About


Hi, mimi ni Elizabeth, nilizaliwa mkoani SINGIDA ,nina familia  nzuri na watoto watatu nina marafiki  wazuri ,ninaishi Dar es salaam Tanzania. mimi sio maarufu ,na ni mtu wa kawaida   ,nafanya kazi na pia ni mjasiriamali. nimejifunza mengi ndani ya mtandao , na nimeona vema  nianze  kukujuza nawe  pia .moyo wangu unatamani kukuhamasisha wewe  uishi  maisha  mazuri yenye  maana kamili. yaani  maisha ya utoshelevu.

Maa-1-300x200 About

Ninawaonea wivu mkubwa watu wanaofikiria sana, wabunifu wa vitu mbalimbali,wanaoaandika vitabu ,wanaoishi vizuri, wanaoona fursa  katika maisha, wale wanaopenda zaidi yangu, ambao wanaishi kwa kutimiza  kusudi . hawa ni watu  ambao wanajua maana ya maisha. nawapenda sana .

ZAIDI KUHUSU MIMI

Nikiwa nimekaa nyumbani  kwa muda mrefu sana  bila kufanya kazi,  nilichoka  nikawa kama mgonjwa . nikaamua kutafuta kazi , kazi ya kwanza  nilifanya kazi  katika  kampuni moja ya gapco kama  cashier , kukusanya pesa za mauzo yote kwa siku , wakati mwingine napata shoti  , nakatwa mshahara , kiwango cha mshahara kilikuwa  TSH 80,000 kwa mwezi.

baada ya muda nilienda kusomea kozi ya  uuzaji wa luku  , kipindi hicho  ndio kwanza mambo ya luku yalikuwa bado mageni,  nilisoma  mwezi mmoja tu nikaanza kuuza luku.  mshahara ukawa kama 120,000/= .

Baada ya miaka miwili nilipata kazi  sehemu nyingine kama Meneja  katika hoteli moja  hapa Dar es salaam   na mshahara ukawa   350,000/= nilifanya miaka miwili pia ,

nilichoka kufanya kazi ya kutwa nzima bila mapumziko ,halafu bado mshahara  hautoshi, nikaamua kupumzika hio kazi , nikaenda  kujitolea katika kampuni moja   ambayo ilikuwa inafundisha ujasiria mali ,pale niliona nitajifunza zaidi njia mbalimbali za kufanikiwa katika biashara badala ya kuhangaika kuajiriwa  na watu kwa mshahara ambao hata  hautoshi.

baada ya muda nikawa msaidizi wa muhasibu  pale  ,nasaidia akiwa hayupo  napokea pesa , napeleka Banki , kila siku kwa sababu  ya uaminifu   , nikawa naandika  hata risiti  ,nafundisha watu njia ya ujasiria mali  . kwa sababu ya kumwamini Bosi wetu  , walituamini hata wafanyakazi wake.

Nilidumu pale zaidi ya mwaka ,wakaanzisha kampuni nyingine nami nikajitosa kuwa moja wa  wakurugenzi .sio tu mkurugenzi ,nikachaguliwa kuwa mkurugenzi wa pesa ( director of  finance) .tukaenda zaidi ya miaka mitatu , tukasambaratika . haikuwa rahisi kwangu  kuamini narudi tena chini.

BIASHARA  NDOGONDOGO.

Nilianza kuuza karanga , ubuyu, viungo mbalimbali vya chai,soya ,unga wa lishe na vitenge vya kukopesha ,wakati mwingine niliingia kwenye mitumba  ilimradi nipate pesa  maana niingia kwenye vikoba  , nilikuwa nabeba mzigo mkubwa sana  natembea kama uonavyo wauza   mitumba wanavyozunguka, maana ilkuwa  ni lazima niingize walau   Sh. 30,000 kwa siku,.

siku moja nilichoka , nilikata tamaa , nikamwomba mungu kazi  , Mungu akanipa kazi ya kulipwa kwa mwezi.

huku nikiwa naendelea na biashara yangu  ya ujasiriamali.

 

Thank youuu.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.