Unahitaji Kuishi Sio kuwepo


Women laughing together outdoors
e180b229c0-mood-1024x512 Unahitaji Kuishi Sio kuwepo
ishi

Unastahili kuishi. Na zaidi ya hio , unastahili  kustawi. Kutabasamu. kucheka. Kupaa. Unahitaji na unastahili kuishi maisha marefu  yenye maana kamili sio maisha ya kujilaumu kila siku.

Ishi maisha yenye Upendo mwingi mwingi sana.

Najua kuwa unapambana . Unajiona kama huna thamani.  Kama vile maisha  kwako  hayahitaji furaha.  Nafahamu  kuwa unafikiri haya sio maisha yako, huwezi kuwa na maisha haya. Maisha amabayo yatakuletea furaha. Unafikiri kuwa  haustahili kupata tabasamu, unafikiri huhusiki kuwa na mapigo ya moyo.

Najua huenda upo kwenye maumivu makali.  Huna haja ya kuwa na huzuni . hakuna haja ya kusikia hivyo.  Huhitaji kulia kila siku usiku. Huhitaji kujiona kama kuna nafasi  imekosa mtu moyoni mwako.

Najua unafiki kuwa  bora kuwa na chochote sio hali uliyonayo sasa.

Najua unataka kukata tamaa. Unafikiria mwenyewe kuwa haifai kuwa hivyo.  Kwamba maumivu hayo na huzuni hizo hazitaondoka. Najua unataka kukomesha.Unataka kila kitu kiondoke. Unataka ulale moja kwa moja.

Lakini tafadhali , Fahamu kwamba, Huzuni hio ni ya muda tu. Maumivu hayo ni ya muda tu. Mateso hayo ni ya muda tu. Hayadumu milele.

Unastahili kuishi sio kuwepo. Unastahili kutabasamu. unahitaji furaha. Unahitaji kuwa na kila kitu ambacho maisha yanakupa wewe.

Maisha ni mazuri  sana, Unahitaji kutambua hili.

Wewe ni mzuri, Hata kama unaamini au huamini. Wewe ni mtu wa kipekee katika Ulimwengu huu.  Kwa hio tafadhali usije ukawa unafikiri tofauti. Usijaribu kufikiri kuwa hutakiwi kuishi.Unaishi na unapumua na  kupanda .

Usiache, usijikatie tamaa. Usiachie huzuni na maumivu yakutawale. Tazama msaada. Ongea na mtu ambaye unaona kabisa kuwa hawezi kukuhukumu, mpigie mtu fulani , sikiliza moyo wako. Pumua na utambue kuwa hata hili litapita tu.

Wewe ni Nuru lakini hujitambui tu.Lakini ipo siku utajitambua. Ipo siki hutasikia maumivu. Ipo siku utajikuta umeamka kwenye mikono salama ya mtu unayempenda. Siku hio utaona kwa nini ilikuwa ndio chaguo sahihi. Hukujikatia tamaa kwenye maisha yako. Ipo siku hutaacha kujiamini.

Vuta pumzi, Toka katembee mahali palipo na utulivu, sikiliza japo ndege wanavyoimba. Mpigie mtu unayempenda mwambie kila kitu.  Lia kama unahitaji. Lala na  ili kupumzika kiakili na kimwili. Sikiliza nyimbo nzuri za furaha. Jiambie Hata hili litapita tu.

Sio kila mara utajisikia hivyo. Sio kila mara utaona rangi ya blue.Kwa hio tafadhali, Endelea kupumua. endelea kutembea.  Endelea kupata vitu vipya. Endelea kupenda watu wapya. Endelea kutabasamu.

Kamwe usiache kumwamini Mungu.  Kamwe usiingie gizani . Tafuta Nuru .  Unastahili haya maisha. Unastahili kuwepo Ulimwenguni. Unastahili na ni mzuri na mwenye maisha ya kushangaza.Ipo siku, Natumaini Kuwa Unaamini hili.

 

Previous Siri Za Kudumisha Mahusiano Yako
Next Kufanya Ngono Bila Ufahamu Inaweza Kuumiza Mahusiano

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.