WANAUME WANAOBAKA WATOTO WANASABABISHA MAUAJI.


suicide-480 WANAUME WANAOBAKA WATOTO WANASABABISHA MAUAJI.

Msichana wa miaka 16 amejiua  baada ya kubakwa na baba yake  na akagundua kuwa ameambukizwa ukimwi, na si ukimwi tu bali na mimba juu.

Msichana huyo alibakwa na baba yake wa kambo huko katika mji wa Kisumu Kenya wakati mama yake alipoenda sokoni. Akamtishia kuwa akipiga kelele atamuua.

Baada ya kumbaka  huyo mtoto akamwambia endapo utamwambia  mama yako  au mtu yeyote akijua atamuua.

Kinachosikitisha zaidi  kilikuwa ni  kufahamu kuwa sio binti yake, na kwamba hapotezi kitu chochote, hata kama akimchinja  endapo atakwenda kinyume na alivyomtishia.

Msichana akawa anakumbuka matishio na akawa kimya bila ya kumwambia mtu yeyote pamoja na mama yake. Akaamua basi tu imeshakuwa.akifikiri ataendelea na maisha ya kawaida tena.

Na mambo yakawa kama kawaida wiki za kwanza, akawa anajitahidi kusahau  na kujaribu kuwa mtulivu na kuwa hodari shuleni, hakuna mtu aliegundua kitu kinachoendelea kwake mwisho wa wiki.

Baada ya wiki kadhaa kupita,msichana huyu mdogo akaanza kusikia dalili za mimba, akawa haelewi,lakini akawa anabuni, akakosa hedhi mwezi wa kwanza, akawa na homa pamoja na kutapika  bila kukoma.

Akawa anaogopa zaidi hata kuongea na mama yake, aliogopa kwamba kama akijaribu kuongea kuhusu kubakwa, asingeuwawa yeye  tu bali hata mama yake. Kwa hio badala yake, kwa siri alienda kwa  Tabibu, na dactari baada ya kusikia maelezo akatoa wazo la kupima mimba.

Matokeo yakaja ana mimba ya baba yake wa kambo.

Haikuishia hapo, Dactari akamuuliza kama ameolewa ama anajua mtu aliempa ujauzito, akajibu  kibinadamu, kama kukubali,dactari akamwambia kuwa inabidi mwanaume aje nae kupima kwa sababu  tayari binti alikuwa ameambukizwa virusi.

Alianza kulia  chumbani kwa dactari, akalia kwa sauti kwa muda mrefu. Na akaanza kumweleza dactari jinsi baba yake alivyombaka .

Msichana akaondoka kwa dactari baada ya dactari kumwambia kuwa maisha yataendelea vizuri tu hata kama umeambukizwa virusi vya ukimwi, utaishi.

IndiaTv883281_LoveJihad_Suicide WANAUME WANAOBAKA WATOTO WANASABABISHA MAUAJI.

Hata hivyo, masikini msichana hakuweza kufikiri kuwa angeweza kuishi akiwa na virusi vya ukimwi akaamua kujiua siku hio hio, tukio liliripotiwa  kwa polisi lakini kabla ya hukumu ingeweza kumsevu baba yake wa kambo kwa kile kilichogundulika kuwa haijulikani kwa nini kajiua. Kuhusu kuchunguza  ilikuja baadae.

Kutokana na ukatili huu wa kijinsia imegundulika kuwa , wengi wanaobakwa , au kufanyiwa ukatili huu , hawatoki mbali  mara nyingi ni wanaume wa karibu, inaweza ikawa ni  wazazi, family friends, majirani , ndugu.ndio wanasababisha ukatili huu.

Ukatili wa kijinsia ni ukikwaji wa haki za binadamu na ni lazima ukomeshwe duniani, si kwa mwanamke au msichana kupatwa na ukatili  wa kubakwa.

 

Previous NJIA 5 ZA UKWELI KUKUWEZESHA KUTAFAKARI KILA SIKU.
Next MASWALI 54 YA KUJARIBU UGUMU WA UBONGO NA KUJUA WEREVU WA WATU WAZIMA:

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.