Watu 10 Wabaya Zaidi Kanisani Kwako


images Watu 10  Wabaya Zaidi Kanisani Kwako

Watu wabaya zaidi kanisani kwako inaweza ikawa sio wale ambao unawafikiria kichwani mwako. Kusema kweli , wanaweza kuwa ni wa muda kwa muda, pamoja na wewe.

Watu wote wamejiweka katika utakatifu, lakini bado wana safari ndefu ya  kujitambua  na kufanyia kazi imani zao, utii wao na utakatifu wao.

Nimeona tabia nyingi sana kanisani hata wewe nafikiri umeona pia.

1.Mafarisayo.

Katika kanisa kuna mafarisayo. watu hawa Yesu aliwaita Wanafiki.  watu ambao wanajifanya ni wakweli lakini ni waongo.  Wanawahukumu wengine  kwa kila kitu, wanajisahau nafsi zao jinsi zilivyo . wanawatishia wengine  kwa maneno yao ya uongo.

2.Walimu wa Uongo.

Walimu wa uongo wapo makanisani, wanaeneza uongo.  wako Kimungu , lakini  mafunzo yao  hayana  ufahamu  katika kuwaponya watu. ni wadanganyifu na  waongo. lakini wewe unatakiwa kuwa makini kujua ni wapi ambapo kuna ukweli.

3.Wazinzi.

Kuna hali hii inaendelea ndani ya watu waliopo kanisani . Watu wanajihesabia haki. Paulo aliwaambia Wakorintho kuwa ni bora kila mtu awe na mke wake mwenyewe, mume wake mwenyewe, kama hawezi kujizuia. lakini zinaa imekatazwa kabisa.

4.Wenye Kujitoa

watu ambao wanasaidia wengine , watu wenye upendo wa kweli, wenye kushika maagizo ya Mungu. ambao wanaufuata msalaba kweli.

5.Mapigano.

Ni kitu gani kinasababisha watu wasielewane, wapigane, Sababu za mapigano ni nyingi, ikiwepo umbea, kuseng’enya, Wivu, . ila unatakiwa kukataa maswali ya wapumbafu yasio na ufahamu, ukijua ya kuwa hayo yanazaa magomvi.

6.Wajinga

Wajinga wote hawataki kupata hekima, wanakataa maarifa , wanadharau mafundisho, wanafanya vitu vya kijinga. Hawatambui mabaya, wamekataa kuelewa. Wanaamini vitu vya kuonekana, wanataka hela. Hawajifunzi kutokana na makosa yao

Ujinga wao unaweza kuwa ni mkubwa kupitiliza. Matokeo ya wajinga hawawezi kutumia uwezo ambao Mungu amewapa kwa sababu  Ni Wajinga. Paulo alisema, Kuwa makini katika kutembea kwako. Usitembee kama mtu asiye na Hekima, lakini  uwe ni mtu wa Hekima.

7.Wenye Hofu.

Kuna ile ambayo  inasema kumcha bwana ni mwanzo wa Hekima  na kumjua  mtakatifu ni ufahamu. Lakini kuna hofu ya mwanadamu. kuogopa kiasi cha kutojithamini, kuwanyenyekea sana wanadamu kuliko Mungu. hio ni hofu mbaya.

8.Wasio Na Imani

Paulo ameandika , Bila imani huwezi kumpendeza Mungu. Kuna watu wapo  ambao hawana Imani . Unaweza kwenda kanisani kila Jumapili Lakini hata hukuzi imani yako. Imani haina mizizi.

Nimekuwa nikijiuliza peke yangu. Lini mara ya mwisho  nimefanya au kuomba kwa imani? Ukweli ni kwamba sikumwamini Mungu kwa ukubwa alionao.Huenda ni vitu visivyowezekana. Vitu vilivyo salama . Mungu anaangalia Imani yako ipo kiasi gani.

9.Wabinafsi

Kila mtu asijiangalie nafsi yake tu, bali akumbuke  kuangalia na wengine katika yale anayopenda kutendewa yeye , awatendee na wengine. kuna watu hujiona wenyewe ndio sahihi lakini wengine sio sahihi. wanapenda kujionyesha kuwa wao wana kila kitu, wao ndio wanajua sana.  Utakuta watu hawa wanabadilisha makanisa kwa sababu ya mawazo yao mabaya.

10.Wanaojionyesha.

Wanaweza wasiwe wabaya, wanaweza kuonyesha upendo na wema.Lakini kwa kujionyesha.

Si kila mtu aitaye Bwana Bwana  ataweza kuwa mtu mzuri. Watu hawa wanaweza kusema kuwa ni wazuri lakini bado wapo gizani. wanaitwa waliopotea. Habari nzuri ni hii. Yesu alikuja kwa ajili ya watu waliopotea.  Hata kwenye kanisa pia.

Mungu anataka Msamaha wake uwe wa kweli kwa watu wote, uhuru kwa kila mtu, Neema  kwa kila mtu, kusamehe, Kuwa mwaminifu na kupendana kila mmoja.

Lakini miujiza ya Mungu . Anainua watu kwa ajili ya kufungua akili wengine  ili waweze kubadilika  na kujitambua ili waishi kwa ukamilifu wa Mungu. Kwa kusudu la Mungu na Utukufu wa Mungu.

Kama umependa makala hii , washirikishe wengine.

Subscribe kupata makala mpya kila mara.

Mungu Akubariki.

Previous Kwa Yeyote Ambaye Anapata Taabu Kujikubali
Next Tatizo Kubwa Ni Kujiona Uko Sahihi Kila Mara

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.