SIFA 23 ZA KIJANA ANAESTAHILI KUWA NAWEWE BINTI.


Kuchunguza.1261205 SIFA 23 ZA KIJANA ANAESTAHILI KUWA NAWEWE BINTI.

Inaweza kuwa ni kazi ngumu sana  ya kutafuta sifa kwa kijana ambae uatoka nae, lakini nataka nikusaidie japo kidogo ili  uweze kujua kama uko na kijana sahihi katika maisha yako. ziko zaidi ya sifa 100 na zaidi, lakini nakuletea  23 zinazoamini kila mwanamke angependa  kufanya uchunguzi na  kuzikuta kwake.

Sifa hizi zitakusaidia , ilimradi uwe mtu makini na mwenye udadisi , usiwe mtu wa kujishusha eti kwa sababu tu unataka  kuolewa. kumbuka kwamba unahitaji  ndoa  na sio harusi tu. pia unahitaji familia  , kwa hio usikubali kirahisi rahisi, usitulie  kufanya uchunguzi ni lazima, mungu hajakuumba kutulia.

1.Awe anampenda Mungu.

2.Awe anajiendesha maisha yake.

3.Awe na malengo yenye mwelekeo.

4.ni mwelewa.

5.Awe anakuunga mkono. 

6.ni mwaminifu.

7.Anawaheshimu wazazi wake.

 8.awe anakuheshimu na ni msafi

9. anaonyesha uvumilivu.

10. ana mtanguliza mungu kwa kila jambo.

 11.Ana uaminifu wa kutosha na  kustahili.

 12.Anaaminika katika kazi zake na matendo yake.

13. Awe ni mtu anaevutiwa na wewe, yaani uwe na mvuto kwake.

14.Ni mtu anayependa kusaidia wengine, hasa wale wenye mahitaji.

15.awe ni mtu anayekuombea , na muwe mnaomba wote.

16. ni mtunzaji mzuri wa pesa.

17.Ana sifa nzuri .

18. Yuko tayari kufanya kazi kwa bidii na awe ni mtoaji.

19. Hafanyi maamuzi ya pupa.

20.Hana mdomo mchafu, yaani haongei upuuzi mbele yako na watu wengine.

21.Ana tabia nzuri.

22. awe ni  mtu anayeonekana kukulinda na kitu chochote.

23.Mara zote hufikiria vitu vyenye akili, na awe na mwanga wa maisha.

Ni safari ndefu  ambayo utakuwa nayo  na unaweza usipate mtu mwenye sifa zote hizi,  lakini najua umepata point yangu ambayo nimejaribu kukupa hapa, ila namuomba mungu akusaidie  angalau upate hata nusu ya hizo sifa. na zilizobaki mungu akusaidie kuzirekebisha.

Kwa sababu hakuna mtu mkamilifu  duniani , aliyemkamilifu ni Mungu peke yake. basi uwe tu makini ili upate mtu ambae utampenda maisha yako yote. si unajua kukalika kwa maisha kunahitaji mambo mengi , na hili ni kubwa katika maisha  yetu sote  la kupata mtu umpendae na yeye akupende.

dalili 7 za kujua kama uko na mwenzi sahihi.

shirikisha  marafiki na watu wengine wa karibu yako na usiache kutoa comments hapo chini.

Previous JAMANI! KAMPA TALAKA MKE WAKE 2015,NI MBAYA, LAKINI NAMUUNGA MKONO:
Next SIFA 23 ZA MWANAMKE ANAYESTAHILI KUWA NA WEWE KIJANA:

3 Comments

  1. […] sifa 23 za kijana anaestahili kuwa na wewe binti. […]

  2. […] sababu huendi tu kuolewa na mtu yeyote ni lazima kuwe na sifa uzitakazo.Sifa 23 za kijana anaestahili kuwa na wewe binti. hapa kuna mambo mengi , maana kuna wasichana ambao hujitangaza kuwa wapo tayari kuolewa , wako […]

  3. […] sababu huendi tu kuolewa na mtu yeyote ni lazima kuwe na sifa uzitakazo.Sifa 23 za kijana anaestahili kuwa na wewe binti. hapa kuna mambo mengi , maana kuna wasichana ambao hujitangaza kuwa wapo tayari kuolewa , wako […]

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.