SOUL MATES.

wpid-man-and-woman-talking1 VITU VIZURI 60 VYA KUMWAMBIA MSICHANA UMPENDAE:

Ninamaanisha kuwa maneno matamu.Wakati kijana uko kwenye process ya kutafuta na kujaribu kuuteka moyo wa msichana, unatakiwa kujifunza  kutumia maneno matamu.Na lazima ujue kuwa sio kila neno  unalotumia litagusa moyo wa mwanamke unayemtaka,Lakini maneno matamu yanafanya kazi ya kushangaza .

Wakati vijana wengine wanalalamika kuwa ni vigumu kuuteka moyo wa msichana, jibu ni rahisi kwa sababu hawatumii maneno sahihi. watu wengi pia  huwa hawana maneno ya kusema na wengine hawajui kabisaaa hata jinsi ya kuanza.

sasa hebu tujifunze haya maneno ya kumwambia msichana unaempenda na unahitaji awe wako  milele.

1.Macho yako ni mazuri , yananifanya nipotelee kwako kila nikiyatizama.

2,Unanifanya niwe mwanaume bora , kwa hio nastahili  mapenzi yako.

3.Tumbo langu hutetemeka unapoleta mikono yako usoni pangu.

4.Wewe ni mzuri na ni mrembo  naogopa hata kukugusa naona kama nitakuchafua.

Kutafuta Mwenza Sahihi.

5.Unapotabasamu huzuni  kwangu hupotea , ghafla nakuwa mtu wa furaha.

6.Ungeweza kupata mwanaume yeyote duniani , lakini  umenichagua mimi.

7.Hapana.wewe sio mnene uko poa na ndivyo nipendavyo.

8.Ninapokushika nashisi kulegea kwenye magoti.

9.Wewe ni rafiki yangu, najifunza vitu vingi kwako,ndiye mtu ambae nimekuchagua, ndio mpenzi wa maisha yangu. ni wangu pekee, wewe ndio kila kitu kwangu.

10.Siamini , maana jinsi ulivyo amazing, lakini upo na mimi.

11.kila nikiangalia muda naona kama hautoshi kukupenda , natamani niwe na wewe milele. yaani wasife.

12.Umenifanya niamini kuwa zipo nafsi zinazoungana, zinazokutana pamoja.

13.Usiku nikiwa naangalia nyota na kuzilinganisha kila moja ili kuelewa ni kwa nini nakupenda,nilifanya vizuri hatimae nikazikimbia.

14.Kukutana nawe  ni kitu ambacho hakijawahi kutokea.

15.Unapoonyesha kunipenda, huwa nazidiwa na hisia , hapo hupotea kabisaaa.

16.Kabla ya kulala ni lazima kwanza nikupigie simu ndio nitapata usingizi.

17.Naweza kuwa nawe maisha yote, lakini bado nahisi kama  haitatosha  kukupenda.

18.Napata furaha nikiwa na wewe.

19. Napenda kutumia muda na wewe.

20.Napenda ngozi yako laini, ninapoigusa.

21.Natamani maishsa yangu yote nikuone ukiwa na furaha.Really-Sweet-Things-To-Say-To-A-Girl VITU VIZURI 60 VYA KUMWAMBIA MSICHANA UMPENDAE:                                       

22.Usibadilike nakupenda jinsi ulivyo.

23.Nikiwa na wewe nafurahi kama mtoto.

24.Napenda nywele zako.

25.Napenda nikukumbatie ninapokuaga.

26.Natamani kukubusu kila sehemu ya mwili wako.

27.Naanza siku na wewe ndani ya mawazo yangu, na ninamaliza  siku na wewe kwenye ndoto zangu.

28. ukiwa na mimi huwa natamani kusimamisha muda, maana muda unakwenda haraka.

29.Nikisikia sauti yako asubuhi , siku nzima ni mtu wa furaha.

30.Tabasamu lako zuri linanifanya niyeyuke.

31.Unaponiaga napata shida kukuruhusu uende.

32. Umenielewa vizuri, ni kama unasoma mawazo yangu.

33.Mungu alikupendelea kukuumba, akili na kila ulichonacho.

34.Najivunia kuwa na wewe na ninafurahia.

35.Napenda unavyosema unanipenda.

36.Mapenzi yetu ni kama mawimbi ya bahari,  wakati mwingi hutulia, na wakati mwingine huvuma,lakini yanarudi palepale.

37.mapenzi yetu yawe kama ua rose ambalo halina miiba.

38.Najua kwa nini watu wanatutazama , ni kwa sababu wewe ni mzuri kuliko mwezi.

39.Muda utakuwa hauna thamani endapo  sitatumia na wewe.

40.kama siku yangu ingeanza na busu lako, nisingehitaji kahawa.

41.Kama ningeambiwa nielezee rangi, basi ningeenda kwenye rangi za rainbow, kwa sababu wewe ni mzuri.ni wa muujiza.

42.Mimi bila wewe  ni  mbaya, lakini ni mzuri nikiwa na wewe.

43.Tukishikana mikono na mioyo yetu inashikana,na nafsi zetu zinapatana .

44.Siku ya kwanza tulipokutana, nilijua ipo siku tutakutana tena, na nafurahi imetokea.

45.Nafurahi tumekua pamoja, sina cha kukosa hata kidogo.

46.Moyo wangu unapumua kama ndege, kila unapotabasamu.

47.Kila ninapokuwa nimeshuka moyo, nikikusikia wewe moyo wangu unapata nguvu.

48.Shika mikono yangu nami nitashika moyo wako, tunza kwa maisha yote.

49.Maisha yote , milele yote,isio na mwisho, toka nimekutana na wewe maneno yote yana maana.

50.Siku naona kama mwaka, na  siku inapita kama sekunde.

51.Natamani ningekuwa  kama pweza mwenye mikono mingi ili nikukumbatie na mikono myote.

52.Siamini katika nafsi mpya, lakini baada ya kukutana na wewe nimeamini, natamani  kama ningeweza kurudi nyuma na kutengeneza kitu.

53.Sitaweza kukutoa kwenye mawazo yangu , kwa maana nakuhitaji uwepo.

54.Kuna wakati nahisi upweke, kwa wakati huo, basi huamua kukupigia simu  na kusikia sauti yako.

55.Ninapokutizama namuona mungu jinsi alivyokuumba na kukubariki.

56.Unanifanya niwe wa muhimu .

57.Ni siri ambayo inanifanya nikutazame  zaidi kwa kila siku.

58.Kuongea na wewe  kila siku unanifanya nikufahamu zaidi na zaidi.

59.Moyo wangu nakupa,nipe moyo wako ili tuifungie kwa pamoja, na tutupe ufunguo mbali.

60.Nakuhitaji muda wote, siku , mwaka na hata milele.

-maamuzi yapi yatakufanya ubadilishe maisha yako.

-tabia saba za wanandoa wenye furaha.

-dalili saba za kujua kama uko na mwenza sahihi.

 

shirikisha rafiki  na karibu kutoa mawazo yako.

 

 

 

45 COMMENTS

  • Assumani, Swali lako limehusisha vijana wengi, lakini nitajibu kwa nafsi yako pamoja na hao wengine wenye tatizo kama lako.
   Tatizo kubwa hapa ni kuwa huwezi kudhibiti fikra zako, Suluhisho ni moja tu uzingatiaji .
   Inaonekana hupendi hio hali na inakusumbua, lakini huwezi kudhibiti akili yako. ni vitu vya kawaida kwa kijana hasa kama umefikia umri wa mahitaji ya mwili. Jaribu kuongea na wasichana , pia jaribu kuingia kwenye mahusiano kama umri unaruhusu. Utaelewa kuwa hakuna umuhimu wa kufikiria.
   Kwa Msaada zaidi. tafuta muda wa dakika 30, asubuhi kwa ajili yako, Kaa kwa utulivu mahali ambapo hakuna usumbufu, Funika macho kawaida bila kulazimisha, Utaanza kuona giza, Fikra zitaanza kuja, zilizopita, zilizopo, na zijazo. Zitakuwa zinaiingia na kutoka.Usihangaike nazo na wala usiziingize, wazo lako ulilouliza nalo litakuja. Endelea kuyaangalia kama kutenga vyombo.
   Endelea na hili zoezi kila siku, kama unaweza fanya mara mbili kwa siku. Na kwa muda mfupi tu Utaona matokeo na pia Utaona Utofauti wako. Nakuhakikishia utapata matokeo bora.

 1. Comment:ni nzuri sana! mi kuna mdada nampenda sana da elizer lkn tumezoeana kuitana dada na kaka, lakini najikuta kushindwa kumueleza ukweli kwa mazoea tulozoeana ya kuitan kaka na dada,,,, je utanisaidiaje? au nifanye nini

  • Hasnuu nashukuru kwa swali lako, Ni kweli ni ngumu kidogo kwa hali kama hio. Lakini ukiweza kucheza na ubongo wake utweza. Na hapo kama tu unampenda kweli. Onyesha uhodari wako kwake, mfanye afurahi na kujiona ni wa kipekee inahitaji nguvu.
   Kwa mfano , anapokuwa na shida na kupata woga wa kitu fulani , usikae kimya, jitahidi kufahamu tatizo alilonalo kisha jaribu kulitatua kama inawezekana, pia mfanye ajisikie yuko kwenye hali nzuri. Lingine ni kuwa makini na mtazamo wako, mavazi unayovaa yawe ya kuvutia. Vaa jinsi nzuri na tisheti inayokukaa vizuri. ikiwezekana fanya mazoezi ya kuweka misuli kidogo kama huna misuli. uwe mcheshi kwake, usiwe na mazoea ya kuongea ongea na wanawake wengine mbele yake, msifie. pia jali sana utu wake kuliko mwonekano wake. msifie nywele zake, macho yake, mtindo wa mavazi yake.
   Mara nyingi wasichana hawana habari na wanachokitaka, kuwa gentlemen . mwache afanye atakacho . wewe onyesha kumjali sana .

  • Jean Chanja, Hofu, mashaka , woga , kutojiamini , Kutojikubali, kutojithamini , hivyo ni vitu vibaya. sio tu katika mahusiano , ni katika kila kitu unachofanya.
   Anza kujitazama ndani yako kama unaipenda nafsi yako, kama unampenda jirani yako, Kama Unampenda Mungu. Kama hujipendi ,hutaweza kumpenda jirani yako, hutaweza kumpenda Mungu. Lakini kama unaweza kujipenda na kuwapenda wengine ni rahisi Kumpenda Mungu.
   Kitu cha kukusaidia hapa . Anza zoezi la kujitamkia wewe kuwa unajipenda, jifanyie vitu vizuri, kula vizuri, kuwaza mema, kuwazia wengine mema, Unaweza ukaanza kusalimia kila mtu unayekutana naye kwa kutabasamu. kabla ya kumwambia huyo mpenzi wako unampenda uso kwa uso. onyesha upendo wako kwa vitendo. Kwa sababu kusema nakupenda ina njia nyingi. kama huwezi kutamka mbele yake onyesha vitendo. wakati huo huo unafanya zoezi la kujipenda mwenyewe, na kuwaambia ndugu zako unawapenda. Unaweza kumwambia baba , mama nakupenda. Ukifanya hivyo , utaanza kuona jinsi ilivyo rahisi kusema nakupenda mbele ya mpenzi wako. Na upendo huo uwe wa kweli sio upendo wa kutaka kitu.

 2. It’s so nice, tuna shukuru sana kwa msaada unayo tu tolea sisi wavijana, ila swali moya ina ni sumbua, lakini, kwa nini kila mara kijana aki tamani kumufikia msichana mara mingi ana shikwa na woga? Hasa kama msichana huyo ni mrembo sana.

  • Asante Maombi Mihiyo. Woga ni adui mkubwa kwenye kila mafanikio ya mtu. Lakini ukitaka kushinda woga katika eneo hilo ni vizuri kama utakuwa mtu wa kupenda kujifunza kutokana na makosa. Jikubali kwanza wewe, jithamini , ipende nafsi yako. soma hii itakusaidia. MBINU 7 ZINAZOMFANYA MWANAUME AONEKANE ANAVUTIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here