Ufanye Mwaka 2018 Uwe Mwaka Wa Tofauti Kwako Kwa …


Beauty Young Woman Blowing Hearts from her Hands. St. Valentines Day Concept. Beautiful Girl in Love. Valentine art design. Valentines Gift
bigstock-beauty-young-woman-blowing-hea-56827535-1024x729 Ufanye Mwaka 2018 Uwe Mwaka Wa  Tofauti Kwako Kwa ...
Upendo wa kweli unaanzia ndani yako.

Ufanye mwaka ujao kuwa mwaka wa tofauti kubwa kwako. umekuwa ukienda mbio kupita kiasi, Geuka , rudisha Gari yako na uanze kutumia muda wako vizuri kuanzia sasa hivi.

Acha uwe mwaka wa kupata ufahamu wa kutosha, Kulisha akili yako , Kulisha roho yako ili ujifahamu jinsi ulivyo wa muhimu. Haitaweza kuja kwa urahisi au kwa haraka, bali itachukua process ndefu kidogo. Kumbuka kinachokuja kwa urahisi hakidumu, Kinachodumu hakiji kwa urahisi.

Ufanye mwaka 2018 uwe ni mwaka wako wa kujikubali, kujipenda, kujijali mwenyewe kwanza kabla ya wengine. Usitake kutaka kitu ambacho huna ndani yako. Ukijaa Upendo ndani yako , utapata upendo kutoka kwa wengine pia. Kwa nini? kwa sababu utakuwa unatafuta mtu wa kumpenda sio kutafuta mtu wa kukupenda.

Kubali ukweli kwamba umekosea. Kubali ukweli kwamba hauko sahihi. Lakini usiache vitu vikuangushe chini. Kubali kushindwa kwako, kukosea kwako kulikotokea miaka yote. Imba zaidi. Cheza zaidi. Fanya kitu chochote ambacho kinaufanya moyo wako ufurahi. Jifanyie party wewe mwenyewe, kwa muda wako mwenyewe.

tumblr_mduasikc6f1qfmyfyo1_500 Ufanye Mwaka 2018 Uwe Mwaka Wa  Tofauti Kwako Kwa ...

Unaweza kuita marafiki zako ukipenda.Achana na wale wabaya, Fanya iwe ni mwaka wa kusafisha  moyo wako kwa watu wote waliokuangusha kwa kitu chochote.Acha iwe ni mwaka ambao unausikia vizuri na kuona watu wanaokuinua juu.

Vaa vizuri . Kula vizuri bila ya kujali kuongeza uzito kwa wakati huu. Furahia maisha yako .

Ufanye mwaka ujao kuwa mwaka wa tofauti kwako. Kubali kwamba ulikuwa sio mtu mzuri. hukuweza kutunza siri . maisha hayakutakiwa kuwa  na chuki. Kwa hio usijichukie. Tambua kwamba wewe ni wa thamani , ni wa kipekee. huwezi kufanana na mtu mwingine. Usizungumzie tena madhaifu yako.

Ni mwaka mpya , Wewe ni mpya. Mwaka ambao utakumbatia zaidi. Utakiss zaidi. utakula zaidi. Utajishughulikia vizuri zaidi. Utatabasamu zaidi.

Ufanye Mwaka 2018 uwe mwaka Wa kujitanguliza wewe zaidi, lakini ukiwa na ufahamu kabisa kuwa unatakiwa kuwafanyia watu vizuri kama wewe unavyotaka ufanyiwe.

Mwaka 2018 ni mwaka wa  kutambua nguvu zako. mwaka wa kutambua jinsi gani unastahili . Mwaka ambao hutajificha  mbali na kioo. Mwaka ambao hutajichukia tena, hutaweza kujikataa tena.

67068-Love-God.-Love-People.-Love-Yourself Ufanye Mwaka 2018 Uwe Mwaka Wa  Tofauti Kwako Kwa ...

Ishi mwaka huu kwa ajili yako. Ufanye mwaka huu kuwa ni mwaka wa kuupenda. Fanya ukipendacho. Penda unachokifanya. Mpende Mungu, Ipende nafsi yako. Mpende jirani yako. Uwe mtu wa Imani. Tumia masaa yako 24 Vizuri.

Mwaka 2018 , jifunze matumizi ya MUDA . matumizi ya muda ni Kufikiria. Kuandika mawazo yako. Kutafuta Information za uhakika kila siku. Kujifunza  kila siku.  Kumshukuru Mungu , Kumkumbuka Mungu, na Kumsifu Mungu Kila baada ya saa kamili. 

Mshirikishe na mwingine. fanya kazi ya Mungu kwa kumwambia mwingine kuhusu makala hii. Mungu akubariki unapofanya hivyo.

Subscribe kupata makala mpya.

 

Previous Kiini Cha Mbinu Ya Furaha Hakuna Mtu Amewahi Kukufundisha
Next Kila Mahusiano Yaliofanikiwa Ni Kutokana Na Wawili Kuwa Na Lengo Moja

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.