n-COMPASSION-628x314 NJIA 5 ZINAZOZALISHA UPENDO, HURUMA KWA WATOTO WAKO
Kumfundisha mtoto wako huruma ni zawadi ambayo ataitunza katika kutoa.

Sio kitu kidogo siku hizi. kwa sababu ya ubinafsi wa watoto wakiwa bado wadogo unaounganishwa na uchoyo , ambao unatokana na tabia ya mila zao, watoto hawawezi kujifunza tabia ya huruma wao wenyewe. Ina maana kwamba wewe unatakiwa kufanya nguvu ya ziada kuzalisha thamani hizo muhimu kwao kwenye maisha yao.

Uwezo wa kujali wengine lazima utokane na wewe katika kipindi chao cha kukua ndani ya familia yako. Kwa jinsi unavyowasilisha matendo yako kwao , ndivyo wanavyojifunza kuwa na huruma kwa wengine. Wataiga mazuri yote kutoka kwako.

Ishi maisha ya kupenda watu na kuwahurumia watu.

155939-160058 NJIA 5 ZINAZOZALISHA UPENDO, HURUMA KWA WATOTO WAKO

Utakuwa unatoa ujumbe muhimu kwa watoto kwa kuishi maisha ya kujielezea hali ya upendo na huruma kwa wengine. ukiwa unaongozwa na maisha ya huruma, watoto watapata ujumbe huo. wataishi hali hio katika maisha yao.

Watoto wakiwa wadogo huiga matendo ya wazazi wao. kwa hio ukiwa na maisha ya kuelezea upendo na huruma kwa watu. watajua jinsi ya kuwafariji watu. kwa kuwa wewe umekuwa mwema kwao , hata katika vitu vidogo sana , wameona hata jinsi unavyoishi vizuri na dada wa kazi , wafanyakazi wote wa nyumbani mwako. hivyo ndivyo unavyoambukiza mazuri kwao.

Pia unahitaji kuonyesha hisia zako za huruma, wema, jinsi gani unavyojisikia unapotoa huduma kwa mtu unaemwonea huruma. kwanza unahitaji kuwaambia watoto kuhusu hisia ulionayo , lakini kwa kadri wanavyojifunza watatia akili hio ndani yao.

Watu wanaokuzunguka nao wafahamu hisia zako

74957253_XS-1 NJIA 5 ZINAZOZALISHA UPENDO, HURUMA KWA WATOTO WAKO

Kwa kadri watoto wanavyokua, wakutane na hali hio kwa majirani unaowasaidia, taasisi ambazo unasaidia, familia ambazo unazisaidia kwa namna moja ama nyingine, mazingira yako kwa ujumla. Uhakikishe watoto wanapata ujumbe kutoka katika kila kona ya chanzo cha upendo na huruma kwa wengine.

Ongea na watoto kuhusu Huruma

o-BLACK-FAMILY-facebook-1024x512 NJIA 5 ZINAZOZALISHA UPENDO, HURUMA KWA WATOTO WAKO
Family

Wanavyoendelea kukua,unaweza kuanza kuongea nao uso kwa uso kuhusu huruma. hii itasaidia kuendeleza na kuelewa nini maana ya huruma na umuhimu wake kwao, kwenye familia, na kwa ulimwengu wote. Kitu cha msingi ni kuonyesha mifano. kuwa mwema kwa ndugu zao, kwenye jamii na ulimwengu kwa kutoa michango ya nguo, sabuni, chakula , kutembelea wagonjwa .

Kuchunguza Huruma

Walee watoto kwa ufahamu na uelewa wa huruma, haiwezi kuwa ndio mwisho wa kitu kimoja hata maongezi kidogo. Badala tu ya kuwaelezea watoto kuwa ni muhimu kuwa na huruma, Unaweza kuchunguza mifano ya huruma –au kuna kinyume chake, tofauti yake na chuki–katika baadhi ya mitandao, kwa mfano, magazeti, taarifa za habari, na kwenye mitandao ya kila siku inayotoa mifano ya huruma.

Jinsi wanavyozidi kuelewa ndani yao, unaweza kwenda ndani zaidi kwenye vyanzo vingine, kwa mfano, vitabu, television shows, films, na wanaozungumzia huruma kwa undani zaidi na wape nafasi ya kufahamu hayo na kukabiliana nayo. Kusudi la kufanya hivi ni kuwajenga mawazo yao, hisia zao na kuwaweka kwenye vitendo ambavyo ni sehemu ya maisha yao.

Jaribu kuwapeleka kwenye kazi za kujitolea, kutoa msaada kwa wengine.

Hakuna njia kubwa ya kuwaonyesha ujumbe wa huruma kwa watoto kuliko kuwapa uzoefu moja kwa moja kupitia kazi za kusaidia na kujitolea bure kwa ajili ya wengine. unaweza kuanza ndani ya familia, kwa mfano , kufanya kazi ndogo ndogo wanazoweza, kumpa hata mbwa chakula na jinsi wewe unavyowasuluhisha ndugu wanapokosana na kuonyesha upendo wa ziada kwao hata wanapokuwa na mafua.

image NJIA 5 ZINAZOZALISHA UPENDO, HURUMA KWA WATOTO WAKO

Unaweza kuweka sheria ya kuwa pamoja mezani wakati wa chakula cha usiku , nafasi hii huleta upendo wa kipeke yake. na utaweza kumjua kila mtoto na tabia yake. na hapo ndipo utakapoweza kuwaonyesha namna ya kuwa wenye huruma kwa kuwaambia historia mbalimbali. kuongea jinsi kila mtu anavyohitaji kumsaidia mwingine.

Kuna faida nyingi na uzoefu wa moja kwa moja, na watoto wataonyesha ubinadamu wao kwa kuonyesha huruma kwa kuona wengine wanavyowasaidia. wanapata pia uzoefu wa hisia za huruma, wema, kujali, na kutosheka. na watagundua kuwa kuna thamani katika huruma.

Watakuwa watoto wa Huruma Gani

Huruma ni kitu cha kushangaza kwa sababu ina sifa maalumu , kwa mfano , Wema, Upendo, na ukarimu, na hii sio tu itawasaidia watoto wako kuwa watu wenye heshima, bali pia utawakoa vizuri katika maisha yao ya baadae.

Watoto wenye huruma, ni wapole, wachangamfu, huwajibika kwa wengine na kusaidia panapohitajika msaada husukumwa na mioyo yao kufanya mazuri.

Watoto wenye huruma pia ni wakarimu na huwa tayari kujitolea kwa wengine.Watoto wanaoonyesha huruma, wana upendo,thamani na kukubalika na watakapokua, watakuwa na urafiki wa zaidi na wafanya kazi wenzao, wenza wao na wazazi wao.

Na kitu kinachoshangaza zaidi kwa watoto ni kwamba kujielezea katika ushindi wa pande zote. watoaji hujisikia kutosheka na wapokeaji hujisikia kupendwa na kutoshelezwa kwa hilo.
Watoto ni wasikilizaji, ni wasikiaji na ni waonaji. wanahitaji kupata hivyo vitu kutoka kwako.

images-6 NJIA 5 ZINAZOZALISHA UPENDO, HURUMA KWA WATOTO WAKO

 

Umependa hii makala? shirikisha wengi wajifunze.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here