UKITAKA KUJENGA UAMINIFU KWA HARAKA, KUNA MAMBO 5 YA KUFANYA


beautiful-smile-1024x681 UKITAKA KUJENGA UAMINIFU KWA HARAKA, KUNA MAMBO 5 YA KUFANYA

Nilikuwa nauza bidhaa yangu  na ni lazima kuongea na mteja wangu ,  na mteja huyu aliniangalia machoni na kusema , kuna wachache sana wamebaki  , halafu aliondoka  na mume wake.

Nilifikiria moyoni na kusema imekuaje huyu mteja aongee jambo hili kwa muuzaji. Kumbukumbu zilikuja kwa kipindi kirefu ambacho nimekuwa nikijenga  uaminifu kwa watu, kila ninapokutana nao.  Ikaja kwenye akili yangu. Imekuwa ni kipindi kirefu nafanya biashara hii kwenye maisha yangu.

Kutokana na hilo napenda kukuletea  mambo matano ambayo nilijifunza kwa wanasaikolojia  ambayo yanaweza kukujengea uaminifu kwa haraka.

1.Onyesha Tabasamu  lililo sahihi.

Wachunguzi wanasema tabasamu la kweli , linawasogeza watu kwa karibu  na linajenga misuli ya  macho , ni dalili ya  kuaminika

Sababu ya kusema kwamba uwe na tabasamu  sahihi,  ni kwa sababu linatakiwa litoke ndani ya moyo wako, sio la uongo, liwe na hisia za kweli.Na kila siku utakuwa unaongeza hilo tabasamu usoni mwako.

Kitu cha muhimu ni kuelewa hisia zako  kabla ya tukio na baada ya tukio. Unatakiwa kuwa positive kila wakati , iwe umepata ulichotaka au hukupata ulichotaka. Malengo yako yawe pale pale kuwa umekutana na zaidi ya wateja uliotarajia.Utaendelea kuonyesha  tabasamu la kweli na  watu wataanza kukuamini .

2.Waonyeshe watu wengine  namna unavyoweza kuwasiliana

Kuwaonyesha watu njia ya kujenga uaminifu ni kitu  ambacho kinahitaji  uwezo  wa kutosha. Hapa ni kulinganisha matendo yako na matendo ya mtu mwingine. Kwa mfano , kama mtu anaongea taratibu na kwa upole, na wewe unatakiwa ufanye hivyo.  Kama utaenda tofauti hamtaelewana na mteja huyo , kama anaongea kwa utani utani na wewe ingia hapo kwa utani mtaelewana.  Na hapo ndipo pa kujenga uaminifu.

Mazungumzo sio ya mdomo tu , unaweza kuongea na watu kwa kutumia lugha nyingine ya mwili, mkono , watu ndio walivyo . kila aina ya watu tofauti . kwa sababu mawasiliano ni mazuri kama yakifanana, watu watajua na  wewe uko hivyo kumbe unajitahidi kucheza mchezo huo.

Watu wanao kuwa na tabia mbaya mara nyingi huwa hawawezi kuona uzuri uliopo kwa mtu mwingine.  Hawawezi  kulingana .

Kumbuka mwonekano sahihi  sio wa kuigiza  kwa ajili ya kumvutia mtu fulani  kwenye mazungumzo . ni ile kumfanya mtu ajisikie vizuri  mnapokuwa mnaongea.

3.Msikilize mtu aliye mbele yako.

Kumsikiliza mtu haina maana kuwa unajidai kuwa karibu yake  kwa kumwangalia usoni.  Ina maana ya kumwangalia na kumsikiliza kwa umakini, hapo ni kumkaribisha aweze kuwa na ujasiri wa kuongea na wewe.  Na kuonyesha kuwa unamjali.

Watu wanapogundua kuwa unawaelewa jinsi  walivyo , na hali zao zilivyo, watakuamini .  na kujiona wako salama.

4.Uwe tayari kuonekana kwenye mazingira magumu.

Katika maoni yangu , naona watu wanaokabiliana na hali zote ngumu , huwa na uwezo zaidi wa kusaidia wengine,  kama utakuwa wazi na mkweli  kwa jinsi unavyoongea  na watu  utaonyesha nguvu  na pia utaonyesha hali halisi ya kukabiliana na hali ngumu.  Haina maana kuwa  huna madhaifu.   Ina maana ya kuwa mkweli  na hisia zako .

5.Onyesha kuwa  unafanya kile unachosema.

Watu wengi wanatafuta  waaminike mapema kabla ya kujenga kwanza huo uaminifu .  Huwezi kutabasamu tu ilimradi kwa ajili ya kujenga uaminifu kwa watu , Fanya kitu tofauti kwanza , kwa kila unachosema na kila unapotabasamu  umekifanya.

Kama utaonyesha unafanya kile unachofanya  tangu mwanzo , hata unapokutana na watu watakuwa na imani kubwa na wewe kulingana na wanavyokuangalia .

Kitu unachohitaji kufanya ni  kuendeleza kile ambacho unakifanya  na kile unachosema  na watu watakuwa tayari kukuamini  katika eneo hilo.

Utajenga uaminifu sahihi kama tu  utakuwa mkweli  kuhusu   kitu unachokifanya  na utaungana nao.

Kama umependa makala hii washirikishe na wengine  wajifunze.

Previous NIAMINI , MIAKA 30 UTAKUWA UNAELEWA VIZURI ZAIDI KULIKO UKIWA NA MIAKA 20
Next KITU KIMOJA KIZURI CHA KUFANYA KAMA WEWE NI MJAMZITO

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.