winstonchurchill1-620x300 Tengeneza Tabia Za Mafanikio

Desturi ni, ”Tabia iliyojengwa kutokana na kurudia rudia  maneno unayotaka yafanyike  ndani yako. Kitu chochote ambacho utakifanya mara kwa mara kinakuwa ni desturi yako.

Wewe ndiye mtu ambaye unaijenga  desturi yako  kwa kujua unachokitaka. Wakati mwingine mtu anaweza kujenga desturi ambayo hakujua kama  ni mbaya. Kwa sababu baadae desturi hio  hujenga matendo na  kushawishi muundo wa tabia yako.

Hivyo ulivyo ni matokeo ya desturi yako.

Wapo watu ambao hawana furaha na desturi zao. kwa mfano utakuta mtu anasema uongo na ghafla anajichukia kwa kufanya hivyo. Kitu ambacho watu hawajagundua ni kwamba  hakuna kitu kinachotokea kwa siku moja. lazima walianza kusema uongo  neno moja na kurudia siku nyingine na kuendeleza  na kuwasababishiwa kuwa watu ambao sio waaminifu.

Kwa hio kama unahitaji kubadilisha desturi yako kumbuka kuwa sio kitu cha mara moja. ni matokeo ya matendo yanayojirudia rudia kila siku. kama utabadili hio desturi ya zamani na kutaka mpya , unahitaji kufanya mpangilio huo huo.

Live-Life Tengeneza Tabia Za Mafanikio

Vitu vibaya havitaweza kukutawala.  kwa hio mtu mwenye tabia za uongo  ni lazima kuamua  kuwa makini  katika kusema ukweli. ukiwa na bidii ya kufanya mabadiliko haitachukua muda mwingi sana.  Utaona  nafsi yako inaanza kuwa na muundo  wa tabia nyingine mpya.desturi mpya itajengwa.

Ukiwa unasema ukweli kila mara kwa muda wa mwezi mmoja tu utakuwa mkweli. na kama  utasema nitahudhuria masomo ya kupata ufahamu  kila mara , utajenga hilo ndani ya nafsi yako . na utakuwa mwenye njaa ya kutaka kujua ukweli upo wapi.

Kama utaanza kuamka mapema , ukarudia kama mara kadhaa, itakuwa ni tabia yako ya kuamka mapema. kama utaanza kufanya mazoezi, na ukarudia mara kadhaa , itakuwa ni tabia yako. kama utaanza meditation, na ukaamua kabisa  na ukarudia mara kadhaa, itakuwa ni desturi yako. kila tabia nzuri unayoitaka , ni lazima ufanyie kazi hio.

Nakutaka ujue kuwa hakuna lisilowezekana chini ya jua hili.  Anza kujenga tabia ambazo unazitaka na utaona mafanikio makubwa katika sehemu zote za maisha yako.

share. usisahau . Subscribe kulia kwako ni bure usiogope

unastahili kupata kitu bora kila siku.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here