green-juices-e1484091410503 UMUHIMU NA FAIDA ZA JUICE ZA MBOGA NA MATUNDA

Mchanganyiko wa mboga na matunda  kwa ajili ya juice, ni lishe yenye afya nzuri,  Juice ya matunda inasafisha mfumo mzima wa mwili wa mwanadamu, wakati juice ya mboga inajenga mwili.

Kwa uzoefu wangu binafsi pamoja na wataalamu wengine wanaoshauri mambo ya afya,watu wengi wamegundua  kuwa fresh juice  ya matunda na mboga ina afya na imekusanya vitamini nyingi na madini mbalimbali yanayohitajika mwilini.

Kwa kuongezea hapo, inaondoa na kusafisha sumu zote mwilini. Kutokana na mtindo wa maisha tulionao siku hizi, milo yetu  inaharibu afya na jinsi tunavyojisikia.Kutumia natural fresh juice ni moja ya njia bora ya kuendeleza  na kutunza afya yako na kuwa na umbo zuri.

Umuhimu wa Fresh  na Natural juice

1-160121155916 UMUHIMU NA FAIDA ZA JUICE ZA MBOGA NA MATUNDA

Napenda kutumia juice katikati ya kila mlo, mchana na jioni, kwa sababu  inanifanya nijisikie vizuri na kuniwezesha nisile vyakula vingine  ambavyo sio vya afya. Sipendi kununua juice zingine kwa sababu zimeongezwa sukari, ladha na rangi ya chakula. ni vizuri kutumia juice yako mwenyewe, ambayo unatengeneza wakati huo huo .

Sio tu ni nzuri , bali unaweza kuongeza mboga mboga  kama matango, karoti, nyanya,  na zingine. Pia juice hio itakuwa haina sukari wala kuongeza ladha  na rangi.

Miili yetu inahitaji fresh juice ya matunda na mboga kwa sababu , vitu hivi vina vitamini na madini., kwa hio kutumia juice hii miili yetu itanyonya  nutrients zilizomo humo ndani ya juice.

Kwa Nini Ni Vizuri Kuchanganya Juice Ya  Matunda Na Mboga badala ya kula kila kimoja tofauti?

Kuchanganya pamoja matunda na mboga inasaidia kuwa na mkusanyiko wa nutrients za kutosha kwa wakati mmoja,  kwa sababu hutaweza kupata kiasi hiki kila mara unapotumia kwa kula kimoja kimoja. utakuwa mwenye afya  nzuri unapotumia hivi vitu kwa pamoja.

Kuchuja Juice Au kutochuja Juice?

Baadhi ya watu hupenda kuchuja juice na kuondoa kamba kamba zilizopo kwenye juice, lakini wataalamu wanasema  sio vizuri kuchuja, kwa sababu  hizo nyuzi nyuzi ni za muhimu  kwenye mwili, zinasaidia kupunguza uzito, kazi ya tumbo,  na kusaidia kupata haja kubwa bila tatizo. kwa  hio usichuje.

Hapa kuna mbinu za muhimu  za kutunza akilini mwako unapotengeneza juice.

1.Epuka kuweka sukari, ili kuifanya juice yako kuwa natural na yenye afya.

2.Hakikisha unachanganya   matunda halisi na mboga  pamoja  na kufahamu kiasi cha kuchanganya  ili usiharibu umuhimu wa virutubisho  unavyohitaji .

3.Mchanganyiko wako usiwe wa matunda makavu, uwe wa matunda na mboga fresh. kama nilivyoainisha , matango, apple, nyanya,  karoti, zabibu, n.k

4.Hakikisha umesafisha vizuri matunda na mboga kabla hujachanganya kwa ajili ya kusaga juice.

Unaweza kutumia juice hii kwa ajili ya kupunguza uzito, kutoa sumu mwilini, kwa ajili ya nguvu na zaidi

Mimi hupenda kuongeza tangawizi kwenye mchanganyiko wangu. unaweza kuongeza  kiungo kingine ambacho unaona kuwa ni fresh na ni kizuri kwa afya. Happy juicing!

=Unataka kuboresha afya ya mwili wako?  fanya mambo haya kwanza

=Kula kilicho safi na bora

 

2 COMMENTS

  1. Samahani mimi hupendi tumia Juice ya mboga ila sijui kama mchanganyiko nao tumia ni sawa… naendelea kuweka Mchicha,karoti,Tangawizi,limo,Hoho je ni sahihi ?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here