Fahamu Mbinu 5 Za Kumwabudu Mungu?


How-to-Worship-God Fahamu Mbinu 5 Za Kumwabudu Mungu?Yeye ni sababu ya kila kitu.

Mungu ni Nuru.

Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake , Viko kwa uweza wake. Tena vinarejea kwake.Utukufu una yeye hata milele.

Hakuna giza lolote ndani yako , ikiwa unampenda Mungu huku bado uko gizani, Utasema uongo, wala kweli haimo ndani yako.

Bali ukiwa ndani ya Nuru kama yeye alivyo nuru, utashirikiana na wengine kwa Damu ya Yesu na kusafishwa dhambi yote.

Mtu anayesema yuko  Nuruni naye anamchukia ndugu yake, bado yumo gizani hata sasa.Kila amchukiae ndugu yake ni muuaji. Muuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.

Yesu ni mwana wa Mungu. Anayeamini kuwa Yesu ni mwana wa Mungu ameshinda Ulimwengu.

Utukufu Wa Mungu Ni Nini?

Ni kujua Mungu ni nani?

Ni Umuhimu wa asili yake

Nguvu zake

Uwepo wake

Mazuri yote ya ndani na nje na sifa zake.

Utukufu wa Mungu upo kila mahali, tazama vitu vinavyokuzunguka.

Utukufu ulianza kuonekana huko bustanini. Bustani ya Edeni, kwa Musa, kwenye .Upendo, Kupitia yesu. mahekalu.

Worship-for-ourselves Fahamu Mbinu 5 Za Kumwabudu Mungu?

Mbinu Za Kumwabudu Mungu.

1.Mtindo wa maisha ya kumfurahia Mungu,

kumpenda Mungu, kujitoa wenyewe kutumikia kusudi lake,  kutumia mwili wako wote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

2.Kwa Kuwapenda Wengine.

Ni wajibu wako kujifunza kuwapenda wengine. wala usiifuatishe namna ya Dunia hii, bali ugeuzwe upya nia yako, upate kujua hakika mapenzi ya Mungu yalio mema, ya ukamilifu na kumpendeza. ndipo utakapokuwa ndani ya familia ya Mungu na Yesu kristo ni kiongozi wa familia. Ibilisi hana familia, bali ana kambi. Jipime uko ndani ya familia au uko kambini?

3.Kwa kukua kiroho kama Jesus.

kwa kufikiri, kuhisi, kutenda, kusikia.

4.Kwa kuwatumikia wengine.

Tumia uwezo ulio nao, zawadi uliyopewa na Mungu, Ujuzi ulionao, kipawa ulichonacho kwa ajili ya wengine.

5.Kwa kuwaambia wengine Kuhusu Mungu.

Mfundishe mtu Upendo wa Mungu. Yeye hapendi ufiche Upendo wake pale unapokuwa umejua Kweli, mwambie na mwingine.

99997-Joyce-Meyer-Quote-We-worship-God-with-our-entire-life-with-every-1024x576 Fahamu Mbinu 5 Za Kumwabudu Mungu?

Kumwabudu Mungu sio kwa faida yako, ni kwa faida ya Mungu. Usichukulie kama ni sehemu ya maisha yako. bali iwe ni  MAISHA  Yako. kumwabudu Mungu ni zaidi ya Nyimbo, muziki,

Kumpendeza Mungu inaitwa kumwabudu Mungu. Kumfurahisha Mungu ni kumwabudu Mungu. Tendo lolote la utii ni la kumwabudu Mungu. Shukurani pia ni kumwabudu Mungu.

Mungu wangu akubadilishe , ujue namna ya kumwabudu yeye peke yake.

Mungu akubariki unapoendelea kujifunza na mimi.

Subscribe.

 

Previous Sheria Ya Upendo
Next Masharti 10 Ya Mafanikio Katika Biashara Na Maisha.

No Comment

Leave a reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.