NJIA 10 ZINAZOFANYA NDOA YAKO KUWA NGUMU KULIKO INAVYOTAKIWA.


023901615_prevstill-1024x576 NJIA 10 ZINAZOFANYA NDOA YAKO KUWA NGUMU KULIKO INAVYOTAKIWA.

Unasaidia ndoa yako kugeuka kutoka katika ugumu kufikia ubaya?

Nilipita mahali kwa ndugu yangu  ,  nilisikia  binti akipata ushauri kutoka kwa mama yake kuwa ndoa ni kazi ngumu,  na nilipatwa na mshangao , lakini nikasikia tena  yule binti akisema , vyovyote mama , tunapendana, mapenzi  hayawezi kuwa magumu hata kidogo, kwa hio hata ndoa haitakuwa ngumu.

Lakini mshangao wangu ulikuwa sio sahihi.

Ndoa ni kazi ngumu. Hapana .  lakini sio kama  kazi ya kimwili. Sio ngumu kama kufanya  ndoa na mtu  mwenye ubongo sahihi. ;Lakini ni changamoto, mara zote ni mahangaiko.  Ndoa inahitaji uvumilivu na uelewa. Ni ngumu. Huo ndio ukweli.

Ingawa mara zote inahitaji uangalizi,  haitakiwi kuwa ngumu kama hivyo, na hapa kuna baadhi ya  njia  ambazo unaweza kuwa unaifanya ndoa yako kuwa ngumu kuliko inavyotakiwa.

1.Kujifanya Malikia.

Umalikia wako haufai kuuleta ndani ya ndoa. kama ulikuwa miss world usahau umiss  huo ukiingia kwenye hatua hio , hasa mbele ya mume wako , 

Kwenye ndoa unahitaji uwe mpiganaji, achana na mambo madogo madogo . unamfanya kila mtu kuwa na matatizo, pamoja na wewe mwenyewe.

2.Huwezi Kusamehe Na Kusahau.

Mume  au mke anaweza kuwa amekosea jambo  katika mambo mengi mazuri anayoyafanya ya baraka na ya kufurahia mwaka mzima.  Umewahi kumuomba msamaha? Kwa hio muombe msamaha sasa kwa kutokuwa na kumbukumbu ya jambo fulani . usipofanya hivyo  Unaleta matatizo kwa kila mtu pamoja na wewe mwenyewe.

3.Wewe Ni Bosi.

Unajifahamu kuwa wewe ni bosi, na tangu shuleni  ulikuwa ukijitangazia kuwa  bosi  na hata marafiki walikuwa wakikuogopa  kuwa pamoja.  Acha kumtawala Mume wako  na kumwambia nini cha kufanya , unaleta matatizo.

4.Huwezi Kuaminika

Mume wako anapokuwa na ujasiri kwako,  wewe unachukua mambo ya familia na kuyapeleka facebook ili watu wachangie shida ya kazi yake au shida ya familia. Unampigia mama yako au marafiki zako  na kuwaambia siri zenu.

Acha kuharibu  uaminifu wa mume wako, hawezi kukubaliana na hilo, utasababisha matatizo kwa kila mtu , ukiwepo na wewe mwenyewe.

5.Mtu Wa Kuzoza

Kila wakati ni mtu wa kulalamika, kulaumu na kudharau mume wako kwa kila kitu anachokifanya, hata kama ni kidogo , ingawa kinakuwa hakifikii matarajio yako. Lakini ndio kuongea  zaidi  mpaka inaboa.Unarefusha shingo mpaka inatoka mishipa.

Jifunze kuongea na mume wako kwa ajili ya mahitaji yako na matarajio yako. Halafu kubali kile anachokifanya japo ni kidogo ili aweze kufanya kikubwa zaidi.

6.Wakati wote wewe ndio uko sahihi

Sio kweli. Kubali maoni ya mwenza wako hata mara moja, linaweza kuwa halionekani kuwa linapendeza kwa wakati huo, lakini kwa matumaini. Hukuolewa na mtu aliekamilika kwa kila kitu. Unafahamu anayo baadhi ya mawazo mazuri na yanaweza kuleta suluhisho. Kwa hio acha kufunika akili yako, kubali mtazamo wake. Unaleta matatizo kwa wengine na kwako mwenyewe.

7.Unatisha Mnapowasiliana Kwenye Kutaka Na Kuhitaji

Mwenza wako anakuwa hajui kama huna credit ya kutosha kupiga simu,  Na wala anakuwa hajui kama siku yako imeenda vibaya. Huenda hawezi kusoma nyakati, hawezi kusoma mawazo yako na wote hamuwezi kusoma mawazo ya mtu. Hata kama ukijitahidi namna gani kumwangalia machoni.

Mwambie kitu unachohitaji, na utarajie hicho kitu kutoka kwake, kwa kufikiria kuwa ni lazima ajue hamu yako, utajihangaisha na hapo ndipo unapoleta matatizo kwa kila mtu na kwako mwenyewe.

8.Umekataa Kuomba Msamaha

Unaweza usiwashe moto kwenye ndoa , lakini utaenda kuharibu  kitu fulani kwenye mahusiano yenu. Kama ilivyoandikwa mwanzo kuwa , utambue kuwa  sio kila mara uko sahihi, utafanya makosa. Kwa hio omba msamaha kwake. Acha kujiona bosi, tambua makosa yako. Unaleta matatizo kwa wengine na kwako pia.

9.Unakuwa Na Wasiwasi Sana Kwa Mwenza Wako

Bila shaka  unatakiwa kuwa na wasiwasi , ila usizidi, jaribu kujua anajisikiaje, anahitaji na kutaka nini, kama ana deodorant na  nguo ya ndani kama ni  safi.  Na kama anakuwa na mahusiano ya pembeni na secretary wake. Lakini kuwa  na tabia za zaidi na kutaka kujua  kila anakoenda,  kutaka kujua ujumbe gani upo kwenye simu yake, na kutaka kujua kila mawazo yake inaboa.

Utaleta matatizo kwa kila mtu pamoja na wewe mwenyewe, unaifanya ndoa yako kuwa ngumu kuliko inavyotakiwa kuwa.

10.Hujakua ,

Mstari wa mwisho ndio huu  , hujakua;. Katika kulalamika, kutoomba msamaha, kutokubali msamaha, yatakuwepo kwenye ubosi wako na kukosekana kwa mawasiliano mazuri. Mara utakapokua  mazuri  na furaha  ya ndoa yako  utayaona, kutokukua kwako kunamfanya kila mtu  apate matatizo pamoja na wewe mwenyewe.

Ndoa mbaya mara zote sio kwa ajili  ya ugomvi au kutokuwa mwaminifu  kwa mwanaume. Ndoa mbaya  mara nyingi inazaliwa  wakati mambo yanapokuwa magumu. Ndoa mbaya mara nyingi  inazaliwa  wakati mwanamke anapofanya  mambo kuwa magumu kuliko  inavyotakiwa.

Unaisaidia ndoa yako kutoka kwenye ugumu kufikia ubaya?Unaharakisha mchakato?  Umekuwa sababu ya kila kitu hapo nyumbani? Tazama unachokifanya ambacho kinaleta stress katika kuweka msingi mzuri.

Halafu badilisha hicho, Kila mtu atakuwa na furaha kwa ajili hio.  Pamoja na wewe mwenyewe.

kama umeipenda hii makala  washirikishe wengi facebook

 

Previous KWA NJIA ZIPI NILIACHA KUJARIBU KUDHIBITI KILA KITU KATIKA MAISHA YANGU.
Next HUZUNI---KISABABISHO NA TIBA YAKE

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.