TUMIA MUDA WAKO VIZURI:


Clock2 TUMIA MUDA WAKO VIZURI:

Nafasi ulionayo katika maisha ni nzuri, ukiwa darasani ulijifunza  vizuri matumizi ya muda. hata unaweza kusoma tena vitabu mbalimbali.ili utumie muda wako vizuri  chukua hatua mpya ya  mpangilio wako kwa  siku , na ipe kipaumbele. anza kujiuliza maswali, je  nahita kujua kitu gani , siwezi kufanya vitu vyote  ninavyohitaji kwa siku?

jibu ni rahisi tu , kila kitu ulichojifunza kuhusu matumizi ya muda ni kama ulipoteza muda tu kwa sababu havijakusaidia kitu.

kabla hujaanza  kutunza muda lazima ujue muda ni nini hasa.

kamusi yangu inasema muda ni  kipindi ambacho vitu hutokea, kama kuzaliwa kukua kuoa na kufa.

KUNA AINA MBILI ZA MUDA 

1.MUDA WA SAA

2 MUDA HALISI

Katika muda wa saa kuna  vipindi , kuna sekunde 60, kuna dakika 60 zina saa moja, kuna masaa 24 ya siku na kuna   siku 365  kwa mwaka.muda wote unapita sawa, mtu akifika miaka 40 ya umri wake, ndio hio si chini ya hapo.

Katika muda halisi  muda wote ni jamaa, jinsi muda unavyopita inategemea wewe unatumiaje unafanya nini , kwa sababu masaa mawili tu unapofanya kitu ni sawa na miaka 12 ,na mtoto mwenye umri wa miaka 12 ni sawa kama amekuwa kwa masaa hayo mawili.

Ni muda upi unakuelezea wewc duniani, je ni muda wa saa au muda halisi?  hatuishi kwa muda wa saa tunaishi kwa muda halisi.  kuna wakati ambao unakuwa na furaha, kuna wakati unapokuwa nsa huzuni, haya yote ni majira . kuna wakati wa kulia , kucheka , kuhuzunika ,kupanda, kuvuna,  wakati wa sherehe na wakati wa msiba. wakati nwa kuwa na kazi na wakati wakukosa kazi.

huu ndio muda halisi wa binadamu kujua kutumia muda huu kwa hekima ya kutosha ili aweze kuishi maisha mazuri na ya   utoshelevu,ina maana kwa kila hatua unayopitia hakikisha unaifurahia na kuutumia vizuri muda wako.

UNAWEZA KUTUMIA MUDA KWA NAMNA TATU:

KIFIKRA

scratching-head-pi_2895834d TUMIA MUDA WAKO VIZURI:

MAONGEZI

rethinking-workpla_2966953d TUMIA MUDA WAKO VIZURI:

 

VITENDO

man_2928722d TUMIA MUDA WAKO VIZURI:

 

Kunapotokea muungiliano katika kazi zako, inabidi kuwa makini na muda wako , kwa sababu kuna vitu ambavyo husababisha kupoteza muda ,fikra maongezi na vitendo vikuongoze katika matukio yeyote.

ZIFUATAZO NI MBINU ZA KUKUSAIDIA  KUTUMIA MUDA  VIZURI.

1.Uwe na kitabu kidogo  cha kurekodia  mawazo yako ,fikra zako ,maongezi yako na vitendo vyako vya wiki. hii itakusaidia kuelewa endapo umefanikisha vingapi na vingapi hufanikisha.pia utajua muda ambao umepoteza na kwa nini.

20150330142247-7-million-dollar-habits-super-successful-to-do-list TUMIA MUDA WAKO VIZURI:

2.Mazungumzo au kazi yoyote muhimu lazima upange muda. uwe na kitabu cha appointment na uwekee kipaumbele fikra zako na mazungumzo na vitendo , kutakuwa na adabu katika uda wako.

3.Jiwekee muda kwa ajili ya kufikiria , kutenda na maongezi  yako nangalau asilimia 50 ya mambo yako yote ambayo yanakupa mafanikio.

4. kuna muda ambao huwa unaingilia kati vitu vingine, inabidi utenge muda huo , wa ofisini , wa  binafsi  ili usiharibu mpangilio wako.

5. uwe na dakika kama 30 kila siku kwa ajili ya kupangilia siku yako , usianze siku bila ya kupanga muda ni muhimu sana kwa ajili ya mafanikio yako.

6.Unapokuwa na kazi za muhimu, hutaki usumbufu , weka mlangoni   noti inayosema usinisumbue. mpaka hapo utakapomaliza.

7. kama wewe  hutumii FB , Instagram kwa ajiliya kazi zako basi funga hizo habari wakati ukiwa na kazi zako.

8.kumbuka kuwa huwezi kupata kila kitu asilimia 100,   kutakuwa na asilimia 20 za  kupoteza  na labda asilimia 80 za faida kwako, kubali hilo.

 

 

Previous MASWALI 60 YA KUMUULIZA MPENZI WAKO , YANAWEZA KUWA YA KUCHEKESHA& KUFURAHISHA:
Next NJIA 6 ZA KUKUSAIDIA MWAKA 2016 UWE WA KUSHANGAZA:

1 Comment

  1. […] sana, ila  itakuchukulia muda mwingi badala ya kufikiri   kufanya vitu vya maendeleo. Tumia muda wako vizuri.  hakuna tatizo kutumia muda kwenye michezo ya tv, iwapo utaweka sawa muda wako wa kazi za […]

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.