Sitawisha Sifa Zinazompendeza Mungu


Creative-God Sitawisha Sifa Zinazompendeza Mungu

Bila shaka , kumpendeza Mungu  kunahusisha mambo mengi zaidi kuliko tu kuepuka  mambo yanayo mchukiza.

Kitu kikubwa unachohitaji ni kupenda mambo ambayo Mungtu anayapenda. Pendo lako lisiwe na unafiki ndani yake. ni bora kuchukia uovu na kufuata yalio mema.

Mambo yanayomchukiza Mungu. 

Matumizi mabaya ya Muda

kukosa maadili

Kukosa Hekima, maarifa, Ufahamu.

Kukokuwa na Imani.

a6ca57a026a5106bb378f1be7c79c907-righteousness-roman Sitawisha Sifa Zinazompendeza Mungu

Jiulize, huvutiwi na watu walio na maoni, mapendekezo, watu walio na viwango kama vya kwako?  Hata Mungu huvutiwa na watu kama hawa pia. Kwa hio jifunze kupenda mambo ambayo Mungu anapenda.

Baadhi ya mambo haya yametajwa katika Zaburi 15:1-5.  Ni mtu mkamilifu na mtenda haki,  kusema kweli kwa moyo wako, Asiyesingizia, hakutoa pesa yake ili apate riba, Hakumtenda mwenzake ubaya. Pia  Tunda la roho , utapata kwenye Wagalatia 5:22,23. upendo, furaha, amani, utu wema, fadhili, uaminifu, upole , uvumilivu na kiasi. Roho saba za bwana Utapata Isaya 11:2. roho ya hekima, ufahamu, ushauri, maarifu, roho ya kumcha bwana, roho ya bwana na roho ya uweza.

Kujisomea pia kunastawisha  sifa za kumpendeza Mungu. kuishi maisha yanayompendeza Mungu. jitihada inahitajika ili uishi maisha ya kumpendeza Mungu.  Kubadilika au kuokoka ni kuvua utu wako wa kale na kujivika utu mpya. Kuishi mapenzi ya Mungu kunaleta thawabu kubwa. Mungu atakufurahia .

A-beautiful-life-does-not-just-happen-it-is-built-daily-by-prayer-humilty-sacrifice-and-love-1024x576 Sitawisha Sifa Zinazompendeza Mungu

Kumkumbuka Mungu kila inapofika saa kamili, kutoa dakika moja tu kwa kila dakika 60, Kumshukuru Mungu na Kumsifu Mungu , Toa dakika moja kama mbegu katika Ufalme wa Mungu. Utaupendeza moyo wa Mungu. 

Kuikumbuka siku ya bwana , kwa kwenda kanisani , msikitini na sehemu zingine za ibada,Unamtukuza Mungu na kustawisha sifa  za kumpendeza Mungu.

Kufanya na kuamini kazi za Yesu.  kazi za Yesu ni kwenda kuwaona Yatima na Wajane, kutembelea Wagonjwa, Wafungwa na wasiojiweza.

Kufanya Kazi ya Adamu. Kazi ya Adamu ni kutunza mazingira. Anza na ya nyumbani mwako kisha toka kusafisha mji wako . Hii itaupendeza moyo wa Mungu. Itaongeza sifa za kustawisha  moyo wa Mungu. Na kila utakalohitaji utatendewa na Mungu.

Mtu anayetoa zaidi kuliko kupokea , mara nyingi Mungu humpa zaidi. Kwa hio toa , wape wazazi, yatima, wajane na wenye uhitaji wa kweli.

Ukipigana na Roho ya Pesa , utastawisha sifa zinazoimpendeza Mungu.

Subscribe kupata makala mpya.

 

Previous Love Is Full Of Brokenness.People Still Need Healing
Next Umesahau Kununua Zawadi Kwa Ajili Ya Mwenza Wako?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.