naturally-attractive-man-1024x503 TABIA 7 ZINAZOMFANYA MWANAUME AONEKANE ANAVUTIA

Unategemea ushauri wa kuonekana handsome, au kwa ajili ya mazoezi, au mrefu, mtanashati, umekosea. Aina ya ushauri huo hautatui tatizo.

Utakachojifunza hapa ni  kitabia na kiakili ambazo zinaongeza mvuto wako.

Utajuaje hili?

Unaweza kujilinganisha mwenyewe na mwanaume mwingine mwenye  uwezo wa kuongea na wanawake kwa ujasiri na kuwa mwenye uhakika na kile anachokihitaji kwa mwanamke.

Ngoja nikuwekee akili yako kwenye ukweli ambao utakuwezesha kuongea na mwanamke  unayemtaka kuwa naye, kutoka naye.

Kwa hio uko tayari? Tuanze.

1.Uliza maswali ya kuwezesha

Unatembea barabarani unamuona mwanamke mzuri na anapita karibu yako na unahitaji kuongea naye. Nini kinaendelea akilini mwako?

Utakuwa unajiuliza maswali, kama akinikataa? Au vipi kama nitajisikia vibaya asipokubali mwito wangu?

Yapo maswali mawili, yale yenye kuwezesha na yale ambayo sio ya kuwezesha.

Yanayowezesha yanakupa nguvu na yale mengine yanakufanya ugande.

Aina ya maswali unayouliza  yanalenga  ulichokichagua na jinsi unavyojisikia.

Unapofikiria kuwa hutafanikiwa , utasikia woga. Lakini kama utalenga katika kufanikiwa  na kuna kitu utajifunza  kutokana na hali hio, utajisikia mwenye nguvu.

Wanaume wenye malengo mazuri na wanawake wanaowataka, maswali yao huwa na nguvu na hujisikia kuwa na furaha kuongea na mtu ambaye ametaka kuongea naye.

Tofauti iliopo kati ya mwanamke na mwanaume ni kutokana na nguvu ya maswali na majibu yaliopo.

Kwa hio kama utaanza kujiuliza maswali ya kama akinikatalia mbele ya kila mtu, Akili yako itatazama  jibu, hata kama halina akili hilo swali, majibu yatakuja kutokana na hilo unaloliwaza, Unaweza kweli kuonekana mjinga mbele ya kila mtu. Majibu ya swali lisilo na nguvu  yanaleta hisia  za mashaka na kukosekana kwa ujasiri.

Lakini kama utaanza kujiuliza maswali mazuri kama , napenda awe wangu?, au kitu gani nitajifunza kutokana na matokeo yajayo? Akili yako itaanza kutafuta majibu  kama vile , siwezi kukataliwa, ni lazima niongee naye, au naweza kutumia uzoefu huu kwa kuboresha ujasiri wangu wa kuongea na mwanamke.

Kwa hio akili yako itaanza kufanya kazi hio na hisia zako zitaanza kuwepo kazini.kuwa makini na maswali unayojiuliza. Kila wakati unapohisi mashaka au hisia za kukataliwa kuwa makini nazo.

Dhibiti akili yako na anza kujiuliza maswali yenye nguvu ya kukuwezesha kushinda na kutegemea  kuongezeka kwa ujasiri unapoongea na wanawake.

2.Meditate

download TABIA 7 ZINAZOMFANYA MWANAUME AONEKANE ANAVUTIA

Jifunze kumeditate, kwa sababu meditation inakufanya uwe mtulivu na unarelax unapokuwa unaongea na mwanamke.

Wanaume wengi wanateseka na wasiwasi pale wanapokuwa wanachat na wanawake wazuri.Kujifunza kumeditate inakuwezesha kuwa halisi, mkweli, na mtulivu kwenye uwepo wa mwanamke, hutakuwa na woga.

Meditation inarekebisha stress. Kwa hio kabla ya kwenda mahali meditate kwanza. Wachunguzi wamegundua kuwa wanaume wanaomeditate wanavutia.

3.Kuwa na mshikamano

Kuwa na mshikamano na mawazo yako, maneno yako na matendo yako.

Kwa mfano; kama unataka kumkiss msichana, lakini ukafikiria kukataliwa, na unajaribu kuficha hisia zako kwa vitendo, utaanza kujisikia mnyonge. Mawazo yako hayako pamoja na maneno na vitendo.

Kwa hio kama unahisi kumkiss fanya hivyo, usisubiri wakati mwingine mzuri, huo ndio wakati mzuri. Wewe fanya hivyo.

Lakini kama utaogopa kufanya hivyo na unaficha hisia zako kwa kuonyesha madhaifu yako kwa kuonyesha dalili ya kutaka kufanya hivyo,ni mwanaume wa kuvutia. Kwa kadri unavyoficha hisia, unazidi kupunguza ujasiri

Kinachoonyesha ujasiri hapa ni kuwa na wasiwasi huku ukijaribu kuficha wasiwasi na kutokuwa na woga wa kuonyesha hicho. Unavyojionyesha jinsi ulivyo unakuwa unavutia na msichana atataka kukusikiliza zaidi.

4.Uwe mcheshi

Mwanaume mcheshi ni yule ambaye hufanya hivyo bila ya kutaka kupata kitu kwa mtu.Uwe mtu mcheshi na utakuwa wa kuvutia.

Kama utaongea utani iwe ni kwa ajili yako pia , usifanye kwa ajili ya mtu mwingine ingawa  atafurahia na kucheka sana.

Kama utaanza kujijali mwenyewe, utakuwa na ujasiri  sio kwa watu wengine tu bali kwa ajili yako. Hii inavutia watu kwa sababu sio tu kwa sababu unafurahisha bali  umekuwa na mvuto wa kipekee.

5.Kuwa mwenye shauku

Ipo tofauti kati ya mtu mwenye shauku na yule asie na shauku. Kama utasema kitu chochote  kwa shauku ya kutosha , kitapokelewa kuliko kama ungeongea bila shauku.

Kuwa na shauku ina maana kuwa akili yako ni ya kipekee, sio tu kwa ajili ya mwanamke bali hata katika mambo mengine. Ina maana hata kama uko single huwezi kujisikia mpweke kwa sababu unacho kitu cha kufanya na ambacho unakitazamia.

Wanawake wanapenda kujua hilo , kama ukiwa mwenyewe bila yeye utaweza kujimudu na hutaharibu mahusiano yenu.Hicho ni kitu kikubwa sana ambacho utakuwa unakifanya wakati mwenza wako hayupo na wewe. Hicho ni kitu cha kuvutia .

6.Usijikatae

Watu wengi ulimwenguni waliofanikiwa, hasa wale ambao wako vizuri katika kuongea na wanawake, wanatofautiana katika kukataliwa, ukilinganisha na wale ambao hawawezi kuongea na wanawake

Ninachokifahamu ni kwamba msichana anapokukataa huwa hakukatai kabisa, hukataa wazo ulilokuja nalo.  Sababu pekee ambayo unayo wewe ni akili yako inavyowaza, kukataliwa au kukubaliwa.

Fikiria kuhusu hili unakataa watu, hata wengine hukataa watu. Kama tukiwa tunakataa watu kila kitu kitakwenda vibaya.

Kwa mwanamke kukataa kuongea na wewe huenda alikuwa na siku mbaya au ulikutana naye muda mbaya . lakini hulioni hilo, unafikiria tu kuwa amekukataa wewe ulivyo.

Kukataliwa ni sehemu ambayo ipo ndani yako, kwa sababu umejikataa ndio maana unakataliwa. Kitu kingine ni kuhusu  wazo lako ulilokuwa nalo, na wakati mwingine unaweza kukataliwa kwa sababu ni mgeni kwao , hawakufahamu . kwa sababu hio baada ya kukataliwa unatakiwa uondoke na tabasamu. Hio itakuonyesha kuwa uko strong.

7.Boresha mwonekano wako.

Wanaume wanaofanikiwa kuwa na wanawake wazuri ni wale ambao wamejiendeleza  vizuri.

Unafikiria  mwonekano wako ulivyo, unaweza kumkaribia mwanamke unayemtaka? Unahisi kukosa ujasiri. Unajihurumia mwenyewe jinsi unavyojiona akilini mwako

Lakini ukijiona kuwa mwanaume mwenye mafanikio  kwa mwanamke, utajisikia mwamko mkubwa ndani yako.shauku hii itasababisha  uchukue vitendo na kuonyesha mwonekano wako kuwa halisi.

Wengi hawajui, lakini unaweza kujibadilisha, sio vigumu.

Kwa kuboresha mwonekano wako kama mtu mwenye mafanikio , kukataliwa hakutakuwepo kwako.

Unaweza kujiuliza , haya yanatokeaje?

Ni kwa sababu kila unachokifanya kwa ajili yako , utafanya na kwa wengine. Na matokeo ya akili yako  inapochagua mawazo mazuri.

Ukiamini unaweza, utaweza. Ukiamini hutaweza ni kweli hutaweza. Na kukataliwa kutazidi kuja kwako. Kila unapotuma ujumbe , usipojibiwa unaumia moyo na hisia zako zinaumia .

Sasa, kwa sababu umefahamu hili , chukua muda wa dakika 30 kwa siku ili  kujitazama jinsi unavyotaka kuwa. Tambua jinsi unavyojisikia, na jinsi ambavyo mtu mwingine anaweza kujisikia.

Unapokaa na kutulia, kujitathimini, utakuwa mtu tofauti mwenye kujiamini, na utaweza kuwa na maswali yenye kuwezesha  na yenye nguvu.

Akili yako itaweza kuwa na ufahamu kuwa unapata kila unachokihitaji.

Kila la heri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here