Unahitaji Kitu Gani?


1_pcpePaMcsMG1pWSowMjL6A-1024x576 Unahitaji  Kitu Gani?

Kitu gani ni vitamini C Yako? Unahitaji nini?  Zoezi: Kuza Nguvu yako ya ndani.

Kwa nini? 

Kila mtu ana matatizo yake. Ukiangalia wengi wana stress, magonjwa, kupoteza, mazingira magumu, Bila shaka ni mengi sana hasa katika kutafuta ukamilifu kwenye kuanzisha biashara mpya,  kulea familia,  Na Bado  kuna watoto wana changamoto .

 

Kwa Ajili ya kuponya ustawi na kukua kibinafsi,  kidogo inachukua muda mrefu ,lakini kuna kitu hapa kimenisaidia mimi, Naamini hata wewe kitakusaidia .

img_20170414_144434 Unahitaji  Kitu Gani?

 

Matatizo mengine ni kwenye uchumi , kulea wazazi, watoto shule, kazi ngumu au chuo, majirani wagomvi au matatizo ya kwenye mahusiano.

Matatizo mengine yapo kwenye mwili, kama maradhi, kuumia, kupata hali ngumu ya hisia zako na hormoni zako.

Matatizo mengine ni kwenye Akili. kama wasiwasi, Hali ya huzuni, Kutojithamini, kujikataa, maumivu ya kutokea kunyanyaswa ukiwa mdogo, Ulemavu , kuogopa kuongea kwenye watu wengi, uchungu wa kupoteza.

Bila shaka tatizo linaweza kuwa  baya , Kama vile  kuhisi hasira kuhusu kufanyiwa vibaya kazini kwako.

images Unahitaji  Kitu Gani?

Kwa kutibu hili tatizo unahitaji kushughulikia siku yako kuanzia asubuhi unapoamka. Angalia aina hizi mbili. mazingira magumu na changamoto zilizopo na chanzo chake.  Matatizo yanapozidi na chanzo kinazidi pia.

Kwa vipi?

Chanzo kinaweza kutokea kwenye Akili yako au Mwili wako au  Kwa walimwengu. Chanzo au Kiini au Mzizi ndio kitu ambacho unatakiwa kuangalia . Kwa mfano Afya njema  inaanzia ndani ya akili yako, Akili ikiwa safi mwili wako unakuwa safi. Mtu wa kushughulikia hali hii ni wewe sio mtu mwingine. Anza kwenye moyo wako, Akili yako Na Mwili wako.

Nitaangalia sana kwenye Sehemu ya Akili yako, sehemu inayoitwa inner strengths. Huku kunahusika sana mambo ya hisia. kwa mfano utulivu wa mtu, Hisia nzuri, kwa mfano Shukurani, upendo na huruma,Mitazamo yako hasa kwenye ujasiri, wema, hekima, juhudi. hivi ni vitu unatakiwa kuwa navyo ndani .

Vitu vingine vya muhimu ni kutembelea yatima, kufanya kazi ya Adamu, kufanya kazi ya Mungu, Kuwafanyia watu wema kama vile ambavyo wewe unataka kufanyiwa. kuishi na marafiki vizuri, majirani.

Ukitaka kukuza nguvu yako ya ndani, Ili kupata ufunguo wa kufungua mlango wa maisha mazuri ni lazima  kuangalia maswali yafuatayo .  Unaweza kutumia mwenyewe ili kuimarisha wengine ni vizuri kuwa na mtazamo mzuri wa kuwa mchunguzi, mwema kwa ajili yako na katika chanzo chako.

1.Suala ni kitu gani? 

Chukua hilo tatizo jaribu kuliweka wazi. Wakati mwingine maisha yanakera . Mara nyingi ni kweli, lakini haisaidii kitu kama utalenga kwenye chanzo au kwenye kutatua.

Kama tatizo lipo kwenye mazingira au mwili, tulia na urekebishe kisaikolojia. Wakati mwingine huwezi kufanya chochote  lakini huenda ukafahamu kilichosababisha.

2.Chanzo cha saikolojia ni kitu gani–nguvu ya ndani– kama ipo kwenye Akili itawezekana kusaidika? 

Huu ni ufunguo wa swali. Linaweza kuwa ni gumu kulijibu.

Vipi- kama umefikiria kitu fulani kupita kiasi, ingeweza kutatua  ?

Na kama ungekaa na kufikiri kama mtoto, haijalishi kulikuwa na ugumu gani, je ingesaidia na kuleta tofauti?

Kuangalia kwa undani zaidi, moyo wako unawaza nini?

Kitu kikubwa ni kuangalia chanzo cha nguvu ya ndani. Cha kwanza ni kuingiza Upendo.

3.Ungewezaje Kuwa na nguvu ya ndani? 

Hii ndio process ya Uponyaji.  Anza kwenye Moyo wako, Halafu Akili yako. Ubongo utakubali kila kinachotoka kwenye Akili yako. Mwili utapokea uponyaji wako.

Process ya uponyaji inanza na Maamuzi ya mtu mwenyewe.  Kama hutaweza kufanyia zoezi la badiliko  ndani yako hakuna mtu atakayeweza kukufanyia maamuzi hayo.

Ukijua vitamini C yako ni nini , nafikiri utatamani uwe nayo kila siku . Kwa hio kila ukiamka Amuru siku yako kwa kutumia muda wako vizuri. chagua vitu vya kufanya. Changanya   Taarifa unazopata na vitendo ili kupata uponyaji wako. Huwezi kufanikiwa kama wewe sio mtu wa kutafuta taarifa za kutosha.

Kwa hio Kitu cha muhimu ni kuchanganya Maneno, Namba ili upate Picha.

Kama chanzo hiki hakiwezi kufanya kazi kwako, au hakijawa clear kwako, Jitahidi kutafuta Kweli. Jijali. Jikubali, Jipende. Upendo unaanza ndani yako. Upendo ni kila kitu. Pendo ni Mungu mwenyewe.

Tafuta taarifa mahali sahihi. kutafuta pesa sio kupata taarifa. pesa ni pesa.kitu pekee ambacho kitakusaidia ni Kumkumbuka Mungu.

Subscribe.

Previous NURU YA MUDA ( THE LIGHT OF TIME)
Next Kitu Kimoja Ambacho Wanawake Huelewa Tofauti Kuhusu Wanaume

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.