NURU YA MUDA ( THE LIGHT OF TIME)


churchcollectionbasket NURU YA MUDA ( THE LIGHT OF TIME)

Kitu chochote ambacho unakifanya  lazima kwanza kiwe na Nuru. Unapoona Nuru umeona Pesa. Hazina zote zimefichwa kwenye Giza. Ni muhimu kuitafuta Nuru ili upate Pesa.

Kila mahali ambapo unaona changamoto , au umekwama kwa jambo lolote katika maeneo mbalimbali ya maisha tambua kuwa huna nuru.Kile ambacho unakitaka na bado hujakipata, huna nuru.

Giza halipendi Nuru, Nuru  haipendi Giza. Kitu kimoja kitaamua kuvumilia na kingine lazima kitaondoka. Tafuta Elimu ya Muda mahali popote ilipo. Kukosa Muda ni maisha yaliopotea.

3U7A1452-1024x683-1024x683 NURU YA MUDA ( THE LIGHT OF TIME)

Kitu ambacho kila mtu alipewa na Mungu ni MUDA. Unapoamua kumfundisha mtu muda unaokoa maisha yake. Bango lako ni watu , bila watu huwezi kuishi mwenyewe. Watu ndio wanatangaza  biashara yako.

Nuru ilioko kwenye Neno la Mungu  Inatenda kazi kubwa katika maisha ya mtu.tamka neno kwenye kila kitu unachokifanya. iwe ni biashara, iwe ni ndoa, iwe ni watoto,  kwenye kazi uliyonayo. Hatima ya maisha yako iko kwenye kinywa chako mwenyewe.

Muda wako ukitumika vibaya utatenda  dhambi.

Muombe Mungu akupe hekima  kwenye kitu ambacho unataka kifanikiwe. Kumbuka Nuru ndio  Taarifa sahihi. Maarifa. Ufahamu.

Kiasi cha Taarifa ulizonazo ndio  Nuru yako.  Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa Maarifa. Sio chakula, mavazi au kitu kingine chochote.  Ukimuonyesha Mungu matumizi ya muda wako anakulipa kwa kuwekeza kwako. Kwa kadri unavyotafuta taarifa ndivyo Nuru inavyotokeza kwako. Ukipata Nuru jina lako linabadilika

DHAMBI ILIYOJIFICHA

Kuna dhambi ambazo zimejificha ndani yako bila ya kutambua. Kama  unatumia sana vyombo vya habari, uko mitandaoni , tambua kuwa utakutana na matukio ambayo sio sahihi. Ukiona mtu amefanya kitu kibaya usimseme. ukinyanyua mdomo wako ukamsema tayari umefanya dhambi.

Ukiona ujumbe mbaya , wa kumsema Raisi, wa kumsema mtumishi wa Mungu, Achana na huo ujumbe usitume kabisa. futa. Kwa sababu kama ukishare utatenda dhambi.

Ukiwa unawazia watu mabaya, unajiwazia mabaya wewe mwenyewe, hizo ni dhambi zilizojifichwa ndani yako, hata kama unaonekana mtu mtakatifu kwa nje .

Ukiona unapita kwenye changamoto nyingi , tambua kuwa unadaiwa Muda na Mungu. Ukiona huna Furaha, Amani, Uvumilivu, Fadhili, Uaminifu, Tambua kuwa Unadaiwa Muda na Mungu. Tambua kuwa Mungu hayupo ndani yako.

Mtu mmoja tu alifanya dhambi ikaingia kwa watu wote. kwa hio wewe ukiruhusu ujumbe mbaya upite kwenye simu yako, utasababisha wengine kutenda dhambi. Kuwa makini na dhambi zilizojificha.  Mitandao ya kijamii  ndiko kunatokea dhambi zilizojificha.

Dhambi ya kurusha matukio mabaya.  Uwe na nidhamu unapotumia mitandao, uwe na nidhamu na akili yako. Tumia Muda wako vizuri.

Mungu akupe Nuru ya kuona fursa za kazi, biashara, ndoa nzuri, amani, furaha na Upendo.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

Previous Wakati Mwingine Mapenzi Ni Rahisi
Next Unahitaji Kitu Gani?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.