Tambua Uwezo Wako Ili Kutimiza Kusudi


tHAMANIpICHA Tambua Uwezo Wako Ili Kutimiza Kusudi

Kila samaki  anao uwezo wa kuogelea lakini anahitaji mazingira sahihi.

Kila kiumbe kina uwezo usiozuilika  kwa ajili ya kupata mafanikio maishani mwake, lakini kitu kikubwa anachohitaji ni maarifa na sehemu sahihi.

Mafanikio.

Ukitaka kujua kuhusu kuzaa ni lazima uongelee Utasa. na ukitaka kujua mafanikio ni lazima uongelee Umaskini. Ni kitu gani utasa? Ni kuwa mkavu kila sehemu.

Unakuwa mkavu kiakili, kimwili, kiuchumi, kiroho. Utasa ni matokeo ya kutofanya vizuri, kutofuata kanuni za Mungu, ni Laana.

Lakini kama utaamua kubadilika, Hakuna kizuizi, hakuna mchawi, hakuna hofu, hakuna mashaka. Badilika kuwaza kwako, mtazamo wako, kufikiri kwako.

Fahamu ufunguo ulio sahihi kwa ajili ya maisha yako. Ufunguo wa kutambua hali zako zote unapohitaji mafanikio

Neno la Mungu liko juu kila mahali. Kama ukijua siri hii , kila kisicho na faida kwako utakiamuru kiondoke. utamuru utasa uondoke. Utakuwa na matunda katika kila eneo la maisha yako.

mbinuusaili_1 Tambua Uwezo Wako Ili Kutimiza Kusudi

Ukijiunganisha na network nzuri lazima ufanikiwe.Utakuwa umejiweka kwenye kilima kinachozaa sana. Unaweza ukawa na mbegu sahihi , lakini tazama umepanda wapi? Ni mahali sahihi? ni wakati sahihi?

Mungu ndio chanzo cha kila kitu. Ili imani yako ikue, Amini na utapata zaidi ya uliyoyataka. Inawezekana kwa kila mtu kuzaa kazi nzuri, familia nzuri, maisha mazuri, nyumba nzuri, gari zuri. Pata urithi wa uzao wako, hata kama ni mshitakiwa bado una haki ya kupata  afya njema, furaha, amani , fadhili, upendo.

Ondoa Vizuizi.

Negative attitude. Mtazamo hasi unaanza na hisia hasi, mawazo hasi , fikira hasi. Na atimae kuwa na matendo hasi. Usiache kazi, biashara eti kwa sababu haijakuletea matunda kwa haraka. Kumbuka kuwa Mungu ni mwanasayansi mkubwa. hakuna aliye tasa kama ukizifuata kanuni zake.

Chochote ambacho utakipanda ndicho utakachokivuna. It is possible. badilisha mwonekano wako,  Usiwe mtu wa nia mbili. Lazima uwe na Imani na kutenda.

Achana na makundi mabaya. Watu gani unaoongozana nao, mazingira gani unayopenda kukaa kwa muda mrefu, Usidanganyike mazungumzo mabaya yanaharibu  na kubadili nia njema.

picajira-wafanyakazi Tambua Uwezo Wako Ili Kutimiza Kusudi
watu gani unaoongea nao

Tembea na wenye Hekima ili uwe mwenye Hekima. Simple. Timiza mashariti yaliopo.

Hofu , woga, mashaka kwa sababu ya umri wako, vinazuia mafanikio yako. Usiruhusu mawazo mabaya ndani yako, Yataathiri mafanikio yako.  Kuwa makini na maneno yako unayoongea kuhusu uchumi wako, mahusiano yako, hisia zako, mwili wako na matendo yako.

Ili uweze kuwa na mafanikio ni lazima uwe kiumbe kipya. Kuwa kiumbe Kipya Ni  kubadilika katika kuwaza kwako, kuhisi kwako, kufikiri kwako, mitazamo yako na matendo yako.

Mungu Akubariki.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

Previous Kaa Kwa Sababu Ya Upendo Sio Woga
Next Njia Ya Kuzia UTI ( Usiwe Na maumivu Wakati Wa Sex)

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.