neworleans_2-1024x683 Wakati Thamani Inapokuwa Wazi Kwako, Kufanya Maamuni Inakuwa Rahisi.

Kufahamu thamani yangu imejaza sehemu kubwa ambayo ilikuwa inakosekana katika maisha yangu.

Thamani yako inakuonyesha jinsi ulivyo, Watu wengi hawaelewi  kiasi cha kutosha  jinsi ya kutambua thamani zao. Thamani yako inategemea matendo yako. Inajionyesha kwenye mazingira yako.  Na mahali unapoelekeza muda wako na nguvu zako katika maisha

Kwa mfano. Mtu mmoja ambaye ameweka nguvu kubwa kwenye kazi yake atakuwa anatumia  masaa ya zaidi , atakuwa anaboresha kazi yake. huenda katika kujitolea muda wa ziada  kuwa na familia yake na marafiki. mtu anayechagua thamani ya familia  husahau  thamani ya kazi yake . kwa sababu kila jioni na kila weekend atakuwa na familia yake. Kile unachokithamini  ndicho kinachosababisha  siku yako kuwa nzuri na maisha yako.

Unafahamu Thamani ipi ya kweli katika maisha yako na  watu wanaokuzunguka? Kama hujui,  unaweza kuwa ni mtu ambaye hana furaha  katika maisha yake na unahisi hujatosheka  na maisha uliyonayo. Na bado hujaweza kujiuliza kwa nini  unahisi hivyo.

couple_having_dinner Wakati Thamani Inapokuwa Wazi Kwako, Kufanya Maamuni Inakuwa Rahisi.

Kila mtu ni muhimu kufahamu thamani yake. Kwa sababu  watafiti wameonyesha kuwa kuna  thamani za aina nyingi ambazo zinaweza kukufanya uwe na furaha  na mwenye kutosheka katika maisha yako kwa muda mrefu. Lakini zipo thamani ambazo zinaweza kukuongoza  katika maisha yasio na utoshelevu.

Hapa chini nitaelezea  ni thamani zipi zina faida  ya muda mrefu  na zenye utoshelevu.

 Unachokithamini Kinakuamulia maisha yako

Nilipokuwa na miaka 20, nilitamani kuishi maisha ya kitajiri, maisha mazuri,  ya mtindo wa wakati ule. Nilipata thamani hio na kuishi kama nilivyotaka  kwa msingi huo huo niliotamani, Mazingira ya maisha yalibadilika baada ya matukio kadhaa kutokea.  badala ya kufocuss  kwenye muda wangu , nguvu na kusudi la maisha yangu  ili kutengeneza  utajiri uendelee, niliishia  kuendelea kuishi katika maisha mazuri kawaida. maisha ambayo nilifikiri niliyataka . Pamoja na kujiendelea kimasomo , lakini niliona bado sijatosheka. nilifahamu kuna kitu kinakosekana katika maisha yangu. Thamani yangu katika imani yangu niliitupa pembeni .

Nilipoamua kuachana na mume wangu nikiwa na miaka 30,  Nilitathimini upya thamani yangu. Nikaamua utajiri  hauna maana tena  kwenye list ya uthamani wa mtu.  Pia niliamua kwamba  Imani yangu  na familia yangu ndicho kiwe kipaumbele changu . Maisha yangu yalibadilika na niliona kutosheka zaidi ya kipimo.  Siishi tena kwenye nyumba za ghorofa kule beach,  lakini haijalishi nina imani na maisha yangu, na nina furaha ambayo sio ya kuitafuta kwa mtu au kwenye vitu.

antonchekhov1 Wakati Thamani Inapokuwa Wazi Kwako, Kufanya Maamuni Inakuwa Rahisi.

Nilikuwa nahisi kama kuna kitu kikubwa nakikosa katika maisha yangu. Kitu nilichokitambua  wakati nilipoamua kubadilisha maisha yangu nikiwa na umri huu wa miaka 30 ilikuwa ni  watafiti walionisaidia  kufanya maamuzi ya kupata maana  kupitia imani  na familia  na sio kazi  na utajiri.  Imenichuka miaka 10 kutambua hili.

Maisha ya Utoshelevu yanatokana na kilichopo ndani yako.

Watu wengi wanahangaika katika maisha yao yote kutafuta utoshelevu na kupata maana ya maisha. Utakuta mtu anaolewa au kuoa lakini  haelewi kwa nini  hatosheki na mume au mke mmoja. Ndugu utatafuta upungufu huo mpaka mwisho kama hutaelewa kiini cha hamu yako. Na hio yote inatoka katika kuchagua thamani ambayo inaleta maana ya maisha. Ona thamani yako kuwa ndio kitu cha msingi ili  ikupatie  utoshelevu  na maana katika maisha yako  ya  kudumu.  Au unafanya uamuzi wa  kuwa na furaha ya muda mfupi  na kujaza vitu vingi bila ya kutosheka navyo?

Watafiti na Wanasayansi walipima hivi vitu vitatu.  Furaha, Utoshelevu na  Maana ya maisha na  thamani, ili kujua kipi kinampa mtu  furaha katika maisha.  Waligundua kuwa , Mahusiano mazuri na yenye maana huwapa watu  furaha na utoshelevu  wa juu katika maisha ,  Kuongezeka kwa utajiri  haumpi mtu furaha  ya  kudumu.

Imani pia ina nafasi kubwa  na umuhimu mkubwa  katika maisha ya utoshelevu. katika kumwadumu Mungu  unaongeza  maisha ya utoshelevu na nguvu .

Mimi binafsi nafahamu kwamba  Imani yangu ndio imenipa utoshelevu mkubwa katika  maisha yangu na familia yangu imekuja sehemu ya pili. Watafiti wamegundua kuwa Msaada wa mahusiano ya ana kwa ana  na imani  ni njia nzuri ya kuongeza  kutosheka katika maisha ya kudumu. lakini kuongezeka kwa utajiri na vitu  au pesa haiongezi furaha ya kudumu. Pata maisha ya thamani kwa kujithamini wewe kwanza.

Faida za Kuelezea thamani yako.

Katika maisha yangu ya mwanzo  sikuwa nafahamu nini maana ya thamani.  Niliishi hivyo kutokana na uzoefu,  kuliko kuwa na ufahamu wa kutambua  na kufanya maamuzi yanayoleta thamani yangu. Hata hivyo,  sikuwa na ufahamu wowote wa kwa nini nilifanya maamuzi hayo . Ilikuwa ni mawazo yangu na hisia zangu tu ndio zilinilazimisha , zaidi ya kuwa na uelewa  wa kuwa na msingi  wenye thamani  kuwepo katika maisha yangu.

CKDdt0zWgAAEKqf Wakati Thamani Inapokuwa Wazi Kwako, Kufanya Maamuni Inakuwa Rahisi.

Watafiti wanasema kuwa watu wenye kufahamu thamani ya maisha yao  hawana stress ya maisha.

Kufahamu thamani yako hutaweza kuwa na stress , badala yake utatosheka na kila ulichonacho. kama ukifahamu hili utakuwa na njia tofauti,  utatambua thamani yako wazi .

Utawezaje kutambua thamani yako

Ni kutazama kitu kilicho na umuhimu katika maisha yako, hapo ndio utatambua thamani yako.

kwa mfano. Kazi, mafanikio, hamu, usawa, uzuri, umiliki, huruma, Elimu, Furaha, Afya, Ukweli, Heshima, Ucheshi, Wema, kujifunza, Uongozi, Upendo, uwazi,  Amani. Tabia nzuri, Siri, Uaminifu, Dini, Wajibu, usalama, Urahisi, uwezekano, kiroho,status,  shukurani, mila, upekee, maono, utajiri, hekima.

Hapo ndio utajua thamani yako iko kwenye nini japo sijaweka kila kitu.

Hapa kuna mifano ya imani ya kujithamini.

Unaweza kuanza kudhibitisha maneno ndani ya ubongo wako kila siku kwa kutamka kuwa

Nathamini Imani ,Nathamini upendo, nathamini uzuri nilionao, nathamini kazi yangu, nathamini maisha yangu,  nathamini  afya yangu, nguvu yangu, tabia yangu…… kila siku. itakuwa ni tabia , na kila kitu kitabadilika  na faida yake itaonekana. Fanya zoezi hilo kila siku. ni kama biashara yako.

Kama unathamini Afya yako, unatakiwa  kuanza kula vizuri, chakula sahihi kwa ajili yako, na iwe ni kipaumbele chako kila siku. fanya mazoezi kama unathamini mwili wako na akili yako. soma kila siku. fanya kitu kipya mara kwa mara.

Thamani itakuja kwako kama ukiwa unafanya zoezi hilo kila siku. Kuishi maisha ya kutosheka  ni deal kubwa  katika thamani  uliyonayo, weka akilini mwako na moyoni mwako kama kweli unataka kutambua thamani yako.

share kwa wengine. kisha Subscribe

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here