Tiba Ya Ndoa Ni Muhimu Kwa Ustawi Mpya?


Amanda-and-Kingsley-Fit-Nigerian-Couple_BellaNaija-Pre-Wedding-Shoot_2016__Kingsley-PreWed-ag-13-of-30 Tiba Ya Ndoa Ni Muhimu Kwa Ustawi Mpya?

Kizazi hiki sasa hivi wanajali  sana tiba ya ndoa, au ushauri wa wanandoa, kwamba unaboresha  Afya, Furaha, Nguvu na utendaji bora.

Na siku hizi wengi  wamejua kumeditate ili kupunguza stress, kula kwa kubalance homoni zao na kuondokana na simu na laptop mahali pa kulala ili waweze kupata usingizi mzuri wa kutosha.

Lakini mahusiano yamesahauliwa katika hali ya ajabu. Hakuna anayejali umuhimu wa mahusiano. Kuna vitu vingi sana wanavyovijali.  Wamesahau jinsi gani mahusiano yanatakiwa kuonekana.

Mwanamke na mwanaume wote wanafikiri kuwa  mwenza  ndiye mtu pekee wa kufuatilia  kila box kwamba anatakiwa kuwa rafiki bora. Mtu ambaye atamkamilisha mwenzake, na mama aliye mkamilifu au baba bora kwa watoto  wao.  Na kama utampata mtu kama huyo unajiona umekamilika si ndio? Huenda, lakini sio kweli.

Ushauri unaotakiwa ni kuhusu kukua kwa mtu kibinafsi kwanza. kama sivyo huo ushauri mwingine sio mzuri.  Ushauri mzuri ni wa kufahamu kuwa na mawasiliano mazuri kitu ambacho kila mtu anaweza kufaidika nacho. Inasikitisha pale mtu anapoamua kufanyia kazi kwa bidii kwa ajili ya kutaka mtu ampende, amkamilishe ,amfurahishe, amjali katika maisha yake.

Mahusiano mazuri ni yale ambayo kila mtu anajua majukumu yake. anafahamu kuwa ni muhimu kwake kuijenga nafsi yake , Ili aweze kumsaidia mwingine katika kuijali nafsi yake. 

Ushauri wa Ndoa unakusaidia wewe na mwenza wako?

Kama unafikiria kuhusu  ushauri wa kufanyia mazoezi, fikiria kama tiba ya kimwili. Hakuna haja ya kwenda kwenye ushauri kama hakuna tatizo la msingi. lakini kama kuna malumbano ya hoja yasioisha kwenu ni muhimu kwenda kwa mshauri au mtoa tiba ya wanandoa, ili kulinda watoto , mahusiano  yenu yaweze kudumu.

Fikiria  hio tiba ni kama kwenda kujiongeza kidogo.

Kama unahisi kupungukiwa na kitu , ni vizuri ukachukua hatua mapema na kwenda kufanya  kama kucheck in.

Binadamu wanakua na kubadilika wakati kwa wakati,  kujali mahusiano inaweza kuangukia kwenye kazi, biashara, uzazi na kazi zingine  zenye umuhimu. Kulea mahusiano ili yawe na nguvu  na kuwa na utendaji mzuri katika ndoa  kwenye vipengele vyote inakuwa ngumu kidogo.

Lakini Uwe makini kwenda mbali zaidi.

Mara nyingi ushauri  hauna jibu kamili, Na katika kesi nyingi,  tiba hio inaweza kupeleka mahusiano pabaya zaidi. Kama utapata mshauri mzuri, aliye sahihi na mwenye matarajio mazuri , utafanikiwa. Vinginevyo utakuwa kwenye risk kubwa zaidi kuliko kuokoa mahusiano yako.

Ukweli unaosikitisha ni kwamba mahusiano mengi  matatizo yao huwa hayapati majibu.  Wanaweza  wasiweze kubadilisha tabia zao . Lakini kama utaambiwa  kuhusu  mawasiliano mazuri, muda wa kutosha wa kuwa pamoja, kudumisha upendo ndani na nje yao, huo ndio ushauri mzuri.

Matatizo mengi hujitokeza pale mwanandoa anapoenda kupata ushauri mahali ambapo sio sahihi. watu ambao wanatumia nafasi hio kwa kudanganya watu na kuwafundisha njia mbovu za kushughulikia mahusiano.

Natumaini washauri wawe ni watu wa  kweli waliobobea katika mambo hayo kwa muda mrefu . Watu wenye kutunza siri za watu. kuwaelekeza njia sahihi.

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Mungu Anapatikana Wapi? Umepoteza Mwelekeo?
Next Jeraha La Aibu Linaweza Kuwa Ndani Zaidi Na La Kudumu

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.