Barua Ya Wazi Kwa Mwanaume Ambae Nitampenda


Mid adult couple on armchair in new home
black-couple-moving-in-together-1024x512 Barua Ya Wazi Kwa Mwanaume Ambae Nitampenda
nitafurahia mikononi mwako.

Kwako mpendwa,

Nafahamu umekuwa ukinisubiri  nifike kwako, kwa ajili yetu , tuweze kukutana. Kwa ajili ya ndoto yako iweze kuwa ya uhakika, Kwa ajili ya kuamini nguvu ya maombi  tena, lakini tafadhali elewa kuwa kwa nini inachukua muda mrefu.

Bado kuna mambo mengi ya kujifunza kwa ajili ya kukua kiakili. Nahitaji kujitambua kwanza vizuri;Nikiwa na nguvu na nikiwa na udhaifu, kitu ambacho kinahitajika sana. Kitu kinachonifurahisha , ni Msukumo , matarajio na malengo yangu binafsi. Hakuna mashaka, Nitakabiliana na matatizo na nitapata maumivu, nitakapokutana na wewe nitakuwa mwenye ujasiri na nitakuwa niko tayari  kukabiliana na changamoto zote za maisha nikiwa na wewe.

Tafadhali Endelea kuwa na Imani. Amini juu ya uzuri wa watu. Usiweke ukuta pindi  unapokutana na  mtu usiempenda.Huenda wakawa hawana matarajio kama uliyo nayo, Lakini nani ajuaye, Huenda wakawa ni wazuri na wenye moyo mwema.Wape nafasi, Jifunze kuwasikiliza.uwepo kila wanapokuhitaji. Bila shaka,  jitahidi kuwatambua na kuwaelewa mapema  maana kuna wale ambao hujifanya watakatifu usoni lakini ndani ni beast.Wajaribu, jilinde mwenyewe.

Sitaki tuwe wategemezi wa dunia hii bali tuwe watoaji, wachangiaji na wafanya kazi  wazuri, kuwasaidia wenye mahitaji,  kuwasaidia kujijua uhalisia wao , na hapo tutakuwa tunajijali sisi wenyewe; hapo ni njia ya kubadilisha jamii na kuwa na maendeleo ya kweli.

Safiri. Nataka pia wewe Ujaribu kusafiri, ujifunze mambo mbalimbali, Jifunze kujipenda, jijali, na ujikubali jinsi ulivyo. jifunze mambo mapya ,lugha mpya ukiweza,  Piga picha na watu mbalimbali ukiwa na furaha. Ili mioyo yetu ikikutana siku hio tuweze kushirikishana uzoefu na kujifunza kwa kila mtu alichonacho.

Nitakushikilia mkono wako. Tutacheka pamoja na kulia pamoja na kuogopa pamoja . Na tutanunua mahindi ya popcorn tutengeneze pamoja, tutapika chakula kizuri pamoja . tutatembelea jumba la  makumbusho pamoja,  na kuona jinsi watu walivyochorwa,  vitu mbalimbali ambavyo vilikuwepo kabla yetu. Tutaimba nyimbo nzuri pamoja. ikiwezekana kila mahali tutakuwepo pamoja. Naahidi kuwa mshirika wako kila mahali.  Rafiki wa kweli wa kimapenzi. ni wewe tu na mimi.

Furahia Maisha yako. Nataka ufurahie kila dakika ya maisha yako. kuwa mtawala wa mawazo yako.  pata kikombe cha kahawa kama unapenda. Kuna siku tutapata kikombe cha kahawa pamoja na kufurahia maisha pamoja.

Popote ulipo , Nafahamu unafikiria kuhusu mimi.

Unafikiria jinsi tunavyotembea pamoja nyakati za jioni, kwa kushikana mikono yetu kwa upendo. Ipo siku, tutafika kwenye nyumba yetu kwa mikono yetu.

Kwa wakati huu unapotaka kukata tamaa,  unapojihisi kama haupo duniani,  nitaonekana sio kwa gauni zuri ambalo unafikiria,  sio kwa majibu ya wasiwasi wako,  sio kama mcheza ngoma,  Nitaonekana muda ambao hukutegemea.  Utatambua kuwa nimeonekana, kwa kuwa sitakukatia tamaa hata kama utaweka ukuta wa aina gani. utafahamu kua ndio mimi ambaye ulikuwa unanisubiri kwa sababu hutakuwa na mashaka kutokana na ukweli  na upendo wangu kwako. Na halafu nitaonyesha haya kwako na utaelewa  kuwa ndio wakati.

Hutakuwa peke yako tena.

Wako mwaminifu

Mwanamke wako.

 

Previous Kama Kweli Yuko Ndani Yako, Angeweza Kuwa Na Muda Na Wewe
Next Jinsi Ya Kuepukana Na Lawama Kwa Zoezi La Kila Siku

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.