Usiseme Eti Kwa Sababu Mama Amepitia Mahusiano Mabaya Na Wewe …Hapana


picmwanaume Usiseme Eti Kwa Sababu Mama Amepitia Mahusiano Mabaya Na Wewe ...Hapana

Mama yako anaweza kuwa amepitia mahusiano ambayo hayakustahili kupitia. Hakujiona kuwa anastahili kupata  furaha  na amani kwenye mahusiano yake,

Kwa hio aliachia mtu amtese, amdharau, amtumie isivyo, aliruhusu  sumu hio iingie kwenye mahusiano  yatawale  maisha yake na alikuwa akiyaangalia jinsi hiohio.

Hata kama utamchukia mtu aliyemuumiza, lakini bado utaangalia na upande wa mama yako kuwa alikuwa hana ufahamu wa kutosha , Fahamu kwamba kwa kutokuelewa kwake ndiko kulileta maumivu hayo. hakujua thamani yake, upekee wake, nguvu yake  na ubora wake. Kitu ambacho kila mtu angekiona kwake ni ujasiri .

Lakini kama ukitazama mwanamke mwenye nguvu, smart, mzuri halafu amekubali  kukaa kwenye mahali ambapo haonyeshi thamani yake, inakufundisha somo. Inakufundisha kuinua kiwango chako, Inakufundisha kuondoa hali ya kukosa usalama, Inakufundisha kufikiri zaidi kwenye maisha yako.

Kuna mtu mwingine kwa sababu ya kuona mateso aliyopata mama yake, Sasa yuko huru. Kuanzia kwenye umri wake mapema, hataki  kutafuta mtu wa kumpa furaha,  Upendo ,Amani, anataka awe navyo yeye mwenyewe, Hataki kusubiri.

Kwa sababu ya mateso ambayo amepata mama yako unaweza kujaribu na kuona mahusiano ambayo sio sahihi , ambayo utaonyeshwa na bendera nyekundu, mtu mdanganyifu, anayekulisha sumu, utamfahamu aliye mkweli na mtu asiyeaminika.

Unaweza kutafuta  tu mtu mwingine ambaye anaishi katika mahusiano mazuri na ukajifunza kwake. lakini kipo kitu ambacho nataka ukijue. Mahusiano mazuri yanaanza na wewe mwenyewe. Ukiwa na mausiano mazuri ya kipekee, na ukiwa na mahusiano mazuri na Mungu. Utapata uongozi wa kiMungu katika maisha yako. Hakuna kitu utakachokosea.

Fikiri na kutazama huko nyuma, Mama alikuwa na mahusiano gani na Mungu, mbali na hio je Alijua kuwa ni lazima kuwa na mahusiano yake mwenyewe? Jibu ni Hakujua. Kwa hio wewe sasa ni mtu ambaye unafahamu. Unauelewa. Una taarifa za kutosha . Kama huna anza kutafuta taarifa nzuri za mahusiano kabla ya kuingia kwenye Jam.

Kila kitu kinahitaji maandalizi ya kutosha. Lakini ukikurupuka , ndio utaishi kama mama  alivyoishi kwa kutokufahamu. Usiseme Mahusiano ni mabaya. Mahusiano ni mazuri sana. Ndoa ni nzuri. Hata siku moja usiseme hicho kitu . Kama umewahi kusema anza TOBA mapema kabla hujaamua kuingia huko. Usijifungie mlango kwa maneno ya kinywa chako.

Uzima na mauti upo katika kinywa cha mtu. uwe makini na maneno unayoongea kila siku.

Watu wengi wanayaishi yale walioongea wakiwa  wadogo. Maisha ya mtu yanatokana na mawazo yake.

Share kwa wingi ili kusaidia wengine.

Subscribe kupata makala mpya.

Previous Kazi Nyingi, Pesa, Na Maisha Ambayo Nimejifunza 2017
Next Wakati Mwingine Mapenzi Ni Rahisi

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.