Unajihisi Uko Kwenye Umri Gani?


How-do-you-feel-about-yourself-when-you-look-in-the-mirror-300x300 Unajihisi Uko Kwenye Umri Gani?

Umri wa kubuni unaweza kuwa unajulikana zaidi kuliko umri wa kweli wa kuzaliwa.

Hujawahi kudanganya  kuhusu umri wako? mimi nimewahi  tena mara nyingi . Hata kwako jibu litakuwa Ndio. Na kwa kila mtu. Na ni kitu ambacho huwa kinaonekana wazi labda uwe na macho machanga usijue umri wa mtu.

Umri wa mtu wa kuzaliwa ule wa kweli sio wa kudanganya , unaweza  kuonekana kisaikolojia  kuwa ni kweli , kwa kwa sababu jinsi tunavyokua,  hatuwezi kujisikia kama tunazeeka  kama miaka inavyoonyesha kwenye kalenda.

Umri wa mtu ni kutokana na jinsi mtu anavyojisikia yeye mwenyewe, kama anajiona kuzeeka  basi atakuwa anazeeka hata nje ya moyo wake. Pia kama anajisikia kuwa bado hajazeeka , mara nyingi watu hawa huwa hawazeeki haraka , na hujisikia  ndani mwao wakiwa ni vijana  miaka 20  nyuma ya miaka yao ya kuzaliwa.

images-1-1 Unajihisi Uko Kwenye Umri Gani?

Kujisikia kijana kuliko miaka yako ya kuzaliwa ni dalili ya mtu kuwa na afya nzuri kiakili, kiroho na kimwili. Umri huu pia unatokana na kuwa na maisha mazuri, hali nzuri ya kiuchumi, ndoa nzuri, familia nzuri,  kazi nzuri,  na inaonyesha kuwa alitumia muda wake kwa akili, alikomboa wakati wake, hakujiingiza kwenye tamaa mbalimbali za ujana .

Wengi ukichunguza , watu ambao wako umri wa kati, hakuna ukweli wa miaqka yao ya kuzaliwa. lakini  wale kuanzia miaka 35 kushuka chini ndio watu wakweli , wanasema ukweli wa umri wao. Wale wengine wote wa miaka 35 kwenda juu asilimia 95 miaka yao  wanayotaja sio ya kweli.

Kwa hio kila mtu  jinsi anavyojisikia ndani yake , inakaribiana  kabisa na ukweli wa kisaikolojia   kwamba  inaleta matokeo ya ndani kuonekana nje,  ndivyo inavyoleta afya ya akili , kimwili na kiroho kuliko umri sahihi wa kuzaliwa.

betterlife-blog-16-300x300 Unajihisi Uko Kwenye Umri Gani?
It’s a race!

Huu ni uchunguzi ambao wanasayansi wamefanya. lakini hata mimi nimefanya uchunguzi nimeona ni kweli hali hio inatokea. Kama utajisikia ndani yako wewe ni mzee , utasababisha hata nje yako kuwa  mzee, pia afya yako kiakili, kimwili na kiroho inaharibika.

Nakupa mtihani kidogo. kama wewe unajisikia  kukata tamaa, unaona kama umepitwa na wakati,  acha mawazo hayo. rudisha umri wako miaka 10 au 20 nyuma, anza kujipenda, kujiheshimu, kujijaalia mwenyewe, utaanza kuona tofauti.

Ukichukua maua mawili , ukaanza kuyatamkia maneno tofauti, mfano ua moja unaliambia maneno mazuri ya upendo, kwamba unalipenda, kwa kuwa linanukia na linaleta baraka kwenye familia yako. Lakini ua la pili litamkie maneno mabaya ya kwamba , hulipendi kwa kuwa halinukii na linaleta balaa ndani ya familia, usiache kulitunza, litunzse huku unalitamkia maneno mabaya.

Nakupa muda mfupi hilo ua litakufa  japo unalitunza. lile lingine litaendelea kumea kutokana na maneno mazuri unayolitamkia. Fanya hilo jaribio, halafu naomba majibu  tafadhali.

Subscribe ili kutumiwa makala mpya mara kwa nara.

 

Previous Tabia Mpya.
Next Imani Inayofanya Kazi Ndani Ya Maisha Ya Mtu

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.