TABIA 4 AMBAZO KILA MTOTO ANAHITAJI AKUE AKIWA NA FURAHA.


CHILDREN1-1024x494 TABIA 4 AMBAZO KILA MTOTO ANAHITAJI AKUE AKIWA NA FURAHA.

Sijawahi kukutana na mzazi ambaye hapendi mtoto wake  awe na furaha, lakini  mara nyingi wazazi wanakuwa wanawazia mambo mazuri watoto wao,  na kutoka kizazi hata kizazi  kunakuwa na mafunzo ya kuwezesha maisha bora ya watoto

Kwa kufupisha  huu umuhimi wa uchunguzi , furaha ina vitu vitatu vikubwa .

.Furaha

.Ukaribu

.Maana

Wazazi wengi hupendelea watoto wao wawe na furaha ya amani .ili wafurahie watoto.mtizamo wa furaha  una leta hamu na  uhitaji wao, na vitu vizuri . hujaribu kuwapeleka sehemu mbalimbali za michezo ili wafurahi,  na mara nyingi hutengeneza vyakula wanavyovipenda watoto na kupanga michezo mingi ili kukutana na watoto wenzao na  zaidi .  hii hufanya watoto wajisikie vizuri , wawe na furaha  na wanapata wanachohitaji.

Ukaribu  ni kutengeneza  nafasi ya watoto  kukutana na changamoto, kazi hii  mara nyingi  inaonyesha kitu ambacho tunakifanya . muziki na michezo ni mfano wa kawaida , lakini ukaribu ni kazi  inayoonekana ngumu kwetu kuifanya kwa watoto. Ujuzi wetu wa kulea watoto uko mikononi.

Umuhimu,  kazi ya kutengeneza ukaribu  mara zote  ni ngumu  na inashida kuifanya kwa sababu ya  majukumu tulionayo.

Maana. Pia inaelezea  huduma ,  inatumia uwezo wetu  kuchangia uzuri wa watoto. Tunapoingia kwenye maana  tunalenga zaidi  kuvuka mipaka ili kupata kusudi  zaidi kuliko malengo na hamu tulizonazo katika maisha . kujali na  huruma ni  sehemu ya mradi wa maana.

Maana na ukaribu unatufanya  tuwe na furaha kuliko   kitu kingine kinavyofanya. Maana pia inaleta furaha kwa wengine. Kwa hio uakaribu wenye maana  ni tabia  ya furaha.

Mazoezi yanaweza kuwa ni moja ya kitu muhimu  kwa mwanadamu.

Ufunguo mwingine wa furaha ni shukrani.

Shukrani ni sehemu ya baraka,  vyovyote itakavyokuwa , uwe ni mtu wa shukrani bila ya wasiwasi na huzuni na kuboresha akili, hisia,  na  afya ya mwili. Shukrani pia  inakuza mahusiano. Na ni moja ya  furaha- kwa sababu inatuonyesha jinsi tunavyofurahia  kazi za wengine.

Ufunguo wa nne  ni  tabia ya furaha ambayo mara nyingi   inafungiwa na mazoezi . mazoezi ni kazi ya kimwili yenye faida za kiafya ya akili . watu wanaofanya mazoezi  sio tu kuwa wana afya,  wana furaha pia. Mazoezi yanaleta afya ya kiwili na afya ya akili, ambazo ni muhimu kwa wanadamu.

Idadi nyingine yenye tabia ya furaha inweza kuwa ni msamaha, utulivu,  mawazo mazuri, wema.  Lakini nimegawa hizi katika  mafungu manne – ukaribu, maana , shukrani na mazoezi- kwa sababu  vinaleta  tabia zingine za furaha  na pi kwa sababu  vinatuweka sawa kati yetu( ukaribu na mazoezi) na pia kulenga  mahusiano yetu  na mawasiliano ( shukrani na  maana).

Unafanyaje kuhakikisha kuwa watoto wako wanakuwa na funguo hizi nne zenye tabia ya furaha?

Hapa kuna mbinu  nzuri, lakini pia kumbuka kuwa kama huzionyeshi hizi tabia kwenye maisha yako, ni kiasi kidogo sana watoto wako wakawa na hizi tabia , ni ngumu kuziiga.

1.Ukaribu.

Mtoto wako kuna jambo analolipenda   au kazi  ambazo huzipenda kuzifanya? Je vitu hivyo unaweza kumtia moyo kuendelea navyo  kama ni ujuzi alio nao, Na je kazi hio inaweza kuleta changamoto za kuendeleza hicho anachokipenda?

Hizi sifa mbili-akili za muda huo alionao zina alama yeyote ya  kuwa atakiendeleza wakati akikua- zina ukaribu na zile kazi anazozipenda.

Kwa watoto wadogo  kucheza kwao ndio kazi zao, kwa ratiba zao za kila siku. Hakikisha ratiba hizo  ziwe na mpango sahihi wa muda. Kwa watoto wa (miaka 7 na kuendelea), wasaidie kutambua  ukaribu mwingine wa kazi ambazo wanaweza kujifunza wanapokua. Kama bado hajaonyesha kitu anachokipenda mwenyewe kwa muda huo, mziki na michezo ni hatua ya kwanza kuanzia, lakini mwanzishie kazi nyingine yenye ujuzi tofauti ili kumpa changamoto , kama vile  art,  bustani au  ufundi.  Uwe na uhakika wa  kutunza muda wa kucheza pia.

2.Meaning.

Mtie moyo mtoto wako kufikiri kuhusu  ulimwengu unaomzunguka,  kujitolea ni moja ya njia  nzuri  ya kuleta maana ya maisha. Lakini  kazi yeyote ambayo inaonyesha wema  na kujali ndio zifanyike. Hii inaweza kuwa kupeleka na kuchukuwa kitu kwa majirani,  kutoa msaada kwa  watu wenye matatizo, au kuandika barua kwa   siasa za kienyeji kulalamikia  matatizo na vitendo vinavyotokea katika jamii.

Hii ni kutunza akili kwamba hatua ya kujitolea kwa ajili ya wengine ni nzuri kuliko kitu chochote,  kama mwanao atashikilia malengo hayo na kuwa anatoa huduma kwa watu ni nafasi nzuri ya kufanikiwa kwa maisha yake ya baadae, ni chuo  hasa hicho.

3.Shukrani.

Njia moja  nzuri ya kusaidia watoto kuendelea na tabia ya shukrani ni kwenye  sehemu ya chakula mnachokula kila siku. Mchana, usiku, kwa mfano, unaweza kuanza kuwafundisha kusema asante kila baada ya kumaliza kula chakula, unaweza kuwauliza kila mmoja kitu gani kwa siku hio amekifurahia. Watasema  kuwa wamefurahia  labda  kuchukuliwa mapema  kurudi nyumbani. Au wamefurahi siku hio baba kawafuata shuleni, na vitu vingine.

Kitu kingine cha kuonyesha shukrani ni  kumshukuru mtu kibinafsi , kwa kupata kitu chochote kutoka kwa huyo mtu, au hata kwa  kuwepo pamoja.

4.Mazoezi.

Mazoezi yanaweza kuwa ni sehemu ya  maisha yako na watoto wako kila siku. Lakini sio lazima yawe ya kwenda gym au hata kuyaita mazoezi. Kwa watoto,  mazoezi ni yale ya kucheza tu kawaida., watoto wanapita huku na huku  na hata kutoka jasho hayo ni mazoezi, hayo yanahesabika. Washauri wanasema  angalau dakika 60 za kucheza  kwa siku  kwa watoto na wale ambao wako karibu kubalehe  zinatosha .

Weka T,V. mbali na sehemu ya kucheza watoto au usiruhusu kila wakati watoto kuangalia T.V, Weka muda maalumu wa kukaa pamoja na familia kila baada ya chakula cha usiku , au unawapa muda maalumu wa kukaa kwenye T.V. Muda mwingi watumie kuongea , kucheza  kusoma na vingine., watumie t.v kwa  kupata mafunzo maalumu tu.

Kwa mfano  unaweza kuwa na   movie za kifamilia  ambazo  mmepanga kuangalia kila siku ya jumamosi , ama  video game za mashindano ya kifamilia.

 

Previous Best Messaging Apps in 2016 for your smartphone
Next UTAELEZEA NINI BAADA YA KUFIKIA UMRI WA MIAKA 25.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.