UELEWA NDANI YA MAISHA YAKO


understanding-life-4-post UELEWA NDANI YA MAISHA YAKO

Ufahamu haufundishwi; hakuna mtu anaweza kufundisha ufahamu, unatakiwa uwepo kama mwanga ndani yako mwenyewe.

Unatakiwa utafute ndani yako. Kwa sababu tayari upo ndani yako tangu kuzaliwa kwako.  Kama ukichimba ndani utaupata.Unachotakiwa kufanya ni kujifunza jinsi ya kuutafuta  kati yako mwenyewe. Sio kwenye mistari, lakini ni katika maisha yako mwenyewe.

Wakati mwingine tunaukataa ufahamu , halafu unakaa pembeni na kutuangali jinsi tunavyohangaika. Saa nyingine unatoa sauti ukiwa karibu na malango ya kutokea na kuingia,  na sauti ya ufahamu ni kwa wanadamu, ufahamu unatoa sauti ili tupate werevu, moyo wa kufahamu maadili. Kwa sababu yote humwelekea mwenye ufahamu na mwenye maarifa.

Ukipata hicho, hutakuwa na kiburi, hutasema uongo, hutaweza kushiriki uovu na wala hutapanda mbegu za fitina kwa wenzako.Na wala hutaweza kuwa shahidi wa uongo.na mahusiano yako yatakuwa mazuri na kila mtu 

Kwa sababu ndani yako kutakuwa na mwanga, na sheria itakuwa nuru kwako

HAKUNA KUWAZA

1-3 UELEWA NDANI YA MAISHA YAKO

Kuna tofauti kubwa katika kutofikiria vizuri au kutofikiria vibaya. Hali ya kutofikiria, ni kutazama tu, unakuwa  kwenye ufahamu,lakini hufikirii. Lakini kama yataingia mawazo…Yataingia, kwa sababu mawazo hayo sio yako; huwa yanazunguka hewani. Yote yapo hewani. Ni kama upepo, kuna fikira nyingi zimekuzunguka.  Yanaingia na kutoka, yatakaa tu kama ukiyakubali na kuyatambua. Na ukiwa na ufahamu zaidi fikra hizi hazikai kwako. Kwa sababu ufahamu ni mkubwa kuliko wazo.

Ufahamu ni kama moto kwenye wazo. Ni kama kuwasha taa ndani ya nyumba  ambapo hakutakuwa na giza. Lakini ukizima taa giza litajaa ndani kwa  sekunde. Linakuwepo hapo karibu .kama ukiwasha taa giza halitaingia.

Mawazo ni kama giza,  huingia tu ndani mwako kama hakuna taa. Ufahamu ni moto. Ukiwa makini, mawazo kido kidogo hayataweza kuingia.

Kama ukiwa kamili ndani ya ufahamu wako hakuna mawazo yatakayoingia. Unakuwa mlinzi wewe mwenyewe kwenye mlango wa akili yako. Hakuna kitakachojiingiza kwako.Kumbuka  hujajifungia, uko wazi kabisa; lakini nguvu yako ya ufahamu ndio iko wazi . Na wakati mawazo yanapokuja utayaona na kuyashughulikia  mapema. Hakuna cha kukuzuru. Hii ndio maana ya kufunguka.

Previous USALITI NI UPI, NA UPI SIO USALITI
Next UPENDO WA KWELI NI UPI NA AMBAO SIO WA KWELI NI UPI?

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.