maisha. Ni muhimu watu hawa wawili kukubaliana kabla ya kuoana . Kama hawataweza kukubaliana baadhi ya mambo ni vizuri kuvunja uchumba huo , kwa sabau ndani ya hilo hakuna kulazimishana kuingia mahali ambapo unaona kabisa kuna mapungufu .

3.Mwili.  Hapa kama mtakuwa kwenye ufalme mmoja na mmekubaliana katika akili zenu  ndipo mtaunganishwa  kimwili ili kuwa mwili mmoja.  Hapo mtakuwa huru kila mmoja. mwili wa mwanamke unakuwa wa mume na mwili wa mume unakuwa wa mke.

Kanuni Za Mafanikio.

ne-csp-schedule Nini Kusudi La Mungu Katika Ndoa Na Familia

Kuelewana katika tofauti zenu. kwa kuwa kila mtu katoka sehemu tofauti , hamtaweza kufanana.Mume usimfananishe mke wako na mama yako. wala mke usimfananishe mume na baba yako.

Ushirikiano. 

Shiriki maisha , malengo ,matatizo na furaha, ukiwa na huzuni mshirikishe mwenzako, ukiwa na furaha hivyo hivyo. mpeane mawazo mazuri., mpende mwenzi wako, upendo usio na sababu. mwambie kila siku kuwa unampenda. mchague kila siku.  Hakikisha hakuna kitu kinachoweza kuingilia kati yenu..

Maadui Wa Mafanikio.

1.Marafiki wabaya

2.Uvivu

3. Uchungu na Hasira

4.Kukosa Uvumilivu.

Jinsi Ya Kutafuta Mwenza Wa Ndoa.

1.Tamani kuwa na mwenzi

2.Jiweke mwenyewe fiti. usitafute mtu sahihi, bali wewe ndio uwe sahihi.  halafu umaanishe.

3.Kuwa sehemu sahihi kwa wakati sahihi

4. Ukimuomba Mungu , unatulia na kuanza kushukuru.  uwe na amani , relax na umwamini Mungu.  fungua macho yako kiroho na kimwili. uwe makini kiroho, mwili uwe na nguvu

5.Chukua hatua ya kumjulisha huyo mtu ambaye umemuona. lakini pia heshimu maoni ya mwingine. usichukie kama atasema hapana.

Makubaliano ya watu wawili katika kipindi hiki ni uchumba.  hakuna muda maalumu uliowekwa, lakini ni vizuri kama utakuwa umekamilika  katika mambo muhimu . kama mwanaume kuwa na kazi, nyumba  na awe  na uelewa.

Katika kipindi hiki ukigundua kuna tatizo kabla ya ndoa ni bora hekima itumike.

Subscribe kupata makala mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here