Tabia Zinazobadilisha Maisha Kwa Urahisi


9f4ca98b43bb04787105bbe616d4e63b Tabia Zinazobadilisha  Maisha Kwa Urahisi

Maisha yanabadilika unapomkaribia Mungu.

Wanadamu wote wanahangaika, Lakini kuna waliozidi zaidi katika kuhangaika .Jifunze kumkaribisha Mungu.

Wachunguzi waligundua kuwa hatua ndogo unayoanza kuchukua inaweza  kukupeleka mbali. Ufunguo ni katika kuchukua hizo hatua ndogo ili uweze kupata mwelekeo.Kujenga maisha makubwa ni kubadilisha tabia, ingawa  ni ngumu .Ni ngumu kutunza nguvu hio kwa muda mrefu ili kuona badiliko.

Lakini ziko tabia ndogo ndogo za kuanzia ambazo zitakuwezesha kufuata mwelekeo wa tabia kubwa zenye  kuleta matokeo makubwa.

Tabia hizo ndogo ukiziongeza kwenye maisha yako ,Huwezi kuona kama ni kubwa, lakini kama ukizizoea  mara moja moja zitakuwa ni kawaida kwako, zitabadilisha kiasi cha nguvu zako , mazoezi yako, mahusiano yako , kazi yako, mawasiliano yako na mazingira yako… katika njia moja kubwa sana .

1.Tabia ya kuwa na afya bora ya mwili.

Tumia glass ya maji ya uvuguvugu kila siku asubuhi kama upo sehemu za baridi, au maji yenye joto la kawaida kama  uko sehemu za joto kama Dar es salaam. Wengi tunatumia kahawa au chai asubuhi kabla ya maji. Jizoeshe  uwe na tabia ya kutumia maji kabla ya kitu chochote. kwa sababu ya mizunguko mingi mara nyingi unaweza kujikuta hutumii maji unatumia soda au juice. Lakini nakushauri tumia maji kila siku asubuhi iwe ndio tabia yako.

480390164_XS Tabia Zinazobadilisha  Maisha Kwa Urahisi

2.Fanya mazoezi japo dakika 10 mpaka 3o. iwe ni mtindo wako wa kila siku. au kama unaweza kutembea mwendo wa dakika 30 sio mbaya. Kama una gari  jaribu kuwa unafanya mazoezi kabla ya kuanza utaratibu wako wa kuondoka. Hii itakusaidia  kuondokana na madhara ya kukaa muda mrefu kazini.

3.Kula matunda yasio na sukari nyingi au kula mboga za majani   kwa kila mlo. Wakati wote fikiria kijani kuwa ndio saladi yako. kipande cha limau,  karoti, tango. Sio tu yatakupa lishe bora bali utapunguza uzito mkubwa.

4.Ukiwa kazini kila baada ya saa moja simama na ujinyooshe.  jaribu kukaa mbali na simu , laptop kwa muda. Ni afya kwa mwili wako na ubongo wako. Sio kazi kubwa ni uamuzi tu.

5.Beba karanga ndani ya begi lako , ukisikia njaa kula , inasaidia kukupata nguvu na kuondoa njaa, na kujenga misuli yako vizuri.

Tabia bora ya afya ya akili.

1.Panga mawazo yako mwenyewe. Soma vitabu mbalimbali, sikiliza  masomo yanayofaa kwenye akili yako. Achana na habari zinazokushambulia akili yako. Uwe na mtazamo ulio wazi, jaribu kusaidia wengine kama unaweza. Pata marafiki wapya, Jifunze njia mpya za mafanikio. Fikiria hekima ambayo unaweza kuijenga ndani ya miaka mitano na zaidi, kama utakuwa mtu wa kuuliza maswali na kutaka kujua.

2.Kaa mahali penye ukimya kwa dakika kadhaa kila siku.  Hatuiti hii kama meditation, kwa sababu hapa hutaweza kunielewa.  ni muda wa kutulia tu peke yako. Hauhitaji kukunja miguu, huhitaji kufunika macho. Ubongo wako unatakiwa kutulia. lakini usiongee wala  kufanya kitu kingine, just sit, vizuri,na pumua kwa urahisi kwa muda wa dakika kadhaa.

3.Chukua karatasi na kalamu andika yaliopo akilini mwako, kisha yafute kabla hujaenda kulala . kwa sababu kufanya hivyo utapunguza  au kuondoa kabisa wasiwasi na huzuni iliokuwepo ndani yako.

4.Jaribu kurudisha mawazo mazuri  ili kuondoa stress iliokuwepo.  Fanya kitu rahisi ambacho ni cha kukumbuka . Hii ni njia nzuri ya kufundisha ubongo wako. Na kusema kuwa kila kitu kitakwenda vizuri. Mimi napenda kusema hivi. Hata hili litapita tu. Nina nguvu kuliko ninavyofikiri. naweza kujifunza kila ninapohitaji kujifunza.Siko peke yangu. Kuna uhuru ndani yangu.

Tabia bora ya Mahusiano.

1.Piga simu, tuma ujumbe au email kwa familia yako au rafiki yako kwa siku.  Hali hii mara nyingi inakuwa ni ngumu.  Upo urahisi tu tunapokutana na wafanyakazi wenzetu tukiwa kazini, kwa sababu tunawaona kila siku. Fanya zaidi , katika kuwakumbuka familia, marafiki unaowathamini.  Itakuchukua muda mfupi tu kufanya hivyo, Kuwa ni mawasiliano mazuri  na watu wanaokuzunguka, wote wa karibu na wa mbali.

2.Waambie kuwa una shukuru kwa kuwa na familia hio, marafiki hao,  Waambie maneno mazuri ya upendo, au andika kinote na ukitume ,  Ni vizuri kuwa mtu wa shukurani kuliko kuwa mtu mwenye woga. Jijenga katika kushukuru kwa kila kitu kilichopo maishani mwako.

Maliza siku yako kwa shukurani. Shukuru kwa ajili ya mwenza wako, masomo yako, kazi yako, watoto wako, maisha yako . hii inasaidia kuondoa mawazo mabaya na huzuni yeyote.

3.Jifunze kusikiliza badala ya kujibu. kwa kupata muda zaidi wa kufikiria  wakati mtu mwingine anaongea. Hii sio tu inaonyesha kuthamini  kile kinachoongelewa , ila inaonyesha kuheshimu na kukubali,pia inakupa muda wa kupima tabia na maneno.

Jipe muda wako mwenyewe, maisha yanatokea.  utakapokutana na stress, kuchanganyikiwa , hasira, au kutovumilia wakati unapokutana na mambo mengi. Kama utakuwa na muda wako, utaweza kuweka mambo sawa, hutaendeshwa kama robot.

Jiambie maneno mazuri kila siku, maneno ya kukutia moyo, maneno ya kukujenga,  maneno ya ujasiri,  maneno ambayo yatakufanya uwaze mazuri .Jifanyie wema . Unachotaka kufanyiwa wewe, anza kujizoesha kuwafanyia wengine.

Jifunze kumkaribia Mungu ndani yako.

Toa maoni yako. Ngoja nikufundishe kitu kidogo hapa ninapokuambia toa maoni yako. ukipata kitu toa kitu. unapotoa maoni yako yanayohusiana na makala hii utawasaidia wengi. utakuwa umefanya kazi ya Kuelimisha kupitia hapa. Mungu akubariki unapofanya hivyo.

Kisha Subscribe ili kupata makala mpya.

Previous Inaumiza Kuwa Mwanamke Mwingine
Next Fahamu Kuishi Kwa Amani Wakati Wengine Hawawezi

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.