20160601182105-reading-successful-traits-book-coffee-studying-1 Tuko Hivi Kutokana Na Tunachokiongea

Ukitaka kujua ubora wa maisha yako , Chunguza  maongezi yako.

Kama mawazo yanaweza kubadilisha lugha, Lugha inaweza kubadilisha mawazo.

Wengi wetu tunafahamu kuwa tunapofikiria  positively, maneno yetu na maisha yetu yanaanza kulingana na mawazo hayo. Hata kama hatuamini kama tu wazuri, tuna nguvu au tu wazima na wenye nguvu nyingi.  Wachunguzi waligundua kuwa hali ya ujasiri hii  inaongeza  kujiamini kwamba ndivyo tulivyo.

Kinyume chake pia ni kweli. Tunapoongea Negatively kwa ajili yetu wenyewe na ulimwengu uliotuzunguka, Maneno hayo yanaathiri hali ya akili yetu na ustawi wetu. Unaposema umechoka , au umeboreka, unaumwa, huwezi kufanya kitu fulani, ni mbaya unapokuwa katika maongezi na watu,  Itakuwa hivyo hata kama ulikuwa huna maana ya kuhisi hivyo.  Kila neno unalosema linakurudia mwenyewe.

elberthubbard1 Tuko Hivi Kutokana Na Tunachokiongea

Mara nyingi maneno madogo madogo  ambayo huwezi hata kuyatambua wakati mwingine. Mfano, Mtu anakuja kwako ana shida ya pesa, Anasema Sijui utanisaidia, nina shida ya kiasi fulani. Moyoni mwake tayari kuna walakini. Sasa huyo mtu utamsaiduaje? Hana imani ya kupata halafu anaenda kuomba kitu.

Lakini vipi kuhusu kila siku, Maneno yaliopo pande zote ambayo yanaleta matatizo jinsi tunavyohisi na kufikiri?  Tutaondoaje yale ambayo hatuyatambui kwa upesi kuwa ni matatizo?

Siku zote wazo sio udhihirisho wa kufikiri. Ni katika hisia…Ni uelewa wa mtu na ni asili ya kawaida kwa mwanadamu

Mawazo ni kama upepo, kila wakati yanapita ndani ya  akili yako na ufahamu wako. Lakini kuna chujio liko , na wengi hatulitumii kwa kuwa hatujafahamu kuwa tunalo.  Kama wewe unapenda kusikiliza aina fulani ya nyimbo , mawazo yako yatakuwa yanakuja ya aina hio hio kwa kila unachokihisi , maongezi yako yatalenga kile unachosikiliza na kukiona kila mara.

Kila kitu unachokifanya ni wewe umechagua. Hakuna mtu wa kukuchagulia maisha yako. Kila kitu hapa Duniani kina kinyume chake. Vitu vyote vimeumbwa  viwili viwili, jaribu tu kuchunguza. Maneno mawili mawili .

Mungu aliumba maneno. Lakini mwanadamu alipewa hiari ya kuchagua . Maamuzi yako ndio maisha yako. Mungu alisema nimekupa leo Uzima na Mauti , lakini kakushauri uchague Uzima. Aliumba neno Tajiri na Maskini, Baraka na Laana.  Furaha na Huzuni.  na mengine mengi .

Kwa hio maisha yetu yanatokana na uchaguzi wetu . Ukichagua kusikiliza  nyimbo za huzuni , utakuwa mtu wa huzuni. Ukiamua kusikiliza nyimbo za furaha utakuwa mwenye furaha. Chochote kile utakachoamua tambua kuwa kina kinyume chake.

Wote tunaona maneno kwa utofauti mkubwa, Tunaona na kusikiliza  kulingana na lugha zetu, ufahamu wetu, nguvu  inaanza  ndani kuaminika  na kuwa ya  kuzoeleka,  nje ya ufahamu na hekima inayotakiwa .

Hatuwezi kuthibiti  maneno tunayotumia , lakini tunaweza  kuyaepuka  kwa kutosikiliza na kuyaongea.  Kuwa mlinzi wa mlango wa akili yako  mwenyewe kwa kila kinachoingia ndani yako, kila unachokitazama  na kuongea.

Ukipanda mahindi utavuna mahindi, ukipanda maharage utavuna maharage. hutaweza kuvuna kitu tofauti.muda msafi , una akili safi, lakini muda mchafu una akili chafu .ongea maneno yenye uzima, ya kukupatia nguvu, utajiri.Miliki maneno mazuri kila siku ongea maneno ya uzima.

Usisahau  Subscribe .

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here