WANAWAKE WATENDAJI NA WANAUME WATAZAMAJI


superiority-feature1-e1385832313774 WANAWAKE WATENDAJI NA WANAUME WATAZAMAJI

Umuhimu wa kuwa sambamba kwenye mahusiano.

Mwenza mmoja anapokuwa ni mtendaji , halafu mwingine anakuwa na mtazamaji au batili, mahusiano yatalega lega.Mwenza mtendaji  anakuwa na nguvu  zaidi.  Lakini hii haihusiani na jinsia

Nimegundua kuwa  wenza watendaji mara nyingi ni wanawake.  Wanawake watendaji  muda mwingi huwa na kazi zaidi ya moja  , pamoja na kazi za nyumbani  na kazi zake za  kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe.

Anaweza kuwa ni mshiriki wa vikundi vingi vya kijamii na kuwa na furaha kuzungukwa na watu. Si rahisi kumshutumu  kwa kuwa nyumbani kwa siku  kadhaa.  Mwanamke mtendaji anaweza kufanya kazi za nje na bado anarudi nyumbani kufanya kazi  za kupiga , kusafisha na mambo mengi yanayohusu  hapo  kwa wakati huo. Lakini mwanaume mtazamaji  anaweza kurudi kutoka kazini kwake na kukaa kwenye sofa , kuangalia luninga na kusoma  gazeti au kukaa na computer..

Unaweza ukakuta wanapata matatizo kwa sababu ya kukaa kwa muda mrefu na kusubiri tu kula.

Mama mmoja alisema , kila akimwambia watoke pamoja kwenda kutembea hataki, ina maana hataki kufanya mazoezi, anataka abaki hapo na kuangalia movie. Sio kitu kizuri kwa afya.

Wanawake wengine wanasema  wenza wao  hawako tayari kujishughulisha ili kupata kitu wanachokipenda , na mara nyingi  hawana  muda wa  kuwa kwenye vitu wavipendavyo. Ndio maana magonjwa yanawapata kwa haraka. Kwa sababu ya  kuwa na huzuni .

Mara ya kwanza  wanaume hawa huonyesha kuwa na nia ya kutaka kufikia malengo yao na nia zao, lakini baadae hubadilika na kuwa watu wa kukaa mara nyingi, na wanawake ndio wanakuwa watafutaji wakubwa.

Wanawake watendaji ni watu wa vitendo sio watu wa kuigiza , na hii ni  tabia yao , wengi wanatoka nazo kule kwao kutoka kwa wazazi wao , hasa wamama.  Ndio maana ni muhimu sana kwa wamama kuwa  active kwa ajili ya kuwafundisha  mabinti zao . Uwe model wa mtoto wako.

Kijana mmoja alisema , alikuwa akimuona baba yake mara nyingi akiwa mbele ya Luninga , wakati mama yake akifanya kazi nyingi. Hata mama yake akijitahidi kumsukuma anyanyuke pale haikuwezekana. Alikuwa ni mvivu.  Hata kama nikimrushia mpira hawezi kudaka  na kunirudishia.

Niliona baba yangu kama ni mzigo kwa mama, MAMA  alikuwa active muda wote.

Wanaume watendaji huwa  ni watulivu  na hushirikiana na wake zao.  Ni  watu wa vitendo sio waigizaji. Kwa hio  wanaume watendaji mara nyingi huwavutia nwanawake  watendaji pia. Na wenye nguvu kama zao. Ni watu wanaojali familia,  sio watazamaji. Na hawa  huwa wanapata ujasiri huu kwa kujifunza au kutoka kwa wazazi wao. Hushirikiana na wake zao kwa kila kazi , za nyumbani za ofisini na za kwenye jamii inayowazunguka.

Kwa kifupi mtu akiwa ni  mtenda kazi ni tiba kwa  mahusiano yao. Mwenza mtendaji huwa na  maono makubwa, hata kama kuna dhoruba inakuja , ana uwezo wa kukabiliana nayo. Lakini wenza wale ambao ni watazamaji , wakati dhoruba inapokuja  wanakuwa hawako tayari,  utawaona kama wameamushwa kutoka usingizini, na hio ni tabia  sio kuigiza.

Mara nyingi hawa wenza watazamaji  hujikuta wanaangukia kwenye matatizo ya  misongo ya mawazo  na kuwa waathirika wa magonjwa   kama ya moyo, na kisukari.

Ni muhimu watu kuwa makini wakati wanapochagua watu wa kuwaoa. Na watu wanaotaka kudumu nao kwenye mahusiano. Umri nao ni muhimu kuangalia. Kwa mfano   unaweza kumuoa mwanamke ambaye bado hajakomaa kiakili au mwanaume ambaye hana malengo.

Mazingira mengine ambayo ni magumu kwa wanandoa ni  pale  panapokosekana hisia za kimwili na  ufahamu unapokuwa ni mdogo au hakuna kabisa. Tiba itahusika.  Jinsi ya  kuweza kumrudisha mwingine kwenye hali ya kawaida  , ya kuwa active kwenye baadhi ya maeneo . Hasa katika kutekeleza malengo.

Washirikishe na wengine .

Previous MBINU 3 ZA KUKUSAIDIA KUSEMA HAPANA PANAPOHITAJIKA KUSEMA HIVYO
Next NGUVU YA KUJIONDOA KWENYE HALI YA UATHIRIKA

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.