Umesahau Kununua Zawadi Kwa Ajili Ya Mwenza Wako?


black-couple-christmas1-600x315 Umesahau Kununua Zawadi  Kwa Ajili Ya Mwenza Wako?

Hapa Kuna perfect solution.

Najua umesahau. Inatokea kwa watu wengi.  Sikukuu na matukio mengi yametokea, nani alikuwa na muda,  Je na mwenza wako?  Mmmm, huenda sio kwa ajili ya kutaka msamaha?

Hapa utapata ukombozi wako. Ok nikuulize swali, kama ungekuwa bilionea, ungeweza kutumia  milioni kadhaa kwa ajili ya  zawadi ya sikukuu, fikiria hilo kwa dakika mbili au tatu.

9d5371_59a180312684497db372003e18893202-mv2-696x522 Umesahau Kununua Zawadi  Kwa Ajili Ya Mwenza Wako?

Kuna mtu nilimuuliza swali hili , akasema Ndio!! kwa sababu nampenda sana mwenza wangu. Naweza kumpa kila kitu ninachokimiliki. Basi niliendelea kushangaa na kumwambia kuwa unadanganya?  Ingekuwa ni risasi kwa mke hio.

Haya, inakuaje kwa zawadi iliyochelewa hapa?

Naendelea.  Kitu kikubwa cha kufanya hapa ni kulist  vitu vyote ambavyo  mara nyingi  mnakuwa na tofauti   nazo, wewe na mwenza wako. Hii huchukua muda kidogo,  Lakini  ni kitu kinachostahili , kina nguvu ya kurekebisha tofauti ambazo mmekuwa  nazo, Hasa  kwenye stress za ndoa, Mioyo yenu, roho zenu. Akili zenu.

Kwa mfano ; Mume ana familia kubwa kuliko mwanamke. Na wote wanataka kuwepo nyumbani kwenu siku ya sikukuu, Familia ya mwanamke wao sikukuu ikiisha wanaondoka, lakini ya mwanaume  wapo tu hapo. Huenda mmekuwa na utata huo miaka mingi. Kitu hiki kinamfanya mwanaume afanye kazi kupita kiasi juani. Amechoka na anahitaji kupata muda wa kupumzika mahali. Mwanamke ana watoto pia anafanya kazi ya part-time . Lakini mwanaume ndiye mwenye kuhudumia kila kitu.  Wakati mwingine mwanaume huamua kupitia sehemu ili achaji betri  yake kabla ya kwenda nyumbani.  Hiki kitu kinaleta ugomvi mkubwa kwa mke wake,  hakijakaa vizuri.

Wengi hapa mnajifananisha na hii familia , Kila upande kunagusa mtu fulani.  Tunafanya hivyo na hakuna soluhisho  ambalo mmefanya.

Kwa kipindi hiki mkumbushe mwenza wako ili muweze kuanza upya, Na kufahamu kuwa kitu hicho kikikaa vizuri , kila mmoja ataweza kufanya kai vizuri  na kupata mafanikio makubwa . Kumbuka kuwa Panapokuwa na Upendo na maelewano , Amani. Mahali hapo kunakuwepo utele wa kitofauti na kuwa matajiri kwa njia nyingi. mtakuwa watu wenye afya kiroho, kimwili na kiakili.

Onyesha Upendo kwa mwenza wako. Onyesha kumthamini, kumjali, mpe muda wa kutosha, Fanya tofauti na ulivyozoea. Hii inazidi pesa nyingi.

Let’s-Gift-Love-This-Christmas Umesahau Kununua Zawadi  Kwa Ajili Ya Mwenza Wako?

Ni kubadili mindset tu. Unafanya hiki kitu kama zawadi.  Ni vitu ambavyo havihitaji kurudishiwa kitu ,  Vitu visivyotarajiwa, ni zawadi iliyo huru; ni ya furaha. Itambue zawadi hii inayoambatana na upendo wa kweli sio vitu.

Ukipeleka zawadi kwa mwenza wako , Halafu  wakati huo huo ana machungu moyoni mwake , zawadi hio haina baraka. itapokelewa lakini haiponyi tatizo lililopo ndani yenu.

Ok! Vipi kuhusu ndoa yako?  Utakubaliana na mimi kwamba , umepeleka zawadi  kwa kuamini kwamba unapunguza machungu uliyomfanyia mwenza wako, lakini  watu wenye ufahamu hawaendi hivyo. Pata uelewa huu leo kwamba, jirekebishe, geuka, kuwa mpya, Kiroho, kiakili na kimwili.

Kama hutaweza kutoa zawadi ya mamilioni , hii ndio zawadi ya kumpa mwenza wako wakati huu wa mapumziko. Mwenza wako atasahau taabu zote alizopata huko nyuma. wote mtakuwa win-win.

Well. Nyote muwe na Sikukuu njema ya Christmas na mwaka Mpya.

Toa maoni yako.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

 

Previous Sitawisha Sifa Zinazompendeza Mungu
Next Vitu 18 Vya Kuacha Kabla Ya 2018

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.