swimming-safety-1024x678 UKITAKA WATOTO WAKO WAWE NA MAFANIKIO BAADAE, ONGEA NAO KWA NJIA HII.
Tunapokuwa na watoto, wengi wetu tunapata taarifa nyingi tuwezavyo kutoka kwenye vitabu, ushauri wa marafiki au ufahamu wowote kutoka kwenye internet.

wengi wao huenda na hizo na kufanya kilicho sahihi. mwisho wake, kila mtu anahitaji kumkuza mtoto wake ili aje kuwa na mafanikio iwezekanavyo.

Kuna njia nyingi za kusaidia , kufundisha na kutia moyo watoto wetu lakini inapokuja kwa njia yetu ya kuongea, tunatengeneza a growth mindset au a fixed mindset?

Muda mwingi tofauti iliopo kati ya kuamini growth mindset au fixed mindset kwa watoto ambayo ni ngumu kuelewa. yote yanaweza yakawa yanahusika katika hilo , lakini sehemu yenye thamani ni mpango wa kujifunza wakati wengine wanatengenezewa mafunzo yaliopita, matokeo ya mwisho , wanalazimishwa kufanya mambo wasioyapenda kuyafanya. eti kwa sababu mzazi amefanya hicho na kuona kina mafanikio kwake.

Growth mindset inatengeneza hamu , nia ya kujifunza zaidi kuliko njaa ya kuhakikisha, na kwa fixed mindset inafanya mambo ya kufanana. Ni muhimu kwa watoto kuwajengea mawazo mazuri na kuangalia anaelekea kufanya kitu gani, kipi anachopenda, ambacho hakitamwangusha katika maisha yake, katika maneno mengine kumlazimisha mtoto kufanya kitu asichoelewa na wala hakipendi , unamtengenezea kushindwa maisha.

Mifano ya kawaida ya kutengeneza na kukuza mawazo kwa maneno.

Kuyakuza mawazo ni jambo zuri kwa uwezo wa mtoto kuliko akili alionao ya darasani . na hapa kuna tofauti za kawaida zinazoonyesha kila wazo.

Fixed mindset: ‘‘ umepata jibu sahihi, umefanya vizuri, una akili sana.”

Growth mindset: ‘‘ Umepata jibu sahihi, umefanya vizuri, umejitahidi sana kuelewa hicho na umefanya.

Fixed Mindset: ”Umepanga haraka hivyo vimchezo vya puzzle! uko vizuri kwa hilo- umefanya vizuri!” na hapo hata hajamaliza kupanga ipasavyo.

Growth mindset: ” Umefanya vizuri! jinsi ulivyojaribu hii changamoto ya puzzle umewezaje? nafikiri utaweza kufanya.!” na hapo labda mtoto hajafanya vizuri kama itakiwavyo.

Kwa nini Kukuza Mawazo Ni Mumhimu Sana.

Growth mindset ni msingi wa encouragement, confidence, ultimately, success. mtoto anapojaribu kufanya kitu kwa mara ya kwanza , mawazo hayawezi kuchoka kwa jinsi ambavyo wanaperform vizuri kazi zao na jinsi gani wako smart. ni muhimu sana kwamba wanaelewa kwamba sio vyote au hakuna kitu- kuna nafasi kubwa ya kujaribu tena na tena.

Hata kama ukienda shuleni , kuna watoto waliolazimishwa kusoma masomo ambayo hawayawezi na wala hawafahamu chochote kuhusu  hilo somo, lakini wale ambao wanapenda somo hilo na ni la muhimu kwao ndio wale ambao ni growth mindset. wanaona urahisi na wala hawatumii nguvu ya kusoma, kwa sababu kipo kichwani mwao.

Yote hio ni kwa sababu ya kutengenezewa kiasi cha uthamini na kufanywa kuwa sio waoga wa kushindwa na kuwa na ujasiri wanapo chukua kazi. na hapo wanakuwa wanaelewa kuwa kuna kujifunza vitu vipya at all costs.

Ni wakati Gani Unatakiwa Uanze Kukuza Mawazo Ya Mtoto?

Wachunguzi wanaonyesha kwamba , hujachelewa na wala hujawahi kuanza kukazania ukuaji wa mawazo kwa mtoto. watoto wengi kawaida hukua na mwazo mazuri , lakini sisi wazazi tunawajaza mawazo tofauti na walionayo. Kama mzazi, tunapenda sana kuwatukuza watoto lakini kuna wakati hatuna ufahamu kuwa jinsi gani watoto wanachukizwa na mashinikizo yetu.

Muda mzuri wa kuanza kumsadia mtoto kukuza kipaji chake ni wakati anapoanza kuelewa lugha. lakini hii haina maana kwanza hakuna tumaini kwa wale ambao wamekwisha kukua- unaweza kuanza kutambulisha na kumwelewesha kitu ambacho anahitaji kukifanya afanye sasa.

Wengi wa watoto wana muunganiko wa mawazo yote , ya growth and fixed mindset kuhusu kiasi vitu tofauti inategemea na uzoefu. lakini kama mzazi unaweza kusaidia kumuhimiza awe na hio growth mindset ili kupata mafanikio mazuri yenye furaha maishani mwake.

=Kuwafundisha watoto jinsi ya kujidhibiti

=Tabia 4 ambazo kila mtoto anahitaji akue akiwa na na furaha.

=Kwa nini nafikiri wanaume wote wanahitaji  therapy.

“I want to know why I lose control on my appetite under certain situations, so I can learn ways to deal with it.”

research-update-stock UKITAKA WATOTO WAKO WAWE NA MAFANIKIO BAADAE, ONGEA NAO KWA NJIA HII.

Umeipenda hii makala? shirikisha na wengine wajifunze

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here