Njia 7 Za Kutumia Muda Peke Yako Zitabadilisha Maisha Yako


980x Njia 7 Za Kutumia Muda Peke Yako Zitabadilisha Maisha Yako

Mwisho mlango umefungwa na kelele zimekwisha. Nilikuwa chumbani mwangu ,Taa zimezimwa hakuwepo mtu yeyote. Ilikuwa ni mapumziko. Tena  kwa muda huo familia yangu ilikuwepo, walikuwa wakipita huku na huku. mara wanafungua hiki mara wanaongea.

Lakini sasa , sasa ninao muda wa peke yangu, nahisi kama  nimemeza dawa ya usingizi inayonilaza kwa haraka.

Usinifikirie vibaya, Naipenda familia yangu, naipenda kweli. Lakini upekee. Naweza kuwa nao kwa muda wa kutosha  kabla ubongo wangu  haujachoka .

Kila mtu anahitaji kupata muda wa peke yake.

Kama wewe ni kama mimi, mtu anayependa mara nyingi kukaa peke yake, wakati mume au mke wako, mtu unayekaa naye chumba kimoja  , watoto wanapoamua kwenda kutembea mahali, Huo ndio wakati wa kukaa peke yako. Wakati mwingine unajikuta hutaki kwenda mahali  hapo ndipo unapotambua umuhimu wa kubaki peke yako.

Utajikuta kwamba kutumia muda ukiwa peke yako inabadilisha maisha yako. tuone hapa kwa nini.

1.Utaonyesha ubora wako  kwa watu ambao wapo katika maisha yako.

kama ulikuwa ni mtu wa kufikiri mabaya kwa kila jambo , utajikuta unawaza mazuri kila mara, utamuwazia vizuri mume wako, watoto wako, ndugu, majirani. Hutakuwa mtu wa kunyenyekea mtu bila sababu  tena . Utakuwa unanyenyekewa wewe.

2.Utakuwa Smart.

Muda wa peke yako utakufanya ujisomee neno la Mungu, utasoma vitabu vya ndoto yako, Akili yako na ubongo wako utakuwa sharp. hutakuwa mtu wa kusahau mambo. Utakuwa unapenda kusikiliza mafunzo yanayokujenga. Kama wewe sio mtu wa kuwa na muda wa peke yako , mtu wa kujifunza kitu kipya , utakuwa sio mtu wa kuwajibika. Hutakuwa mtu wa kuchukua hatua katika maisha yako.

3.Utaboresha Afya yako.

Inafanana na namba 2, Unaweza kutumia muda wa peke yako  kwa kufanya kitu cha Afya Kiakili, kiroho na kimwili. unafanya meditation, unaomba ukiwa mwenyewe, unafanya mazoezi. utajikuta unapunguza au kuondoa kabisa maumivu uliyonayo, unaboresha furaha. hutajisikia upweke, na zaidi sana  utatumia muda wa kutosha kuongea na Mungu. Utajikuta unaondokana na stress kabisa na kuongeza ustawi wa maisha yako.

4.Utaweza kutatua matatizo yako kwa urahisi.

Kila unapoongea na watu , utawaelewa kwa upesi, huwezi kupata shida hata kama wanafikiria ya tofauti, utaweza kudhibiti hali hio. utakuwa mtu wa kutafuta seminar ili kujifunza. utaanza kugundua njia sahihi ya kuongea na kila mtu. utajua jinsi ya kutumia taarifa nzuri unazozipata.

5.Utakuwa mtu mbunifu. Nyakati za Mshangao utaziona

Ni sawa na namba 4, Unapotumia muda vizuri ukiwa peke yako, utaweza kupata vitu usivyotarajia. Utajua haraka kitu gani kitafanyika kabla , utapata ubunifu wa wazo jipya la biashara, kazi, ndoa . Ubongo wako utakuwa sharp kwenye kutatua matatizo  kwa akili ya kiMungu, akili iliyo sahihi, mawazo sahihi, shauku sahihi.

6.Utakuwa na Nguvu Za Kutosha.

Ukitumia muda wako peke yako,  ni njia nzuri ya kupumzisha kila kitu , hata kama wewe ni mtu usiependa kukaa peke yako au uwe mtu wa kupenda kuwa peke yako. Tafuta muda wa kuwa peke yako wakati mwingine.

7.Utajisikia Mtulivu na mwenye Furaha.

Unapokuwa na muda wa peke yako, utaweza kufocus kwenye mawazo yako na hisia zako- Na sio mwingine yeyote. Huhitaji msaada wa mtu mwingine  unapotaka kuwa mwenyewe. Ni wewe tu. Ni hali ya  kujijali. Watu ambao huwa wanajijali ni watu wenye furaha muda wote na ni watulivu kuliko wale ambao hawafanyi hivyo.Kwa  sababu muda wa peke yako  unasababisha kurahisisha mizigo mikubwa ya mawazo yako.

Tumia angalau muda wa dakika 20 kila siku kuwa mwenyewe, mimi sasa hivi natumia dakika 30 za kuwa mwenyewe kwa kufanya meditation. naona faida zake . Kila kitu nakifanya kwa urahisi, natatua mambo kwa urahisi.pamoja na kwamba ni mtu ambaye niko busy sana  sijisikii kuchoka. kila kitu kinakaa sawa.

Lakini  mara utakapoanza kuwa na muda  wa kutosha peke yako, utajikuta  unaona miujiza ambayo hujawahi kuona maishani mwako, hutaweza kutoa jasho kwenye kazi , utafanya kilaini. Utaishi maisha ambayo hujawahi kuishi. huko ndio kuishi wakati uliopo. Ishi sasa kwa kutafuta muda wa peke yako. Kwa nini uteseke na akili yako. Anza kutumia muda wako vizuri sasa.

Nakutakia Mwaka Mpya Mwema Unapoamua Kutumia Muda Wako Vizuri.

Subscribe ili kupata makala nzuri kila mara.

 

Previous Vitu 18 Vya Kuacha Kabla Ya 2018
Next Natumaini Mwaka 2017 Ni Mwaka Ambao Umekufundisha Maumivu Makali Ya kutosha

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.