debt-ball-and-chain_featured Wakati Inapokuwa Vigumu Kujisamehe

Utawezaje kujisamehe mwenyewe aina ya msamaha ambao  hauwezekani?

Umefanya kosa fulani au umemuumiza mtu  mwingine au mwenyewe,  Na sasa unajisikia hasira, unajilaumu, unajiona una hatia, una huzuni, au unajisikia aibu.

Kama mtu mwingine amekukosea, ungehitaji akuombe msamaha, Na ungeamua  kumsamehe au kutomsamehe. Lakini unapokuwa umefanya makosa , Hatua hizo kwako hazipo wazi. Huenda huamini kuwa unahitaji kusamehewa, Au unafahamu lakini hujui jinsi gani ya kujisamehe, na unajisikia vibaya.

Utawezaje kujisamehe unapohisi kuwa haiwezekani?

Kitu cha kwanza ambacho nakutaka ukifanye ni wewe kufahamu jinsi ya kujikubali jinsi unavyojisikia sasa hivi.

Fahamu kwamba sio kila mtu mwenye kuwa makini au kuwa na uhakika  wa kukubali kwamba amekosea, Mara nyingi kila mtu hujiona kuwa yuko sahihi. Kubali kwamba wewe ni aina ya mtu huyo ambaye anaweza kulitambua kosa na kusema kuwa umehusika katika hilo. umefanya kitu kibaya, lakini ndani ya msingi wako , wewe ni mtu mzuri.

Kanuni za kujisamehe mwenyewe ni zile zile ambazo unawasamehe wengine. Unapomsamehe mtu au kujisamehe ni kuachilia . lakini sina maana ya kujifanya unasamehe kumbe ndani umeweka kinyongo Hapana. Msamaha sio udhuru au msamaha wa jujuu. na haina maana kwamba hutaweza kukumbuka. Kusamehe ni kukubaliana na yaliotokea na kupata njia ya kusonga mbele.

Kwenye ndoa na familia, wengi huwa wanafanya makosa ambayo ni  ngumu kusamehe. Yasiosameheka. Lakini kuna kitu kimoja ukumbuke kuwa wale waliofanya makosa yasioweza kusameheka na wale ambao wamefanya makosa rahisi kusameheka, wote wamefanya makosa.Wote ni wanadamu. Wanadamu wanafanya makosa. Yote ni makosa. Sisi ni viumbe ambao hatujakamilika, na wote tunahitaji kusamehewa.

Wote tunajitahidi kutumia mbinu mbalimbali ili kuepuka makosa. Wakati mwingine mbinu hizi hazitusaidii kitu, Wazazi wetu ndio kioo chetu, hawakuweza kufanya vizuri baadhi yao, mitazamo yetu na kujihukumu kwetu au imani zetu .Nakutaka ukae kimya kwa muda  na ujisemeshe hivi; ”Nimefanya nilichofanya kwa sababu mimi ni mwanadamu na mwanadamu sio mkamilifu

Kubali kilichotokea. Elewa jinsi gani na kwa nini kilitokea , Ona picha hio katika hali ya kuachilia. kusamehe, kiwe ni kizuri au kibaya.

Kujisamehe ni kuhitaji utulivu na kuwa na mtazamo mkubwa kwa kila kilichotokea. Umefanya na lazima ushughulikie matatizo yaliojitokeza na ukubali kuwa hutaweza kubadilisha hilo limefanyika na limepita.

Fikiria kuhusu kile kilichokufanya ufikie kutenda hivyo, ulikuwa unataka kukutana na kitu gani? Somo gani ambalo umejifunza hapo na huenda ulishaambiwa na wazazi wako. Kuna uzoefu wowote ulionao au imani yoyote?  Utakapojua Kwa nini umefanya ulichokifanya utakuwa tayari upo kwenye njia nzuri ya kujisamehe na utakutana na kile ambacho ulikihitaji .

Angalia kama kuna kitu kimekubadilisha, Umejifunza nini kutokana na hilo kosa, Utaboreshaje maisha yako.  Sema mwenyewe kama hivi kila siku , Nimejisamehe mwenyewe. Kwa makosa yangu na kujiruhusu kusonga mbele, Yaliopita yamepita , Natazama yajayo. 

Baada ya kuwasiliana peke yako na msamaha,  unaweza kuwasiliana hata na mwingine ambaye umemkosea kwa urahisi, kwa kuelewa na kuomba msamaha wa kweli. Utaweza kutafuta njia nzuri ya kufanya kitu fulani kwa mtu ambaye umemkosea kwa kumsaidia ili aweze kuboresha maisha yake. Jionyeshe mwenyewe na Ulimwengu ambao umejifunza kutokana na makosa.

Mwisho uje na mpango mzuri. Chukua somo ambalo umejifunza na ulifanyie kazi  kwa vitendo. Jiulize utafanyaje ili usirudie kosa?

Hakuna faida yoyote au kitu kizuri  kinachoweza kuja  kwako kama utabaki kwenye mtego huo wa kutojisamehe, Utajitesa na haitakusaidia wala kumsaidia mtu mwingine. Kwa ajili ya kusaidia wengine na kuyafanya maisha yako kuwa mazuri ni kuanza kujisamehe mwenyewe.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here