Ukitaka Kuendelea Kulenga Kitu Ukitakacho


Inspirational-WAHM-Work-at-Home-Mom-500x333 Ukitaka Kuendelea Kulenga Kitu Ukitakacho

Usijikatie tiketi ya kuacha kwa ajili  yako wewe mwenyewe.

Huenda uliingia katika njia ya waovu na hukujua kama uko humo. Ukazidi kutembea katika njia zao mbaya. umefika katikati mambo yamekuwa mazito huwezi hata kuyakabili.  Usikate tamaa jibu lipo. Kaa fikiria upya mahali ulipokuwa na ulipo sasa , Kisha  anza upya.

Kila mtu Duniani hupotea mara kadhaa na kujipata tena. Usiogope mtu wa Mungu. Utajipata tena. Huenda umekuwa mjinga kwa sababu ya kutokutafuta taarifa sahihi katika maisha yako. Huenda tatizo lako ni Ugonjwa unakusumbua na hujui dawa yake, Huenda umepotelea katika ulevi , huenda umekuwa malaya , umekuwa mlevi, mwizi, mdanganyifu,  umeshindwa kuacha sigara, au ulevi ulionao. Hio yote ni kukosa maarifa usijute sana.  Bado upo kwenye Ujinga , Hata mimi nilikuwepo kwenye ujinga huo mojawapo lakini nilipogundua kuwa nimepotea nilikanyaga break ya gari langu nikasimama nikarudi nyuma.

1_XVS7inx27yVmsgGv4KzhOA-1024x757 Ukitaka Kuendelea Kulenga Kitu Ukitakacho

Sikutaka kula tena mkate wa uovu. wala sikutaka tena kunywa divai kwa jeuri ya kijinga,  nilianza kutafuta njia sahihi ya maisha yangu . Nilianza kutafuta Nuru ya kweli.  Nuru inayong’aa mchana na usiku. Nikakutana na Yesu.  nikaanza kuona  Nuru.

Nuru hio ni Hekima. ndani ya Hekima kuna Maarifa, Ufahamu, Uweza, Na roho ya Ushauri. Roho ya kumcha bwana.

Niliposikiliza Kauli ya Mungu niliona Uhai ndani yangu. Nikaona afya ya mwili wangu.

Ndugu linda sana moyo wako kuliko yote unayoyalinda. maana ndiko zitokako chemchemi za uzima wako.  Kuulinda moyo wako ni mojawapo ya kujipenda mwenyewe.  Kumpenda jirani yako na Kumpenda Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote na kwa Muda wako uliopewa na Mungu.

Jiepushe na kinywa cha ukaidi, usiongee maneno machafu, usifikiri mabaya , jitahidi kufikiri mambo mazuri kila mara, ongea maneno ya kukuponya, kuponya mwingine. Maneno ya kukutia nguvu na kumtia nguvu mwingine. Mfanyie mtu mwingine kitu ambacho unataka ufanyiwe.

Kuwa mwangalifu na mahali unapoenda kila siku. Tunza Muda wako ukupatie utajiri badala ya hasara na uje kudaiwa na Mungu.  Usienda sehemu ambayo sio sahihi, kwa wakati ambao sio sahihi na  kufanya kitu ambacho sio sahihi ni kosa.Kupoteza muda bila faida ni dhambi.

Muda wa ibada nenda ibadani, Muda wa kazi chapa kazi, Muda wa kujifunza jifunze. Muda wa familia ni wa familia na muda wa kupumzika ni wa kupumzika.  Muda wa kufikiri ni wa kufikiri ili kupata mawazo mapya katika kazi yako, familia yako, jamii yako.

Usipoteze muda wakati zipo kazi nyingi sana za kufanya . Kama hujui kazi za kufanya ambazo huwezi hata kutafuta kwa jasho njoo kwangu nitakuelekeza kazi za kufanya ili upate malipo makubwa kuliko kazi unayofanya sasa.  Huenda kazi yako ina changamoto nyingi njoo nikupe njia ya kuondoa changamoto zako na utafanya kazi kwa faida kubwa.

Kuna mambo mengi nimeandika kwenye makala zangu lakini najua kabisa kuwa hujaelewa kitu . nitafute nikuelekeze vizuri kitu cha kufanya uondoke mahali ulipo . Akili uliyonayo sasa haiwezi kukutoa  hapo ulipo , unahitaji  kuvutwa  ili utoke kwenye hilo tope.  utoke kwenye giza hilo  ulipo sasa. Mimi  sijui unateswa na nini , lakini nina uhakika akili yako ndio inakutesa.  Utatokaje hapo ulipo, njoo kwangu nitakusaidia.

Heshima yako itatokana na  matendo , maneno na mawazo yako. Wakati Matendo yako yanatokana na  mawazo , picha iliopo ndani yako, na mitazamo yako.

Think God

Andika unayosikia na kuona

Hamasika na utafute taarifa sahihi.

Nikutakie Jumapili njema . Subscribe ili usikose makala nzuri .

Previous Nikae Au Niondoke?
Next Kwa Nini Ni Ngumu Kupata Upendo Ndani Yako (kujipenda)

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.